Elections 2010 Toka kwa mwenzetu, mpole, mwadilifu, mbarikiwa na mpenda JF kwa moyo - Masanilo

Mwafrika

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,490
226
Nilishangazwa sana na kitendo cha Nakaaya kuamua kukabidhi kadi ya CHADEMA kwa Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni mgombea urais kupitia chama hicho. Nakaaya kwenye Magwanda ya CHADEMA nilikuwa namwona kama nuru ya vijana wenye mioyo ya kimapinduzi na wenye kutakia mema Tanzania yetu. Baada ya kutafakari sana nilimegundua nilikuwa nakosea, Nakaaya ametumia haki yake na maamuzi yake lazima yaheshimiwe. CHADEMA ni taasisi na si mtu ama watu, wengi watajiunga na wengi wataondoka ila chama kitakuwepo na kitaendelea kuimarika kwa wale wote wenye moyo na itikadi za CHADEMA.

Mapinduzi ya kweli yanahitaji askari wenye moyo na wale wenye uwezo wa kujitoa muhanga. Sasa kama unapewa ice cream na unaweza kutoa siri wapi alipojificha jemadari mkuu wako ni hatari sana! Heri ukaachana na mapambano kabla hujasaliti. Nimeonana na Nakaaya mwanzoni wa mwaka huu nikampongeza kwa wimbo wake wa Mr Politician tukaongea mengi, mipango yake ya music na siasa. Anajiamini sana hana haiba za wadada wengi wa Kitanzania, anapenda ishi maisha yake. Siku ile alikuja na ML class Mercedes Benz nyeusi, Mchungaji nikaweka heshima. Sijui kama ni la kwake ama alikuja safisha nyota!

Kama kweli Mil 30 alizoahidiwa mwisho wa Kampeni kama wale wasanii wenzake, walio kwenye kampeni za CCM, ndicho hasa kilichomtoa CHADEMA basi siasa hatoziweza maana akipewa dhamana yuko tayari kuuza hata uhuru wetu.

Kuwa Upinzani kunahitaji uwe na moyo wa Simba, si kila mtu anaweza. Mchungaji nimejitoa muhanga niko tayari hata kujilipua uongozi wa imla na kikoo wa CCM ufikie mwisho. Nimalize kwa kumpongeza sana sana kwa uamuzi wake wa kwenda kwenye kundi la ndege analofanana nalo rangi! Sababu anajua udhaifu wa kiutendaji wa Mwenyekiti wake mpya basi kura yake bado tunaihitaji CHADEMA.

Vote for Slaa

Wenu Mchungaji

Rev Masa

Peace to you all
 
shukrani mchungaji kwa upembuzi yakinifu
 
Hivi kweli kuna sababu ya kuunga hii na ile thread mama ya huyu binti kukabidhi kadi ya CHADEMA kwa Kikwete? Sijui nani anafanya haya

Kulikuwa hakuna sababu yoyote mzee. Natumaini hata Nakaaya mwenyewe ataisoma muda si mrefu kwa vile imekuwa hapa ikijitegemea.
 
Mchungaji nadhani hata Nakaaya akiiona hii itamuuma sana, umeongea kwa kutumia Busara ila Ujumbe umefika
 
Hapa nilipo ninamtumia email Nakaaya asome hili somo la mchungaji

Kwa kuwa amebadili simu basi kwenye e-mail mwambie akumbuke wosia wa mchungaji, ukiwa mwanasiasa usiwe muongo na ukiwa muongo basi uwe na kumbu kumbu neno la mwisho tuliloongelea Ile Alhamis pale Lounge jioni jioni hivi!
 
Leo nimepitia video zake zote..kwa kweli sasa wabongo wengi ni noma..mimi kama (mbongo) mTz imebidi nijifikirie mara mbilimbili.
Not any more, hatuwezi kuwashangaa wenzetu, mfano wanaijeria!!
 
Mtalia sana tu

na hakuna budi mwsiho chama mvunje au wahuni wote mufukuze akina slaa na mbowe

chadema bye bye
 
Kwa kuwa amebadili simu basi kwenye e-mail mwambie akumbuke wosia wa mchungaji, ukiwa mwanasiasa usiwe muongo na ukiwa muongo basi uwe na kumbu kumbu neno la mwisho tuliloongelea Ile Alhamis pale Lounge jioni jioni hivi!

Mchungaji, yaani I'll make sure kwamba nimeongea naye ana kwa ana ili nimpe "peace of my mind"
 
Nakaaya is nobody in the politics of Tanzania (she is better of doing what she does best....music). Hakuiongezea chochote Chadema (sikujui hata kwamba ana jihusisha na siasa) na hata iongezea chochote CCM. Kumjadili mnampa tu publicity ya bure na kumkweza. Kama watu mmesha tambua kuwa chama si mtu ni watu kuendelea kujadili na kufungua thread nyingi kuhusu mtu mmoja kuondoka inaonyesha kuondoka kwake kume kuwa na impact fulani. Anyway they are way bigger fish to fry.
 
Roho inaniuma sio kwa sababu amebadili mwelekeo, ila kwa sababu kwa mbali napaa hisia kwamba amefanya uamuzi huu chini ya shinikizo ambalo moja kwa moja linatupeleka kuaamini kwamba nyuma ya shinikizo, kuna noti.

Siamini pia kama Nakaaya ana tatizo kuuuuubwa kivile la njaa hadi akubali hizi cheap politics! Nashindwa kuelewa, lakini kama ni ubunge wa viti maalum, au nafasi ya u DC au vyovyote, ajua anavipaa kwa gharama kubwa sana ya matumaini ya watanzania waliokuwa wamemwekea juu yake....ni usaliti!

Nakaaya, kwa nini umejiuza bei rahisi hivyo? tafadhali zingatia ushauri wa mchungaji Masanilo!
 
Back
Top Bottom