Toka jimboni arumeru: Mambo yaanza kupamba moto, mgombea ccm ajitoa,kisa mchezo mchafu....

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
HEKAHEKA za kutafuta mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Jimbo la Arumeru Mashariki zinazoshika, kasi zimeingia doa baada ya mmoja wa wagombea aliyejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo kuamua kujitoa akilalamikia rafu ukiwamo mchezo mchafu wa rushwa.

Aliyejitoa katika mbio hizo ni Rais wa Mtandao wa Vijana nchini (YDN), Elipokea Urio akidai kuwa mchezo mchafu umekuwa ukichezwa kwa baadhi ya wagombea wenzake wa CCM kutoa rushwa.

“Nimeamua kujitoa kwa roho moja kabisa kutafuta ridhaa ya chama kiniteua kitokana na mchezo mchafu wa rushwa unaoendelea huko Arumeru Mashariki. Ninajua mchakato hautakuwa wa haki, sasa kwaini nichafue historia yangu?”alisema Urio akihoji.

Katika hatua nyingine, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeonya kuwa kitamuengua kwenye kinyang’anyiro hicho mgombea yeyote atakayebainika kwenda kinyume cha maadili na maelekezo ya kampeni za kuwania uteuzi wa chama hicho kwenye uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Arumeru, Totinani Nandonde alitoa onyo hilo juzi, wakati akimkabidhi Mhadhiri wa Sheria, Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Anna Mghwira fomu ya kuomba uteuzi kuwania ubunge jimboni humo ambaye ni mwanachama wa tano kujitokeza ndani ya chama hicho kuwania nafasi hiyo.

“Ili kudhibiti hujuma na matumizi ya fedha katika kampeni, chama kimepanga siku ya mkutano mkuu maalumu wa wilaya utakaotumika kuwapigia kura za maoni wagombea wote kuwa ndiyo siku ya kampeni kwa wote wanaowania uteuzi. Hakuna mgombea anayeruhusiwa kupita huko kwenye kata na vijiji kufanya kampeni hivi sasa,” alisema Nandonde.

Wakati huohuo pamoja na Takukuru kuonya wagombea ubunge wanaowania kuteuliwa na CCM katika Jimbo la Arumeru Mashariki juu ya matumizi ya rushwa katika kinyang’anyiro hicho, baadhi ya wagombea hao wanadaiwa kuendelea kutoa mlungula bila wasiwasi wowote.

Katika kuhakikisha inazuia matumizi ya rushwa katika uchaguzi huo, Takukuru imetoa onyo hilo kwa wagombea wote sita wa CCM baada ya kukutana nao juzi jioni.

Hata hivyo, hatua hiyo haijasaidia lolote huku uchunguzi ukionyesha kuwa baadhi ya wagombea wakimwaga fedha kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya Arumeru utakaofanyika leo, kwa kuwagharamia usafiri kutoka maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, malazi na chakula.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa gazeti hili mwishoni mwa wiki,unaonyesha kuwa rushwa hiyo imekuwa ikitolewa kwa baadhi ya makatibu wa CCM wa kata, ambao nao hugawa kwa wajumbe wa mkutano huo wa kura za maoni waliopo katika maeneo yao.

Uchaguzi huo mdogo umepangwa kufanyika Aprili Mosi, mwaka huu kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, marehmu Jeremiah Sumari aliyefariki kwa saratani ya ubongo mapema mwezi huu.

Source : Mwananchi
 
tutasikia mengi! Urio ameshindwa kupambana na mafisadi wenzie! Mtu kama Kitoi mtoto wa marehemu Sumari wanamwaga shekeli vibaya ili wapitishwe na wajumbe!huyu akiwa kny mtandao wa EL,bado wagombea wengine!naona urio ameona asife maskini bora ajitoe!
 
Hata Elipokea na yeye amechukua form? Ee kweli nimeamini chama kinayumba sana!! HUYO NI TAPELI HAFAI HUYO!!! Bora amejiengua mwenyewe maana alijua kuwa hafai na hawezi.....huyu Kijana nadhani alitaka tu cheap popularity ili nae asikike!!

Dah! Nimeshangaa sana wajemeni!!
 
Urio kesha chukua za kwake! baada ya kuombwa kujitoa! asituzuge!
 
Kwa ccm mtu asikudanganye ushindani upo kwa watu wawili tu na mmoja wao ndo atapita kwdnda kugombea SIO SUMARY na ELISHILIA KAAYA . Wengine ni wasindikizaji tu
 
Ugomvi wa ndugu sisi huwa hatuinglii!!. "Ndugu wakigombana wewe chukua jembe ukalime"!
 
Ufisadi ndiyo uhai wa CCM, bila ufisadi CCM haiwezi kuendelea kuwepo kwenye ulingo wa siasa za bongo.
 
tutasikia mengi! Urio ameshindwa kupambana na mafisadi wenzie! Mtu kama Kitoi mtoto wa marehemu Sumari wanamwaga shekeli vibaya ili wapitishwe na wajumbe!huyu akiwa kny mtandao wa EL,bado wagombea wengine!naona urio ameona asife maskini bora ajitoe!

Vita vya panzi furaha kwa kunguru
 
Mbona bado mechi hata haijapangwa...Acha tuone..Msisahau mwenyekiti wa tume Kikongwe na kuchezea Excel hajui mara hesabu zinaenda ndivyo sivyo..usikie UDP wameshinda wakati hata mgombea hawakuwa naye
 
Mimi huwa sishangai nikisikia rushwa imetembea ndani ya CCM nitashangaa siku nikisikia wameendesha uchaguzi wao bila ya rushwa.
 
Hakuna mwenye uwezo wa kupambana na mkono wa Lowassa nchi hii.

sentesi zako zinakera, angalia usijegeuka mtumwa wa hiyari, kama unadhani lowasa ni goliath subiri utamuona daudi pindi pakipambauka.
 
Back
Top Bottom