Toleo la mwanahalisi wiki hii lanunuliwa kwa mpigo tabora!

M-bongo

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
338
71
Waheshimiwa wana wa nchi! moja ya taratibu zangu za kila siku ni kuingia JF asubuhi na jioni kila siku na kusoma magazeti ya Mwanahalisi, Raia mwema, Rai, Mtanzania, mwananchi kila toleo.
toleo la mwana halisi wiki hii halijafika Tabora nimeenda kulitafuta sehemu zote husika bila mafanikio hata kwa maa-agent wakuu ndipo mmoja wa vendors alipo ning'ata sikio kuwa chapisho lote kwa mkoa wa Tabora limenunuliwa na mtu mmoja ambaye hakutaka kunitajia. swali gazeti hili lilikuwa na kitu gani ambacho kimesababisha kununuliwa lote maana uzoefu wangu mdogo unaniaminisha kuwa gazeti likinunuliwa lote basi ujuwe kuna mtu ameguswa kwa namna moja au nyingine hivyo kwa kufanya hivyo ni kuficha kile kilichokusudiwa! nisaidieni mliopata bahati ya kuliona na kulisoma lilikuwa na kitu gani cha ajabu na je kwa kuficha magazeti yote hasa kwa mkoa wa Tabora kwa weza msaidia mfichaji kutekeleza matakwa yake?
 
Hakuna story yoyote yenye interest ya Tabora, labda makala ya Salva Rweyemamu wa Ikulu, inayomsema vibaya Profesa Lipumba wa CUF. Kama hivyo ndivyo, ndio tutathibitisha yale yanayosemwa kuhusu Lipumba na ubia wake na "watu wa Tabora."
 
Hakuna story yoyote yenye interest ya Tabora, labda makala ya Salva Rweyemamu wa Ikulu, inayomsema vibaya Profesa Lipumba wa CUF. Kama hivyo ndivyo, ndio tutathibitisha yale yanayosemwa kuhusu Lipumba na ubia wake na "watu wa Tabora."

- How Huo "Ubia"?..

-Tulisikia Salva kapelekwa Masomoni...ilikuwa kweli au....? au Anaandika akiwa Ughaibuni...?
 
Back
Top Bottom