Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Chuo cha Mabaharia pale kuna wizi mkubwa unafanyika. Wameingia mkataba na Azam Marine kupack meli zake pale. Lakini pesa zinaliwa na Mkuu wa chuo, Mhasibu Mkuu na Bwana Said ambaye ni Manager wa Azam Marine.

Mchezo unaofanywa ni kwamba pesa zikiingizwa kwenye akaunti ya chuo kama malipo ya huduma wanayopata siku hiyohiyo zinahamishwa.

Kwa mwezi, gharama za kupaki meli ni roughly 27mil
 
Jipu kwa wanafuatili na kufanya uchunguzi wa milion saba kwa dk, ule uchunguzi urudiwe upya waliokamatwa wote wana hatia sawa kwa nini wengine wapunguziwe makosa?

Wanaoendesha kesi wachunguzwe upya, wanamzunguka boss wao Mlowola, wanampa taarifa za uongo makampuni yaliyofanya ubadhilifu miatatu 300 wamekamatwa watu wachache ambapo mhusika hajataja wateja wake wote....
 
Tunaomba waziri wa NISHATI na MADINI, Mh. Sospeter Muhongo atusaidie kuharakisha uingizwaji wa umeme katika kijiji cha IHOWANZA kilichopo kata ya IHOWANZA, wilaya ya MUFINDI na mkoa wa IRINGA.

Ni muda mrefu sasa umepita tangu transfoma ifungwe lakini bado umeme kufika bila sababu za msingi.

Tunaomba Waziri awaulize wanaoshughulikia umeme katika eneo hili kuwa kuna tatizo gani kwani siku zinazidi kwenda bila kuona matokeo.

Ahsante.
 
Maafisa utumishi wa Manispaa ya Ilala in majipu makubwa mnoo! Watumishi kupanda madaraja in mtihani na ukipanda mshahara baada ya mwaka mmoja na nusu hadi miwili ndo unaongezeka; yaani sijui wakoje?

Likizo ya mwaka juzi, pesa mpaka leo hawajalipa!

Mishahara Ilala ni wa mwisho kupokea Tanzania nzima
 
Tunaomba waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi atusaidie huku mkoani Njombe hasa Halmashauri ya mji wa Makambako.

Kuna walimu waliopanda daraja mwaka 2013 ambao walitakiwa kupanda daraja mwaka huu 2016 kama ambavyo wachache wao wamepanda. Tunaomba msaada katika hilo, kwani inaumiza sana unapoona mtu ambaye mlikuwa katika daraja moja anakuacha hivi hivi na wewe ukiwa unamwona kwa macho yako.

Pia kufanya hivyo ni kutengeneza matabaka katika vituo vya kazi na nchi kwa ujumla kwa kuwa mshahara ya watu hawa ambao ni wamoja itatofautiana.
 
Naomba waziri anayehusika katika upandishaji madaraja hasa kwa walimu atupe ufafanuzi juu ya vigezo vinavyotumika kupandisha madaraja walimu katika nchi yetu.

Kwa mfano, walimu fulani wapo katika daraja moja. Baada ya miaka michache utakuta walimu hawa wakiwa na sifa zinazofanana wanatofautiana katika ngazi mshahara na madaraja ndani ya wilaya, mkoa na nchi moja. Haya yote yapo katika mkoa wa NJOMBE, hasa katika Halmashauri ya mji wa Makambako.

Naomba, kwa kuwa upandishaji wa madaraja umesitishwa kwa muda, basi pale kazi hiyo itakapoanza tena wakumbukwe hata wale waliokuwa wamesahaulika au wamepuuzwa mara ya kwanza ya upandishaji madaraja mwaka huu 2016.
 
Chanjo ya polio mpaka sasa nina mtoto wa miezi 9 anaenda wa kumi hajapata, private hospital hakuna kama inatakiwa tulipie naomba mtuelekeze wapi kulipa siyo tatizo
 
Ukosefu wa maji ya visima au suluhisho la maji wilaya ya Bukoba vijijini wakati Mbunge yupo, japo hajaweka plasta mdomoni, lakini hajawahi kuongea matatizo halisi ya wakazi wa BUKOBA VIJIJINI.

Tunavyoongea dumu la maji katika vijiji vya Ibwera, Kaazi, Kigabilo, Kansenene, Kanazi, Rulongo etc ni sh 700, mbunge yupo hana msaada wowote.
 
Kuna ndugu yangu alienda ofisi za TTCL akaambiwa kuna kitu kinaitwa jirani kampeni. Akaomba hiyo huduma akajazishwa fomu hii wiki ya tatu hajapata huduma. Ni masikitiko na fedheha kwa wateja.TTCL mnahitaji kutumbuliwa na Dr. Magufuli maana mmekuwa vidonda sio majipu tena.

Hii imetokea ofisi za TTCL, Pugu road
 
OMBI KWA RAIS MAGUFULI. Mheshimiwa rais Magufuli, mimi kama mtanzania na mzalendo wa kweli katika nchi hii, naomba :-

(1)Nikupongeze kwa kazi nzuri unazozifanya ili kuleta nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma.

(2)Usikate tamaa katika kupambana na ufisadi na kuhamasisha watu kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato chao.

