only83
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 5,343
- 2,525
VIJANA wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Arumeru, juzi waligoma kupokea posho ya Sh 5,000 kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige kwa madai kuwa ni ndogo na za kuwadhalilisha.
Magige alitoa posho hiyo mwishoni mwa wiki kama asante kwa vijana waliomsindikiza katika ziara yake wilayani Arumeru mkoani Arusha kutoa msaada wa baiskeli kwa walemavu katika eneo la Oldonyo Sambu.
Vyanzo vya habari vilieleza kuwa ziara hiyo ilianza saa 5 asubuhi na kumalizikia majira ya saa moja jioni na baada ya hapo Magige alitoa fedha hizo kwa mmoja wa wapambe wake ili awagawie vijana waliokwenda katika ziara hiyo iliyoonekana zaidi kuwa ya Jumuiya ya Wanawake ya chama hicho (UWT).
Baada ya mgawo huo, inadaiwa vijana hao walizisusa wakidai ni kidogo na zinalenga kuwadhalilisha.
Umefika wakati wa sisi vijana kugoma kutumiwa kwa ujira mdogo kwa manufaa ya watu, tumekwenda ziara siku nzima halafu anatupa Sh 5,000, hii dharau kubwa.
Huu ni udhalilishaji wa kutufanya kama watoto wadogo wa kubembelezewa pipi, sasa udhalilishaji wa aina hii umefika mwisho kwa wabunge wa namna hii turudishe hizi fedha mara moja, alisikika akishawishi wenzake kijana mmoja aliyekuwepo katika msafara huo.
Mbunge Magige alipoulizwa juu ya suala hilo, alisema hana taarifa ya UVCCM kukataa kupokea posho hiyo na kutaka kugombana kwani wenye kujua hilo ni wao wenyewe na wao ndio wanaopaswa kuulizwa.
Mimi sina taarifa ya hilo la kukataa posho ya ziara wala vijana kugombana, lakini ingekuwa vizuri zaidi ungewauliza hao hao vijana juu ya sakata hilo, alisema Magige.
Mmoja wa wanachama wa UVCCM Arusha, Philimini Amo alipoulizwa, alidai kweli vijana hao walikataa posho hiyo na kudai kuwa hali hiyo ilijitokeza kutokana na Magige kupewa taarifa potofu na wapambe.
Source : Habari leo