Elections 2010 Tomorrow people je watanzania tuko tayari?

Je watanzania tuko tayari?

  • ndio

    Votes: 0 0.0%
  • sijui

    Votes: 0 0.0%
  • labda

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    1

idrismkindi

Member
Oct 1, 2007
10
1
Watanzania uchaguzi umewadia ila nashindwa kuuliza kama tumejitayarisha kwani hata mwenyewe bado nina maswali. Uchaguzi huu naufananisha na ile nyimbo inayoitwa “Tomorrow people” ni kama muimbaji aliimba mahsusi kwa ajili ya Tanzania kwenye chorus anasema, nanukuu “Tomorrow people, where is your past? Tomorrow people, how long will you last? Je? How long will we last watanzania? Na pia anaendelea “If there is no love in your heart - so sorry

Then there is no hope for you - true, true” No love No hope. Watu hatupendani sababu tu ya vyama, eti ni wapinzani hata harusi hatualikani, misiba hatuliwazani ukiuliza unaambiwa eti baba wa bwana harusi CUF au yule marehemu ni CUF bwana? CUF ni ya nani kama si watanzania wenzetu? Kama hatuna Love then hatuna Hope. Na baadae tunamaliza eti tunahitaji kuitengeneza kesho kwa kuisahau jana, jana ambayo tulikuwa tunakula sahani moja kwenye harusi, na pia tunazika pamoja?

Love ilikuwepo Hope ikapatikana ila tu chama ndio kilikuwa kimoja. Mbona kabla ya huko kulikuwa na vyama vingi? Kina TPP, TANU, ASP na vingine ila watu walipendana? Mwimbaji anasema, “Tomorrow people, where is your past? So you're in the air But you still don't have a thing to spare You're flying high While we're on the low o-o-oh.

Stop telling me the same story” Tuchague watu ambao tuko nao sambamba sio wanaofly high ila hawana kitu chakuspare huku chini wakati sisi tunakufa very very low kwenye treni. Leo wanasema sisi watanzania ni wamoja kesho yule CUF bwana, yule si CHADEMA yule? Mimi CCM hatuwezi kula pamoja??? How? Why? Wanasema tuitengeneze kesho yetu leo kwa uzoefu wa jana, Je? Uzoefu tunaukumbuka?

Jana ilikuwa chungu ile mbaya Maduka ya Ujamaa ukienda kununua sukari eti lazima ununue na majani ya chai kwani kama mimi nataka kutengeneza juice majani nipeleke wapi? Jana ambayo tulipewa ruksa ila sisi wa chini tulidokoa tuu waliokula hao wa juu. Jana ambayo tuliambiwa tule majani ila ndege lazima inunuliwe.

Jana ambayo umeme tulikatiwa eti kina cha maji halafu yule RICH akaingia kati. Leo tutajitahidi kutengeneza ila vitendea kazi hatuna, miundo mbinu mibovu ukianzia kwenye barabara, reli, bandari ndio hoi kabisa tutatengenezaje kesho? Kilimo kwanza mvua zenyewe? Mashamba hakuna wachache wameshajilimbikizia, jembe la mkono pagumu hapo. Halafu sasa kesho akipata madaraka asiyefaa kwanza analipa madeni yake binafsi kwa waliomuweka madarakani, then ainufaishe familia yake halafu ndio akumbuke watanzania waliompigia kura.

Tuwe makini jamani, kwani hatuchoki? “Tomorrow people, where is your past? Tomorrow people, how long will you last?”. Sijali unamchagua nani awe CCM, CUF, CHADEMA, UDP au hata NCCR ila kabla hujamchagua jiulize kwanza is he or she the best candidate? Is he or she going to remember the past? Is he or she going to last long?

Otherwise mwimbaji wa hii nyimbo “tomorrow people” tutakuwa hatujamtendea haki, yeye kishapeleka ujumbe na nadhani unatakiwa uwe received mwaka huu 2010. Ingawa yeye alikuwa anapeleka message mahali pengine ila hata sisi watanzania katugusa. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom