Tonny Ngombale Mwiru afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Wanaanza kumshughulikia mzee wa watu. Kwa nini toka 2008 kesi haijasikika mpaka isikike leo baada ya Kingunge ku-align na EL
 
Jamani Mzee Kingunge si ndiye mshauri wa msuala ya siasa JK kule Ikulu?
Has Kingunge fallen out with JK?Aafu haonekani tena kwenye majukwaa.
Ukichanganya na la kuondolewa Bashe(mtu wa RA) picha fulani inajito

keza
Kingunge alitukana mamba kabla ya kuvukia mto. Jamaa watamshughulikia mpaka akome. Na ile biashara ya parking anaenda kunyang'anywa. Biashara ya sembe inayosimamiwa na Kinje iko mashakani nayo.
 
du! ccm wabaya sana ukiwasapoti uozo wao unaonekana mwema siku ukiwa changanya wanakupiga kama hawakujui
 
Mzee wetu anao watoto wenginf kwa wale watu wa 70's na 80's mtaelewa.akiwa mkuu wa mkoa Mbeya alikuwa na mke mkubwa watoto wake mmoja alikuwa anaitwa Muya.kawaida small house ina nguvu.
 
Kingunge amelikoroga, wakimaliza kwa Tonny, watakuja kwa Kinjekitile Zungu la unga!
 
Hii kesi mbona ya 2008. Ilikuweje hadi isubili uteuzi wa Mgombea kupitia CCM?

Kwa maana hiyo CCM na Polisi hulinda na huwafahamu wezi! Ila wakipingana nanyi tu mnawatia ndani?
 
Hii kesi mbona ya 2008. Ilikuweje hadi isubili uteuzi wa Mgombea kupitia CCM?

Kwa maana hiyo CCM na Polisi hulinda na huwafahamu wezi! Ila wakipingana nanyi tu mnawatia ndani?
Hii post inachanganya watu tu, habari hii ni ya zamani imeletwa humu zamani sana kuna mtu tu ameifufua
 
Agosti 18 mwaka 2010 gazeti la Tanzania Daima liliripoti kuwa mtoto wa mwanasiasa Mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Tonny Mwiru alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na makosa manne ya kula njama, kuwasilisha nyaraka za uongo, kughushi na kujipatia sh. 424 kwa njia ya udanganyifu.

Ilidaiwa Tonny Mwiru na wenzalke waliwasilisha nyaraka za uongo katika Kampuni ya SCI(Tz)Ltd na kujipatia sh. 424,488,799.29.

Aidha ilidaiwa kuwa Tonny aligushi maombi ya ujumbe kasi wa kuhamisha fedha wenye namba 17 wa Agosti 27 mwaka 2008 kwa nia ya kuonesha ujumbe huo ni halali na ulitolewa na SAVISHANKAR RESMAN ambaye ni Mkurugenzi wa SCI(TZ) Ltd wakati kosa la tatu la ambalo TONNY alitenda ni kuwasilisha nyaraka 2008 katika Benki ya Barclays (TZ) iliyoko mtaa wa Ohio jijini ambapo aliwasilisha nyaraka za uongo ambazo ni fomu ya maombi ya ujumbe kasi yenye namba E7 kwa mfanyakazi wa benki hiyo, BITUN CHIZA. Shitaka la nne la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo ilidaiwa kuwa Oktoba 9, mwaka 2008, katika Benki ya CRDB , Tawi la Kijitonyama, alijipatia kiasi hicho kupitia akaunti namba 01j014293000 akionesha Kampuni ya SCI(TZ)Ltd imeidhinisha ilipe kiasi hicho cha fedha kwa Kampuni ya TEMM POWER LTD.

Dhamana kwa TONNY Mwiru, ilizua utata Mahakamani hali iliyopelekea mawakili wa Serikali waseme walikusudia kukatia rufaa masharti ya dhamana hiyo Mahakama Kuu haraka iwezekanavyo. Mawakili hao walisema Masharti ya dhamana hiyo yalikwenda kinyume na masharti ya dhamana yaliyoainishwa kwenye kifungu cha 148(5)(e) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ambapo kifungu hicho kinasema Mshtakiwa yeyote anaye kabiliwa na makosa ya fedha taslimu au mali ambazo zinazidi thamani ya shiingi milioni moja basi mshtakiwa huyo atapaswa awasilishe nusu ya fedha taslimu au hati ya mali yenye nusu ya thamani hiyo na si vinginevyo.

kwa mujibu wa taarifa hiyo, TONNY KINGUNGE NGOMBALE MWIRU alikuwa anakabiliwa na makosa ya kujipatia Tsh. Mil.424 lakini Masharti ya dhamana yalikuwa ni sh.20 tu.

Utata wa masharti ya dhamana hiyo ulipelekea Mwenykiti wa Chama cha siasa cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila atoea ya moyoni kama kawaida yake na hii hapa ni nukuu ya kile alichokisema: "Au huyo TONNY ni kwa sababu ni mtoto wa Mzee KINGUNGE ndiyo maana Hakimu alibabaika na kujikuta anatoa Masharti yanatokinzana na kifungu cha 148(5)(e) cha Sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 2002?

Au inapofika watoto wa vigogo kuvuruzwa Mahakamani ndiyo basi baadhi ya Mahakimu wetu wanaamua kupindisha sheria makusudi?"
Mwisho wa kunukuu.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, kabla ya Hakimu MIRUMBE kutoa Masharti ya dhamana hiyo alimtazama usoni Tonny sekunde kadhaa na kisha alimuuliza kama Mzee KINGUNGE NGOMBALE MWIRU ni baba yake, ambapo alijibu kiwa ndiyo.

Hali hii ilijenga mazingira ya sababu za kiwepo kwa utata wa Masharti ya dhamana kwa bwana TONNY KONGINGE NGOMBALE MWIRU ambaye alikuwa anatuhumiwa kujipatia kwa njia ya udanganyifu zaidi sh. Mil.420 ambapo kwa mujibu wa kifungu cha 148(5)(e) ch sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai alipaswa kutoa fedha au mali yenye thamani ya sh. Mil. 210 na siyo mil.20.

Kwa wale wanaojua mwisho wa kesi hii ulikuwa vipi, atujuze.
 
Kingunge anao watoto wengine zaidi ya Kinje, yuko mwanamke mmoja hapo Dodoma.
 
Back
Top Bottom