Toleo maalum la miss tz 2009

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18


http://www.globalpublisherstz.com/ijumaawikienda/
pix.gif
[2]Tathmini ya miaka 15 ya shindano hilo, inaonesha kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya Watanzania hawana kimuhemuhe na Miss Tanzania tofauti na angalau ilivyokuwa miaka minne iliyopita.

Katika hilo, Kamati ya Miss Tanzania inayoongozwa na Hashim Lundenga ‘Anko’, inalaumiwa kwa jinsi inavyowalea warembo na kuwaacha ni sawa na kondomu kwamba kazi yake ikiisha inatupwa na kutafutwa nyingine.

Mfano huo unachambuliwa kuwa Kamati ya Miss Tanzania mara inapompata mrembo na kumaliza kumtumia, humwacha akiwa hana A wala B mtaani, huku wao wakiangalia mtu mwingine atakayewawezesha kupata fedha mpya.

Mbele ya hilo, Kampuni ya Compass Communication inaonesha kuimarika zaidi katika shindano lake la Miss Universe kutokana na ushiriki wake mzuri kwenye fainali za dunia Miss Universe, pia jinsi inavyowatunza warembo wake.

Ijumaa Wikienda limegundua kuwa licha ya ukweli kuwa Miss Universe Tanzania ina miaka miwili tu tangu ianze mwaka 2007, lakini sera za Compass zimelenga kuwasaidia warembo.

Limebaini kuwa tangu mshindi wa mwaka juzi, Flaviana Matata mpaka wa mwaka huu, Illuminata Wise, Compass imeendelea kuwalea na kuwatafutia mikataba ya mitindo kwenye nchi mbalimbali, hivyo kuzidi kuboresha maisha yao.
Tofauti na Miss Universe ya miaka miwili, Miss Tanzania yenye miaka 15 mpaka leo hakuna mrembo inayoweza kujivunia kuwa imemtengenezea mazingira ya kuishi kama staa.

Ijumaa Wikienda lina ‘data’ za uhakika kuwa Kamati ya Miss Tanzania ipo kibiashara zaidi kwa kuwa inaangalia zaidi fedha za wazamini kuliko mrembo ambaye wanamvalisha taji kwa mwaka mzima.

Wajumbe wa kamati hiyo wanawekwa kizimbani na kusomewa mashtaka kwamba mara mrembo anaporudi kutoka Miss World, huwa hawana habari naye, isipokuwa hungoja kipindi kingine cha mavuno kutoka kwa wadhamini katika fainali zinazofuata.

Kufuatia tabia hiyo, hivi sasa kuna warembo wanahangaika mitaani, wakibaki kuwageuza mapedeshee kuwa mitaji yao kutokana na kukosa msingi bora Miss Tanzania.

Uchunguzi unaonesha kuwa shindano hilo huwapa umaarufu mkubwa warembo, hivyo hutaka kuishi kulingana na hadhi ya majina yao, kitu ambacho huwa ni kinyume baada ya kutelekezwa na kukosa msingi wa maisha.

Gazeti hili limebaini kuwa kutokana na kiu ya warembo kutaka kuishi maisha ya kifahari, huku Miss Tanzania ikiwa haijawapa dira, hujikuta wakigeuka watumwa wa ngono wa ‘mapedeshee’ ili tu waweze kupata ‘goodtime’.

Gazeti hili linakwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa mwaka 1994 wakati Aina Maeda anavalishwa taji la Miss Tanzania, mashindano hayo yalikuwa katika hali ya kusuasua.

Hata hivyo, mwaka 1998, wakati Basila Mwanukuzi anatawazwa Miss Tanzania, fainali hizo zilianza kuchangamka na kuwavutia zaidi Watanzania, kiasi cha kuwa gumzo la kitaifa kila fainali zilipowadia.

Tathmini inaonesha kuwa tangu mwaka 1997, shindano hilo limepoteza umaarufu na halina mvuto na kwamba mara ya mwisho watu kuhamasika na fainali hizo ni mwaka 2006, pale Wema Sepetu alipovalishwa taji.

Chanzo cha fainali hizo kupoteza umaarufu kinatajwa kuwa ni uteuzi wa warembo wabovu ambao wanashindwa kufanya lolote Miss World, pia kitendo cha Kamati ya Miss Tanzania kuyafanya mashindano hayo kuwa ya kitajiri.

Katika hilo, Kamati ya Miss Tanzania inalaumiwa na asilimia kubwa ya Watanzania kwa kutumia vibaya jina la nchi yao, wakati linawahusu wale wenye fedha nyingi peke yao.

