Toka jimboni Arumeru: UVCCM Arusha wagomea posho toka kwa mbunge...

Inasikitisha sana unachokisema hukijui vizuri maana hata hao viongozi wa chama chako nao wanayafanya hayo hayo! Tena bora CCM tunatoa michango ya kuimarisha chama chetu kwa hiari na kwa kuhamasishana kukihuisha chama chetu kwa kukichangia harambee, kuna vyama vingine wamewekeana viwango vya lazima, kama 'payback charges' kwa kupewa ubunge!

Ndugu Kigwangalla, USIKIMBIE HOJA! Kwanza naomba nikufahamishe hivi:
1. Mie siyo mwanachama wa Chama chochote cha siasa! Kwa hiyo sina viongozi "wa chama changu".
2. Niliyochangia kuhusu Mh. Catherine na posho iliyoonekana ndogo mpaka kukataliwa, niliunganisha na wito wa mwenyekiti wa UWT CCM kuwa wabunge wa viti maalum wachangie jumuiya hiyo, kwa hiyo kwa kuwa Mh Magige alikuwa anafanya kazi ya jumuia yake, alikuwa AUTOMATICALLY anaitikia wito wa Sofia Simba!
3. Nilichangia kuhusu KUONGEZEKA posho za wabunge kuwa Mnalalamika kuwa Mnaombwa PESA na watu mnapowatembelea!
HOJA IKO hapo.
4. Kwa "Vyama vingine kuwekeana viwango vya lazima" Hakuhalalishi CCM kugawa pesa kwa vijana wanaowasindikiza kwenye mikutano ya hiari!
 
[h=2]UVCCM Arusha: Maneno ya uzushi yakomemeshwe[/h]


By John Ngunge



22nd February 2012
email.png



printer.png

comment_bubble.png



Baadhi ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Arusha, wamesema maneno ya uzushi yanayolenga kuwagawa na kuibua hali ya kutoelewana ndani ya umoja huo lazima yakomeshwe.
Akizungumzia taarifa za uzushi zinazotolewa dhidi ya umoja huo, Masoud Rajab, kutoka Lemala alisema jana kuwa vijana kwa miaka yote wamekuwa wakifanya kazi za kujitolea ndani ya CCM na umoja wao, hivyo taarifa zilizotolewa kuhusu vijana kugomea posho zimewafedhehesha.
“Vijana tumesikitishwa na kauli hiyo siku zote tunafanya kazi ya kujitolea hakuna anayelipwa,” alisema.
Rajab alikwenda mbali zaidi na kuomba mwanachama wa CCM aliyehusika na kueneza habari za uongo kwa lengo la kuwafitinisha vijana na kuipaka matope UVCCM achukuliwe hatua za kinidhamu.
Alisema mlezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Steven Wasira, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) tayari alishakuja akazungumza na umoja huo hapa kuhusu makundi yaliyokuwapo.
Alisema tofauti zilimalika na wakakubaliana kufanya kazi na sasa wameanza tena kuibuka na kuleta uchonganishi kwa vijana.
Naye Mjumbe wa Baraza la Vijana Arusha Mjini, Kafimbi Juma, akizungumzia kitendo hicho alisema anashangaa kuona UVCCM imetulia lakini kumbe nje watu ambao si wanachama wa UVCCM hawataki kuona hali ya utulivu.
Alisema UVCCM lazima ifanye kazi za kujitolea na kikubwa Mbunge Catherine Magige, ni kijana na amekuwa akizunguka mkoa mzima kutoa misaada kwa jamii.
Alisema mbunge anaposindikizwa kufanya kazi na vijana kuna baadhi hawataki kuona hali hiyo.
Hivi karibuni, Mbunge Magige, alitoa msaada wa baiskeli kwa watu wenye ulemavu katika eneo la Oldonyo Sambu wilayani Arumeru.
Katika shughuli hiyo, vijana wa UVCCM waliongozana naye kwa lengo la kumsaidia kupakia na kushusha, hata hivyo taarifa zilizoripotiwa zilidai vijana hao waligoma kupokea posho iliyodaiwa kutolewa na Magige, jambo ambalo wamesema si kweli.



SOURCE: NIPASHE
 
Hivi wewe ni Doctor kweli au ni Getruda Lwakatare type?!!Ila jina lako kwa mjibu wa kabila fulani hapa tz lina maanisha mlio wa debe tupu linapoanguka chini,nadhani maana hii ni kielelezo halisi cha wewe mwenyewe hata na ukoo wako wote.Kama ndiyo wewe nakushauri usiwe unachangia kitu hapa JF,kuwa msomaji tu wa kawaida,kinyume chake mkuu utasababisha matatizo makubwa sana hapa...au umetumwa kuja kuwa source ya Ban hapa JF na ma.ga.m.ba?!!!!!

ingefaa ujibu hoja badala ya kushambulia personality ya mtu.unaweza kuwa humpendi mtu lakini akawa na hoja ya maana
 
CCM sio chama cha siasa ni genge la walafi matumbo mbele ila iko siku yao; ghadafi aliiipata fresh,,mobutu,mubarak,KANU HAPA BONGO SI MBALI;yanayotokea Arusha,Mbeya na Songea ni ngurumo za radi watanzania wanaanza kuamka;

Agesema LEMA kuwa atamwaga damu ya wazee wa kimeru polisi wangekufa nae ila wakisema wazee washii hakuna noma shega tu mpaka Msajili anawaenezea ujumbe.
 
Back
Top Bottom