Toleo Jipya: Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania

Kwa muda sasa nimekuwa nikifanyia kazi toleo hili jipya la Kijitabu cha Mwalimu cha "Uongozi wetu na hatima ya Tanzania". Ni matumaini yangu wale waliopata shida kuelewa toleo la awali lilivyo na wageni kabisa watapata nafasi ya kujisomea kijitabu hiki ambacho kingekuwa ni lazima kwa wanafunzi wetu wote (kuanzi ngazi za chini hadi za juu kusoma.


View attachment 9488

Aksante bwana M. M. M. kwa kutupa kitabu chenye manufaa makubwa. Inatia moyo kuona vijana wa kizazi kipya wanamuenzi mwalimu J. K. Nyerere kuliko wazee ambao walikuwa karibu naye. Pia inatia moyo kuona kuna watu (kizazi kipya) wanafanya jitihada kuokoa nchi yetu nzuri Tanzania toka mikono ya makuwadi wa ubepari na ubeberu (licha ya kuwa hawajijui kuwa wanafanya ukuwadi kwa watu wa magharibi).
UJUMBE: "Wanaotaka Kumuua Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Hawatafanikiwa Kamwe" M. M. Mwanakijiji.
 
Aisee hivi humu kuna watu hawajui nini sababu ya kuanzishwa JF? Simuelewi huyu Bwassa anapomshambulia MMKJ kuwa ana haki ya kukihariri kijitabu hiki kwanini? Kama vitabu vya dini virihaririwa sembuse cha Mwalimu! Pili kama kuna sehemu ambazo wewe umeona kuwa jamaa kapindisha ingekuwa busara ukazihighlight ili wote tuone maana wengine hatuja pata bahati kusoma cha kwanza. Tatu Unapomsema kuwa kakimbia nchi unamaana gani? Kwamba mtanzania hana haki ya kuishi apendapo? Mtu anaweza kwenda popote akaishi bila kuingiliwa. Nne kazi ambayo hawa jamaa wamefanya ya richmond na Meremeta sidhani kama mwalimu angekuwepo angefanya hivi!!!!! Mfano wakati benki ya biashara inauzwa si alikuwepo je alifanya nini? Alitoa mawazo tu lakini benki iliuzwa tena kwa bei ya kutupa. Hivyo mwalimu ni kweli alikuwa kiongozi mwadilifu lakini kuitwa mwanadamu tu inatosha kumfanya awe na kasoro kibao. Hivyo please watu wakifanya vitu vya msingi wape credit siyo kuleta complaints zisizonamsingi.

Bravo MMKJ KAZI UNAFANYA KUBWA ENDELEA HIVYO HIVYO.
 
Yaani mpaka sasa hujui utakipataje? Pole.

Msaidie tu mwenzio hadi aone kitabu chenyewe mwee mbombo jilipo mwanafyale. Mkono angalia attached files bofya pale kisha utaamua kama una open au save baadaye ataamua kukifanya kuwa kitabu mwenyewe
 
Toleo Jipya: UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA
Huyo anayejiita M.M.M. Mwanakijiji ametenda kosa la jinai kwa kuchukua kazi ya mtu, kuiwekea maoni fulani halafu kuita “Toleo Jipya”. Mbaya zaidi ikiwa mtu mwenyewe amefariki, kama Mwalimu Nyerere. Kama “Mwanakijiji” angetaka kitabu kisomwe angeomba ruhusa ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere, yenye haki ya kunakili kazi za Mwalimu, halafu akichape upya kitabu hicho na kukisambaza, bila ya kukiuza! Haki ya kunakili mtu hajichukulii tu kama apendavyo, huwa inaombwa kwa wahusika! Ndiyo maana ukisoma kitabu chochote, huwa inaandikwa kuwa kunakili, kutumia yaliyomo au kuchapisha upya, lazima upate idhini ya Mtunzi au Mchapishaji. Mwanakijiji inaelekea kuna mengi huyajui, usipotoshe watu, tafadhali!
Bwassa
 
tanzania yetu inahitaji kutoka katika hali iliyopo na kwenda katika hatua ya juu zaidi kidemokrasia. Sasa watu wa aina ya akina tindikali wanapokengeusha mawazo mazuri kwa kudai eti mwandishi alishakufa hivyo toleo la pili la mzee mwanakijiji halina mashiko simuungi mkono.