Watanzania wanalaumu kuwa Kamati ya Miss Tanzania imeweka mbele tamaa ya pesa kwa kuweka kiingilio cha fainali hizo kuwa ni kati ya shilingi 50,000 na 100,000, kiasi ambacho ni kikubwa mno kwa Mtanzania wa kawaida.

Kamati ya Miss Tanzania, pia inalaumiwa kwa kuweka mbele ‘njaa’ kwa mdhamini kiasi cha kusahau wajibu wake wa kuandaa warembo wenye sifa.

Pointi nyingine inayotajwa kuondoa msisimko wa Miss Tanzania, ni kuporomoka kwa hadhi ya Miss Dar City Centre tangu mwaka 2004.

Kutokana na picha hiyo, watu mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni kuwa pengine huu ndiyo mwanzo wa mwisho wa Miss Tanzania kwa kuwa katika macho ya sinema ni kama linakuwa kwa sababu ya wadhamini lakini kwenye mtazamo halisi linapumulia mashine.

Wema Sepetu kinara wa skendo Miss Tanzania

Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu ndiye mrembo mwenye rekodi ya kuwa na skendo nyingi ambazo zilijulikana na kuandikwa na magazeti mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa tathmini ya warembo wote waliowahi kubeba taji la Miss Tanzania tangu mwaka 1994, Wema ndiye anayeongoza kwa skendo nyingi.

Skendo ya kwanza kuhusu mrembo huyo ni ile ya kushiriki mashindano ya urembo wakati akiwa na umri wa chini ya miaka 18, kitu ambacho ni kinyume cha taratibu za mashindano.

Habari ya kwanza kuhusu mrembo huyo kuwa ‘anda 18’, iliandikwa kwa mara ya kwanza na Ijumaa Wikienda, mwaka 2006 wakati Wema alipokuwa Warsaw Poland ambako Fainali za Miss World zilichukua nafasi.
Mara baada ya kurudi nchini akitokea Poland ambako alifanya vibaya, Wema alianza kuandamwa na skendo mbalimbali za ngono, rekodi ambayo haijavunjwa na waliomfuatia.

Katika skendo hizo, Wema alihusishwa kimapenzi na baadhi ya wafanyabiashara wenye majina makubwa Dar ambao hujulikana zaidi kama ‘mapedeshee’ kabla ya wasanii Khaleed Mohamed ‘TID’ na Heri Samir ‘Mr. Blu’ nao kutajwa kutoka naye.

Wema pia alitajwa kutoka na staa wa filamu, Steven Kanumba lakini wakawa wanakanusha kabla ya mambo yao kuwa kweupe ambapo baadaye waliachana kwa taadhira, ikiwemo kufikishana mahakamani.
Katika sakata hilo, Wema alilala mahabusu siku mbili kwenye Gereza la Segerea, Dar es Salaam akidaiwa kuvunja kioo cha gari la Kanumba.

Wema pia aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mjasiriamali, Jumbe Yusuf Jumbe na kuzuka zogo kubwa la kifamilia ambapo mama wa Miss Tanzania huyo, Mariam Sepetu aliingilia kati.

Mss Tanzania huyo mstaafu pia anahusishwa kutoka na mbunge mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ingawa amekuwa akikanusha kwa nguvu zote.


Miss TZ yapongezwa
Baadhi ya wananchi waliohudhuria Fainali za Miss Tanzania mwaka huu wameimwagia sifa Kampuni ya Lino Internationl Agency Ltd na kamati nzima ya Miss Tanzania kwa kuonesha waziwazi kuwa inatenda haki.

Wananchi hao walinong’ona na gazeti hili kuwa kitendo cha majaji kumpa taji, Miriam Gerald anayetokea Mwanza, Kanda ya Ziwa kimeonesha kuwa hakuna upendeleo Miss Tanzania.

Walisema, fikra za wengi zilielekea kuwa kwa sababu mwaka jana, Nasreen Karim aliyetokea Mwanza, Kanda ya Ziwa kushinda, isingekuwa rahisi mtu wa kanda hiyo kuibuka tena mshindi.

“Hii imenipa hamasa na nimeamini Miss Tanzania ni wakweli, ingekuwa hawaangalii vigezo, hapa huyu dada wa leo asingeshinda, angetafutwa wa kutoka sehemu nyingine ili tu ionekane mshindi anaweza kutoka popote,” alisema Mark Kimodo wa Ubungo nje ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar zilipofanyika fainali hizo.

