Toleo Jipya: Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Kwa muda sasa nimekuwa nikifanyia kazi toleo hili jipya la Kijitabu cha Mwalimu cha "Uongozi wetu na hatima ya Tanzania". Ni matumaini yangu wale waliopata shida kuelewa toleo la awali lilivyo na wageni kabisa watapata nafasi ya kujisomea kijitabu hiki ambacho kingekuwa ni lazima kwa wanafunzi wetu wote (kuanzi ngazi za chini hadi za juu kusoma.

26771_381954701155_687191155_4549403_7853556_n.jpg

Toleo la awali lilikuwa na cover hii:

0F7C1C70-4737-4429-B032-D9F4386DE9D3.jpeg
 
Attachments

  • UONGOZIWETUNAHATIMAYETU.pdf
    582.3 KB · Views: 2,973
mimi nitajenga mazingira ya kuwafanya wanangu wakisome kitabu hiki, ni hazina kubwa. M.M.M asante kwa version hii, inaeleweka na kushawishi kusoma page to page. Ile ya kwani nilisoma kwa kuruka ruka.
 
Kama Mwanakijiji ni kitambo sasa.....Ila kwa kweli Nashukuru kwa kitabu hiki..hasa hiki kizazi cha sasa ambacho mambo kama haya kuyajua ni kupita wewe..mkubwa.
Keep it up.
 
Mwana Kijiji
Ahsante kwa jitihada. Je inawezekana kikachapwa na kuuza mitaa ya DSM? Je haina legal implications?
 
Mwana Kijiji
Ahsante kwa jitihada. Je inawezekana kikachapwa na kuuza mitaa ya DSM? Je haina legal implications?

Ninadhani wewe ni unique of all the people. Yaani kitabu umekipata bure. Sasa unataka uuziwe. Ungeuziwa, pengine ungedai kisambazwe bure. Kama lengo hapa ni kufikisha ujumbe kwa watu wengi iwezekanavyo, kwa nini unataka kiuzwe? Hii ni sawa na debate kwamba mosquito nets zitolewe bure au cost-sharing?
 
Hamna mwenye haki halali ya kusambamba maandishi ya kitabu cha mtu baada ya kukibadilisha badilisha.

Mwandishi wa kitabu hakutaka paongezwe nukta wala kupangilia upya aya zake. Angetaka asaidiwe kwenye uandishi angeshamtafuta huyu M.M.M kabla ya kukichapa.

Mwandishi ashafariki halafu tunaambiwa kuna toleo la pili. Ukiuliza nani kaandika, eti ni zimwi lisilo na jina linajiita M.M.M, na sisi tunakibugia, hivi sisi tuna akili kweli?
 
Asante mzee kwa hili, tatizo WaTz wa hali ya chini watakipata je? Ingekuwa vizuri kifahamike zaidi kwao kabla ya oktoba!
 
YEEEEEEEEEEEEEEEEEEES Nimefanikiwa kukidownload hapa bila jasho nakisoma taratibu. Thanx mzee!
 
Hamna mwenye haki halali ya kusambamba maandishi ya kitabu cha mtu baada ya kukibadilisha badilisha.

Mwandishi wa kitabu hakutaka paongezwe nukta wala kupangilia upya aya zake. Angetaka asaidiwe kwenye uandishi angeshamtafuta huyu M.M.M kabla ya kukichapa.

Mwandishi ashafariki halafu tunaambiwa kuna toleo la pili. Ukiuliza nani kaandika, eti ni zimwi lisilo na jina linajiita M.M.M, na sisi tunakibugia, hivi sisi tuna akili kweli?

well.. labda MMM hakuwepo wakati huo!! lakini siyo jambo jipya kuandika na kuhariri maandishi ya wale waliotutangulia.. ndio maana utaona hata biblia na qurani zimepangwa na watu vizuri baadaye na hata maandishi ya kina Plato na wenzake yamehaririwa baadaye.

Kitabu cha Nyerere kilikuwa na makosa mabaya sana ya matumizi ya herufi. Itakuwa ni uzembe kuendelea kusoma lugha ya kiswahili ikiwa imemomonyolewa... Hii inaitwa "journalistic liberties".. Unaweza ukakipitia na kulinganisha mpangiliko wangu wa kihariri na kijitabu cha awali.. kama kuna makosa tunaweza kujadiliana na kuona kwanini nimechukua maamuzi fulani. And no.... sometimes we have to deal with the ghosts of our history past..
 
Asante mzee kwa hili, tatizo WaTz wa hali ya chini watakipata je? Ingekuwa vizuri kifahamike zaidi kwao kabla ya oktoba!

Asante MKJJ.Geneka kama MKJJ ameweza kutuletea, je huoni kuwa sisi vilevile kuwasambazia watu vijijini?
 
"Hatuwezi kuachia utamaduni wa woga ukawa ni mbinu au sifa mpya ya uongozi. Na sasa lazima
tukiri kwamba utamaduni huu wa woga unaanza kuwa ni sehemu ya tatizo letu la kitaifa"
.

I will always remember these words, funny enough watu kama Makamba, Chiligati na hata JMK mwenyewe sidhani kama wanaona hili ni tatizo.
 
Nyambala .. hicho kijitabu kina quotes ambazo huwezi kuona CCM wakiziweka kwenye kumbi zao au kwenye matangazo yao..
 
Nyambala .. hicho kijitabu kina quotes ambazo huwezi kuona CCM wakiziweka kwenye kumbi zao au kwenye matangazo yao..

This is absolutely true na nnadhani kuna quotes humuz zikitolewa kwenye mikutano, semina au makongamano ya CCM, wanaccm wengi wanaweza kufikiri ni hoja au nukuu kutoka upinzani.
 
Mwandishi ashafariki halafu tunaambiwa kuna toleo la pili. Ukiuliza nani kaandika, eti ni zimwi lisilo na jina linajiita M.M.M, na sisi tunakibugia, hivi sisi tuna akili kweli?

Dah ubidamu kweli kazi.
Mtatunyonya mpaka lini nyie?
 
Back
Top Bottom