Toka iringa: Wanafunzi wa kike wamuua mwalimu wao kwa kutaka kumbaka mwenzao..

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Bulongwa kilichoko Wilaya ya Makete mkoani Iringa, wamemuua kwa kumshambulia kichwani mkufunzi wa chuo hicho, Dk. Jumbe Mafingo, kwa madai ya kupinga jaribio lake la kutaka kumbaka mwanafunzi mwenzao.


Taarifa za awali za makachero wa polisi zilieleza kuwa mkufunzi huyo aliuawa baada ya kutuhumiwa kwamba alitaka kumdhalilisha kijinsia mwanafunzi wa kike, Jean Laison Mwakabuta kwa kutaka kumbaka.Tukio hilo la kuuawa kinyama kwa mkufunzi huyo ambaye ni mwalimu wa nidhamu chuoni hapo, lilitokea juzi usiku nyumbani kwake mjini hapa.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, Dk. Mafingo alifikwa na umauti baada ya mwanafunzi huyo kuamua kwenda nyumbani kwake usiku ili kumkabidhi maelezo yake ya kimaandishi kuhusu sababu zilizomfanya alale nje ya chuo.Ilielezwa kuwa muda mfupi baada ya kuingia kwenye nyumba ya mwalimu huyo, mwanafunzi huyo alianza kupiga kelele kuwa anabakwa.


Alisema kufuatia kelele hizo, wanachuo wengine waliamka katika vyumba vyao na kwenda hadi eneo la tukio na kuanza kumshambulia kichwani mkufunzi huyo hadi kumuua.


Kamanda Mangalla alisema Dk. Mafingo aliuawa kwa kushambuliwa na kitu kizito kichwani.

“Huyu Jean Laison Mwakabuta, aliambiwa na Dk. Mafingo ambaye ni mwalimu wa nidhamu chuoni hapo, aandike maelezo ya maandishi kwa sababu gani alilala nje ya chuo,...baada ya kuandika maelezo hayo, aliamua kuyapeleka nyumbani kwa mkufunzi huyo usiku, sasa baada ya kugonga mlango na hatimaye akaruhusiwa kuingia, alianza kupiga kelele kwamba anabakwa…na ndipo wanafunzi wenzake waliposikia kelele wakaamka na kukimbilia eneo hilo na kumshambulia mkufunzi huyo hadi kufa,” alisema Kamanda Mangalla.


Ilidaiwa kuwa siku moja kabla ya tukio hilo, uongozi wa chuo hicho cha Bulongwa ulitoa ridhaa kwa wanachuo wote kwenda kutembea nje ya chuo kwa lengo la kuwapunguzia msongo wa mawazo ya masomo na Jean Laison Mwakabuta hakurejea chuoni hadi siku iliyofuata.Kamanda Mangalla, alisema wanachuo wanne akiwamo mwanafunzi Jean, wametiwa mbaroni kuhusiana na mauaji hayo.
 

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, ...

“Huyu Jean Laison Mwakabuta, aliambiwa na Dk. Mafingo ambaye ni mwalimu wa nidhamu chuoni hapo, aandike maelezo ya maandishi kwa sababu gani alilala nje ya chuo,...baada ya kuandika maelezo hayo, aliamua kuyapeleka nyumbani kwa mkufunzi huyo usiku, sasa baada ya kugonga mlango na hatimaye akaruhusiwa kuingia, alianza kupiga kelele kwamba anabakwa…na ndipo wanafunzi wenzake waliposikia kelele wakaamka na kukimbilia eneo hilo na kumshambulia mkufunzi huyo hadi kufa,” alisema Kamanda Mangalla.

.


Maelezo ya polisi yanaonekana kupwaya, almost kama anaficha kitu, hasa hapo kwenye red. Yaani mwanafunzi aamue kupeleka statement nyumbani kwa mkufunzi usiku? Na kwanini alimkaribisha ndani? Kama ni statement si angepokea na mwanafunzi akarudi zake? Alimkaribisha ndani usiku huo kwa lipi?
 
na huyu mkufunzi kwa nini hana vitasa makini ili tottoz wasiweze kumharibia mipango yake, japo yawezekana kabisa kuwa wadada walipanga kuwa ikitoka kelele tu wamvamie na kumlimboka....
 
seems ni tukio la kupangwa, kwa mazingira ya tz itakua ngumu sana kuujua ukweli unless wahusika wa-confess.
 
seems ni tukio la kupangwa, kwa mazingira ya tz itakua ngumu sana kuujua ukweli unless wahusika wa-confess.
Ni kweli! maana hatuna kabisa Polisi wenye ujuzi wa kupeleleza kwa kina, ndiyo maana wameshindwa hata kuwakamata waliomtekka nyara Dr. Ulimboka pamoja na kutajwa na mhusika mwenyewe na badala yake wanahangaika na kuwakamata machizi na kuunda unda hadithi ili wakishapeleka mahakamani watu wasihoji hadi wasahau. Ni werevu sana kwa maana wanafahamu mfumo wa mahakama za Tanzania kesi hii inaweza chukua hata miaka mitano! Shame on this government!
Kwa tukio hili yaelekea wanafunzi walipanga kumwua mtu aliyekuwa kikwazo cha wao kufanya watakavyo. Lakini katika ya mazingira ya uwepo wa mapolisi wa sampuli yetu kuna kitu hapo?
 
Ukiangalia haraka haraka wanafunzi walipanga kumdhalilisha mwalimu wao,baada mwalimu kuonekana mkali na kutaka maelezo ya kina kwanini alilala nje chuo....kwa maana haikuwa lazima apeleke nyumbani kwa mkufunzi na tena usiku,pia haiwezekani dakika chache amegonga mlango na kuanza kupiga kelele za kubakwa!!!kumbuka huyo binti ni mtuhumiwa shuleni kwa kulala nje,kuna shida hapo (watuambie kama mkufunzi alimuambia apeleke hata nyumbani maelezo yake,la sivyo )wanafunzi walipa nga kumnyamazisha mwalimu wa nidhamu ambae mara zote ndio mbaya wao no 1 (shule zote za bweni)...
 
Mkuu Skills4ever naungana na wewe kabisa,huyu dada alikuwa amejipanga na wenzake kumdhalilisha ticha maana maticha wa nidhamu sehemu yeyote huwa wanaonekana wanoko!Polisi wafanye uchunguzi makini!!
 
unaleta habar za mwaka uliopita? Kama huna cha kupost ni bora uwe mchangiaji.
 
maelezo ya polisi yanaonekana kupwaya, almost kama anaficha kitu, hasa hapo kwenye red. Yaani mwanafunzi aamue kupeleka statement nyumbani kwa mkufunzi usiku? Na kwanini alimkaribisha ndani? Kama ni statement si angepokea na mwanafunzi akarudi zake? Alimkaribisha ndani usiku huo kwa lipi?

nafikiri unafikiria kutoka angani. Wewe ni mwalimu, uko kwenye majumba ya shule. Ukigongewa mlango unafungua au unakataa kufungua? Mi nadhani lazima uitike wito. Sidhani kama hakuna mambo mengine jaribio la kuhondomola(kubaka) linaweza kugarimu maisha, lazima walikuwa wamejipanga.

Cha kuuliza ni kwa nini mwanachuo apeleke maandishi yake usiku badala ya kupeleka wakati wa saa za kazi?
 
Back
Top Bottom