Kamati ya Miss Tanzania imepongezwa kwa kutangaza utalii wa ndani kama ilivyo kauli mbiu ya mwaka huu ya mashindano hayo.

“Lundenga na wenzake wanastahili sifa, wamejitahidi kuutangaza utalii wa ndani, tunaomba waendelee hivi hivi,” alisema Rosemary Balinyukwa wa Kijitonyama, Dar kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini.

Richa Adhia ndiye miss kimeo?

Miss Tanzania 2007-08, Richa Adhia ameweka rekodi ya kuwa mrembo aliyeonekana kimeo tangu siku ya kwanza anakabidhiwa taji na aliendelea hivyo mpaka alipomaliza muda wake.

Richa, siku anakabidhiwa taji mwaka 2007 kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar es Salaam umati mkubwa ulilipuka na kukataa matokeo hayo.

Hata hivyo, upo ukweli wa wazi kuwa sauti za Watanzania zilizopazwa, ziliongozwa na hali ya ubaguzi kwa sababu Richa ana asili ya Bara la Asia.

Tathmini inaonesha kuwa kukataliwa kwa Richa hakukuwa Miss Tanzania peke yake, kwani ‘nuksi’ ilimuandama mpaka Miss World baada ya Kamati ya Miss Tanzania kushindwa kumtumia DVD inayoonesha kazi za kijamii alizozifanya kabla hajaondoka.

Kwa matokeo hayo ya kutomtumia DVD, Richa alifanya vibaya Miss World na hata aliporudi alibaki kuwa mnyonge na kuweka rekodi ya kuwa mrembo mkimya zaidi Miss Tanzania.

Lundenga alivyoaibika kwa Nancy

Miss Tanzania 2005-06, Nancy Sumari ndiye mrembo aliyefanya vizuri zaidi na kutengeneza rekodi ambayo haijafikiwa na yeyote nchini kwenye Fainali za Miss World baada ya kufanikiwa kutinga Sita Bora na kubeba Taji la Miss World Africa.

Ushindi huo wa Nancy ulikuwa ni sawa na aibu kwa Mratibu wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga ambaye alimtabiria mrembo huyo kufanya vibaya hata kabla hajapanda jukwaani.

Nancy, mrembo aliyeingia Miss Tanzania akitokea Kanda ya Kinondoni, anabakiwa kuwa bora mpaka sasa kwani kabla yake hakuna mrembo nchini aliyefanya vizuri Miss World kumfikia na baada yake haijatokea.







Mamisi vipenzi vya watu

Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu, 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe, 2001, Happiness Magese, 2004, Faraja Kotta, 2005, Nancy Sumari, 2006, Wema Sepetu ndiyo warembo wenye mvuto zaidi kijamii.

Kwa mujibu wa tathmini ya gazeti hili, warembo hao ndiyo ambao wamebaki kwenye masikio na midomo ya Watanzania wengi.

Katika pointi hiyo, Miss Tanzania 2002, Angela Damas na wa 2003, Silvia Bahame wanakuwa warembo waliovutia zaidi wakati wakiwa na taji lakini baada ya kukabidhi wakazimika ghafla.

Hoyce, Jacqueline ‘K-Lynn’, Happiness, Faraja, Nancy na Wema wanashika rekodi ya kuwa na mvuto zaidi kwa sababu hawajasahaulika mpaka leo.





Warembo waliodorora na mataji

Miss Tanzania 2007-08, Richa Adhia na wa 2008-09, Nasreen Karim ndiyo warembo ambao walipoteza mvuto wakiwa na mataji yao mkononi na kusababisha vipindi vyao kukosa mvuto na msisimko.

Hata hivyo, Nasreen aliwahi kulalamika kuwa anakosa ‘kampani’ kutoka Kamati ya Miss Tanzania ndiyo maana anashindwa kuchangamka na kufanya shughuli za kijamii.

Kwa upande wa Richa, ipo wazi kwamba aliathirika kisaikolojia tangu siku ya kwanza anakabidhiwa taji kwa kukataliwa na Watanzania na baadaye kukosa ushirikiano wa Kamati ya Miss Tanzania kwenye Fainali za Miss World, hivyo kumsababishia kufanya vibaya.[/left]


Source: ijumaa wikienda
 
Sasa wewe ulitaka wafanywe nini baada ya muda wao kwisha. Kwani kuna warembo wangapi ambao huwa hawashiriki miss Tanzania na wanafanya shughuli nyingine nyingi tu. kwani nini hawa ma-miss wakimaliza muda wao na wao wasifanye shughuli nyingine kwa maendeleo ya taifa letu??!!!
 
Back
Top Bottom