Tunahitaji kutoka katika authoritarianism na kufanya democratization sasa mtu anapotoa mawazo ya baba wa taifa kwa kuangalia mwono wa kusaidai anapoonekana amekosea sana sio sawa.

Kama unalinda maslahi ya tabaka linalotesa wananchi jua haya mapinduzi yatashinda tu hata kama itachukua milongo kadhaa.big up mzee mwanakijiji aluta continua.
 
Toleo Jipya: UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA
Huyo anayejiita M.M.M. Mwanakijiji ametenda kosa la jinai kwa kuchukua kazi ya mtu, kuiwekea maoni fulani halafu kuita "Toleo Jipya". Mbaya zaidi ikiwa mtu mwenyewe amefariki, kama Mwalimu Nyerere. Kama "Mwanakijiji" angetaka kitabu kisomwe angeomba ruhusa ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere, yenye haki ya kunakili kazi za Mwalimu, halafu akichape upya kitabu hicho na kukisambaza, bila ya kukiuza! Haki ya kunakili mtu hajichukulii tu kama apendavyo, huwa inaombwa kwa wahusika! Ndiyo maana ukisoma kitabu chochote, huwa inaandikwa kuwa kunakili, kutumia yaliyomo au kuchapisha upya, lazima upate idhini ya Mtunzi au Mchapishaji. Mwanakijiji inaelekea kuna mengi huyajui, usipotoshe watu, tafadhali!
Bwassa

Bwassa, inavyoelekea wewe mwenzetu unalinda sana maslahi ya 'Baba wa Taifa' kuliko Mtanzania mwingine yeyote. Hapa nina nakala ya hicho kitabu cha "Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania" nilichonunua kwenye moja ya maonyesho ya vitabu vilivyoandikwa na Mwalimu Nyerere yanayofanywa mara kwa mara na Taasisi ya Mwalimu Nyerere. Kitabu hicho hakina mahali popote palipoandikwa kuhusu hatimiliki kama ambavyo vimeandikwa vitabu vingine vya Mwalimu Nyerere. Nyuma ya kitabu hicho kimeandikwa "Published by Zimbabwe Publishing House. Printed by Jongwe Printing and Publishing. Design and Layout by Ink Spots." Kwenye maonyesho hayo Nilinunua pia kingine cha "Freedom and Unity/Uhuru na Umoja". Hicho ndicho kimeandikwa maneno yafuatayo: "Any requests for permission to quote, extract from this work, or to reprint it in part or in whole, or to translate it into any language, must be addressed in the first instance to: The Personal Assistant to President J.K. Nyerere ….."

Kama ntakuwa sikosei, nahisi kijitabu hiki cha "Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania" kwa maudhui yake, hakikuandikwa maneno hayo ya ‘hatimiliki' kwa makusudi kabisa ili kiweze kuchukuliwa kama mojawapo machapisho ya kawaida kama hotuba za Mwalimu Nyerere ambazo alikuwa akizitoa kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa katika kipindi chote cha uongozi wake na maisha yake kwa ujumla. Wananchi na watu wengine wamekuwa wakipata hotuba hizo kwa njia mbalimbali ikiwemo ya kugawiwa nakala wakati zilipotolewa ‘live' bila kupewa masharti yoyote ya hatimiliki, kutonakili ama kutojadili yaliyomo. Pia, huenda kitabu kile Mwalimu aliamua kukiuza kwa bei ndogo tu ili kuweza kufidia gharama za uchapishaji maana kilichapishwa nje ya nchi na wakati huo Mwalimu alikuwa ni Mstaafu asingeliweza kumudu kuchapisha kwa fedha zake mwenyewe. I might be wrong, but that is my assumption.