(3)Usitumie muda na akili nyingi kuwaza juu ya watanzania wenzetu ambao wameamua kuunda magenge ya kutetea ufisadi na mafisadi. Watu hawa si wazuri sana hasa kwa mustakabali wa nchi yetu. Kila jambo jema unalolifanya kwa ajili ya nchi yetu, wao wanajaribu kupotosha ukweli huo na kujaribu kuwaaminisha watanzania kuwa kila unachokifanya siyo kizuri.

(4)Ukaze uzi zaidi ili nchi yetu iweze kupiga hatua za maendeleo. Naomba wale watakaojaribu kuleta fujo, uwape adhabu ambayo kwa hakika hawawezi kurudia tena. Ni lazima ifike muda watanzania tuache kelele zisizo na msingi wowote na tujikite katika kufanya Kazi kwa bidii. Maendeleo hayaji bila kwanza kukubali kuumia kidogo. Ni lazima kuwe na muda wa kuchumia juani ili siku zijazo tuweze kulia kivulini.

(5)Kama itawezekana uanzishe mfuko wa kuchangia kwa hiari. Mfuko huo utashughulikia masuala muhimu kama vile majanga ya asili nk. Fedha hizo tuchangie kupitia M-PESA, TIGO PESA, HALO PESA, BANK nk. Bila shaka watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu wanaweza kuchangia.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MBARIKI RAIS MAGUFULI NA VIONGOZI WOTE WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. AMINA.
 
Mheshimiwa rais Magufuli, kwa kuwa baadhi ya watu wanasema wewe ni dictator, basi kwa maoni yangu nafikiri ni wakati sasa wa kuonesha u dictator mkali angalau hata kwa watu wachache tu ili iwe fundisho kwa wengine.

Kwa namna hiyo watu watatofautisha mtu dictator na asiye dictator. Kwa akili yangu mimi, bila kutumia ubabe kidogo nchi hii haitaendelea hata kama tutakuwa na kila kitu. Pia demokrasia, huruma na upole vikizidi sana katika nchi, kupiga hatua za maendeleo itakuwa ni vigumu sana.

"UKICHEKA NA NYANI UTAVUNA MABUA".

Mungu mwenyezi akulinde(rais Magufuli), akubariki na awateketeze maadui zako kwa moto mkali ushukao kutoka juu.

Amina.
 
BUREAU DE CHANGE ZOTE ZIFUNGWE ZINAHATARISHA UCHUMI WA NCHI.

1. zinachangia kutorosha fedha nje ya nchi
2. zinasababisha ukwepaji kodi kwa sababu waagizaji wa mizigo wanatumia kufanya miamala ya T/T,.
3. Million saba kwa dakika zilifichwa huko. zinasababisha money laundering itokanayo na madawa ya kulevya,
4. wamiliki wengi ni BOT worker.
5. zimevunja sheria za nchi zilizowekwa na watanzania.
6. Hazikaguliwi na kusimamiwa ipasavyo.
7. Pato lake halitokani na biashara halisi
8. Zinasababisha shilingi ya Tanzania kukosa thamani.
9. Zinasababisha kupanda kwa dola na kusababisha ugumu wa maisha kwa watanzania.
10. zinasababisha Rushwa kukidhiri kwenye huduma ya mabenki.
11. Hazichangii maendeleo ya jamii kama ilivyo kwenye mabenki. Mheshimiwa Rais mimi kama mtafiti na mtaalam wa mambo ya fedha napendekeza zifungwe na shughuli yake ifanywena mabenki tu. Kwa hiyo hili ni jipu kubwa sana.

MHESHIMIWA RAIS NAPENDEKEZA TAFAKARI,FANYA UTAFITI THEN TUMBUA KABISA HILI JIPU'
 
Mkuu wa Chuo cha ufundi Arusha ni jipu. Magazeti yameandika kwa kirefu juu ya namna ambavyo uongozi wa chuo kupitia Mkuu wa chuo umekuwa ukifanya chuo na rasilimali za umma kama shamba la Bibi. Napenda kusifu na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kupambana na ufisadi nchini.

Kwa umakini mkubwa baadhi ya maeneo kama Chuo cha Uhasibu Arusha na chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha tayari vyuo hivi vimeshafikiwa na tayari hatua zimeshachukuliwa. Sehemu pekee yenye shida iliyobaki katika eneo hili ni Chuo cha ufundi Arusha.
 
Mkuu wa Chuo cha ufundi Arusha ni jipu. Magazeti yameandika kwa kirefu juu ya namna ambavyo uongozi wa chuo kupitia Mkuu wa chuo umekuwa ukifanya chuo na rasilimali za umma kama shamba la Bibi. Napenda kusifu na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kupambana na ufisadi nchini.

Kwa umakini mkubwa baadhi ya maeneo kama Chuo cha Uhasibu Arusha na chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha tayari vyuo hivi vimeshafikiwa na tayari hatua zimeshachukuliwa. Sehemu pekee yenye shida iliyobaki katika eneo hili ni Chuo cha ufundi Arusha.
7640_10153996847952487_1296214619587581403_n.jpg
 
Chanjo ya polio mpaka sasa nina mtoto wa miezi 9 anaenda wa kumi hajapata, private hospital hakuna kama inatakiwa tulipie naomba mtuelekeze wapi kulipa siyo tatizo
Polio ziko nne sasa Sijui hajapata ya ngapi
 
Sorry hakupata chanjo ya kifaduro na ile ya matonne ya vitamin A, ndo ilikuwa kasheshe kupata Ila sasa amepata nayo ni baada ya kusafiri kwenda mkoa mwengine.
 
Back
Top Bottom