biwak mbagwa
Member
- Nov 8, 2015
- 18
- 2
Mhemiwa Rais fanya uwezavyo tupate katiba mpya,right aliokuwa anafanya hayati Molinge yangekuwa katika format leo ungefanya kuyaendeleza tuu,Mungu ibariki Tanzania.
Maoni yangu umeishayaongea kwenye hoja zako.Naomba nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anayoifanya ili kulikomboa taifa letu fukara. Najua nchi hii tukimuachia Rais peke yake hataiweza kamwe kwani kunachangamoto kubwa sana za kitaifa ambazo tumezilea kwa muda mrefu sana kama taifa na hivyo kuwa donda ndugu kwa maendeleo na mustakabali wa taifa letu. Mfano mafisadi na wala rushwa ambao wametamalaki katika taifa hili toka ngazi za juu hadi chini.
Rais kwa kumtazama jinsi anavoongea na kutenda inaonyesha ana nia ya dhati kabisa ya kulikomboa taifa hili. Ila katikati ya kulikomboa taifa anamaadui wengi waliokuwa wakinufaika na mfumo mbovu wa uongozi wa taifa hili. Maadui hao wapo ndani ya CCM na wengine wapo nje ya CCM hili ndugu zangu lazima tulijue bila ubishi, pia na Mheshimiwa Rais analijua hilo.
Kumjua adui ni jambo moja na kupambana naye ni jambo jingine.
Mheshimiwa Rais mimi binafsi namuomba Mungu akujalie hekima na busara zaidi ili wewe nasi wananchi kwa ujumla wetu tushirikiane tuipeleke nchi yetu mbele; Pia Watanzania tuweke itikadi zetu zote pembeni zikiwepo za kisiasa, kidini na kikabila. Najua katikati ya juhudi za kulikomboa taifa ADUI ni wengi sana hasa wanufaika wa mfumo uliotufikisha hapa, lakini kwa umoja wetu kama taifa tutashinda.
Mimi binafsi ni mwanachama wa CHADEMA lakini nachokiomba upinzani kwa ujumla tusiendeshe siasa kama ushabiki wa Simba na Yanga. Hili ni taifa hivyo vizazi vingi vyetu vitakuja na kustaajabu madudu tuliyokuwa tunayafanya kwa kutokua na mikakati yeyote ile zaidi ya ubishani tu. Kwa sasa si wakati wa kumvizia Rais na serikali yake wakosee ili kupata sehemu ya kuwakosoa, nacho kiomba tunapo ona mambo hayaendi ni wakati wa kumuona Rais na kutoa ushauri kabla janga halijatupata kama taifa vinginevyo Rais akatae huo ushauri. Naomba tuige siasa za watu wa Ulaya na Marekani. Ambapo wao baada ya chaguzi hurudi na kuwa kitu kimoja kujenga mataifa yao.
Pia CCM naomba muelewe kuwa sasa ni wakati wa kulijenga taifa imara kiuchumi na sio wakati wa kuchuma kupitia serikali. Tunacho mshukuru Mungu tumempata Rais anayesubutu kufanya anachokisema hivyo ni wakati wa kumwacha Rais awe huru na sio kumzonga Rais na kumpanda kichwani na kuliyumbisha taifa.
Rais tuliyempata sio Mungu hilo tulijue anamapungufu kama mwanadamu hivyo anahitaji washauri wazuri wenye nia njema wasio na hila , pia hawezi kugeuza hii nchi kwa siku moja hilo tulijue.
Mtanzania mwenzangu toa mawazo yako tumsaidie Rais kulijenga taifa letu.
Jipu lingne lipo Chuo cha usimamizi wa fedha IFM huyu acting rector aliyewekwa ni Bonge la jipu na yeye pamoja na wenzie wachache ndie aliyekwamisha maendeleo ya chuo kabla hajawa acting rector
kundi kubwa lkn hamna nguvu ni wa kuburuzwa tuSisi watanzania tuliowanyonge, tuliokuchagua tunakuunga mkono kwa 100% kwa hatua zote unazochukua zidi ya mafisadi na wahujumu uchumi. Wanao jaribu kukukatisha tamaa ni wachache sana, ila kundi kubwa tupo nyuma yako. Mungu wetu mkuu atawaangusha wote wale wanaonena maneno ya kejeli juu yako.
Kama walivyopata kunena juu ya udhaifu wa serikali iliyopita, basi watanena maneno ya kukukatisha tamaa kwa sababu tu wao wanaweza kupata muda kwenye vyombo vya habari, ila wananchi tunakuelewa zaidi wewe amri jeshi mkuu, maana ndiye tuliyekupatia dhamana ya kusimamia maslahi ya taifa na sisi wanyonge.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Dr. Magufuli!
Ndugu wana JamiiForums,
Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.
Karibuni sana.
MWONGOZO:
Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.
Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
Ndugu wana JamiiForums,
Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.
Karibuni sana.
MWONGOZO:
Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.
Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
**USHAURI MDOGO KWA WAZIRI WA UTUMISHI**Ndugu wana JamiiForums,
Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.
Karibuni sana.
MWONGOZO:
Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.
Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
Hao ndio watz wwanaofanya matamasha ya kuwapongeza wapiga viroba , ili kuwatongoza wazuie wageni wasipewe kazi, na wao waongezwe mishahara.Jipu uchungu nimeliona hospitali ya Mwananyamala kitengo cha maabara watu wanaanza kupewa huduma saa tano. Na wakati wafanyakazi wanafika ofisini saa moja wao ni stori tu na kuacha wagonjwa wanaendelea kuzidiwa....
Mtu amepima toka jana lakini kumpa tu majibu yake asubiri hadi saa tano ndo waanze kutoa majibu....wao na stori tu ofisini