Mjadala aliuouanzisha Mwanakijiji ninavyouona zaidi ya kitu kingine chochote ni kwa manufaa ya mawazo ya Mwalimu yaliyowekwa kwenye maandishi hayo. The controversial Mwanakijiji's "Toleo Jipya" sioni kwamba linabadilisha mawazo ya Mwalimu bali kuyajadili na kuona yanavyoweza kuendana na hali halisi ya matukio ya wakati huu nchini mwetu.

Mkuu Bwassa, tusifike mahali tukakosa kumtendea haki Mwalimu Nyerere na kutowatendea haki Watanzania wenye nia njema ya kutaka kujadili kuhusu aliyowahi kusema ama kuyaandika Baba wa Taifa letu kama wosia kwetu sisi 'Watanzania wake' eti kwa sababu tunataka uwepo urasimu wa hatimiliki. Kwa kusema hivyo, sina nia ya kutaka Mwanakijiji asifuate utaratibu, la hasha. Ni kuweka angalizo tu kwamba ninavyoona Mkuu Bwassa, you are trying to build a mountain out of a molehill!
 
Tindikali, Niliuliza swali. Asante kwa jibu.

Namtetea kwa msingi kwamba sidhani kuwa yaliyoandikwa kwenye kitabu hicho ni 'taboo' hayapaswi kamwe kuchambuliwa na kujadiliwa na yeyote anayetaka kufanya hivyo.

nakumbuka wakati nasoma shule ya secondary kulikuwa na mitihani ya kiswahili na kiingereza unaambiwa uchambue kitabu fulani je haya ni makosa kuweka mtazamo wako kuchambua alichotunga mwingine na je nini madhumuni ya mitihani hii?
Ndio maana naunga mkono kuwa nyerere angekuwepo si ajabu angepitisha kichapishwe kama toleo la pili huo nimtazamo mjomba. bibi ntilie usipoteze muda watu wengine ni wabishi tuuuu
 
Hamna mwenye haki halali ya kusambamba maandishi ya kitabu cha mtu baada ya kukibadilisha badilisha.

Mwandishi wa kitabu hakutaka paongezwe nukta wala kupangilia upya aya zake. Angetaka asaidiwe kwenye uandishi angeshamtafuta huyu M.M.M kabla ya kukichapa.

Mwandishi ashafariki halafu tunaambiwa kuna toleo la pili. Ukiuliza nani kaandika, eti ni zimwi lisilo na jina linajiita M.M.M, na sisi tunakibugia, hivi sisi tuna akili kweli?

Kitu muhimu ni ujumbe wake. Sijakisoma ila nitaona kama ujumbe wake unajenga au la.
 
Mzee Mwanakijiji,
Nimekisoma kitabu chako na hakika kimenifahamisha vizuri chimbuko la kudai serikali tatu limetokana na zanzibar kujiunga na OIC. Kifupi nimeelewa zaidi kwamba ni sisi bara tunaotunga mambo mengi machafu na ya kukera ambayo yalimtatiza mwalimu pasipo kupewa sababu za msingi. Wangesema wazi kwamba maadam Zanzibar wamejiunga na OIC basi tutengane, kwani bara hatutaki kuwa pamoja na serikali iliyojiunga na OIC.
 
Thanx alot Mwanakijiji but not only u....JF at large....nimejifunza mengi katika kitabu chako,,,,,plz usikiite kijitabu.... kimebeba mambo mengi sana......Ubarikiwe MKJJ
 
Mi nawashangaa watanzania wenzangu ambao bado wana shabikia CCM, hata Baba wa Taifa angekuwepo leo hii asingekuwa CCM! Aliandika kitabu kama hiki, kuna hotuba ambazo ni mwongozo kamili kwa Taifa letu alizisema lakini hatusikii! Sisi ni watu wa ajabu kabisa. Fikiria alisema "... serikali ikusanye kodi.." huku akimwangalia Basil Mramba-(utafikiri alijua atakuja kuwa waziri wa fedha) lakini yeye akawa anasamehe kodi kama hana akili sawa sawa "...acheni mabaya ya awamu yangu...chukueni mazuri...ajabu mnachukua mabaya na kuacha mazuri..." Maneno haya kwangu mimi kama Mzalendo yana maana kubwa sana, alitabiri ni kweli yanatokea. CHUKUA HATUA!
 
Back
Top Bottom