Toka bungeni leo: Muswada umepitishwa... Nini hatma yake?

mimi nasikitika huyu mama badala ya kujibu hoja anaanza kuishambulia cdm na tindu lissu
 
Hivi kulalamika kwenye mitandao kunasaidia nini?

Hivi hamjui ya kuwa hakuna kuvuna pasipo kupanda, na sharti uliwe ili ule? Hivi unadhani waafrika kusini weusi walipata usawa kwa kucheka cheka mitandaoni, au kwamba ndoto za Mchungaji Martin Luther King zilitimia kwa yeye kulala kitandani kuota mitandaoni? Kila mla huliwa na kama tunaitaka katiba mpya na nzuri lazima tuliwe na FFU.

Jamaa watatupiga kweli kweli, na mimi nahisi watatuua hasa, lakini hakuna jinsi.....sasa nasema baasi, mwanangu T mie babako nipo tayari kwenda vitani barabarani, kitakachonikuta Mungu atakulinda wewe, jipe moyo, bora kufa kuliko kuishi huku unadhalilika. Nasubiri tamko.....!
 
Jamani tumekwisha uwiiii, msifikiri kwenye referendum mtaweza kuikataa hiyo
Katiba ya CCM, kwa NEC hii tuliyonayo itachukachua tu hadi hiyo 50.1% ipatikane
nahisi kuchanganyikiwa, tunalipa upumbavu wetu kuwachagua hawa Magamba!
 
Hivi kulalamika kwenye mitandao kunasaidia nini? Hivi hamjui ya kuwa hakuna kuvuna pasipo kupanda, na sharti uliwe ili ule? Hivi unadhani waafrika kusini weusi walipata usawa kwa kucheka cheka mitandaoni, au kwamba ndoto za Mchungaji Martin Luther King zilitimia kwa yeye kulala kitandani kuota mitandaoni? Kila mla huliwa na kama tunaitaka katiba mpya na nzuri lazima tuliwe na FFU. Jamaa watatupiga kweli kweli, na mimi nahisi watatuua hasa, lakini hakuna jinsi.....sasa nasema baasi, mwanangu T mie babako nipo tayari kwenda vitani barabarani, kitakachonikuta Mungu atakulinda wewe, jipe moyo, bora kufa kuliko kuishi huku unadhalilika. Nasubiri tamko.....!

nina bro wangu ni askari, anasema, yakitangazwa, ataanza kuvaa kiraia ili naye afe na watanzania. na akilazimishwa kubeba bunduki, basi atakufa na askari wengi vipofu
 
wajinga ndio wali wao lakini nchi ikiwa na idadi kubwa ya wajinga, inawaweza kutupeleka kubaya kama tunakoelekea sasa!
Ndio maana wazungu wanajitahidi kufadhili elimu kumbe.
Who did not expect this one?
 
Kombani anasema wamekaa na kamati,wamekaa na wananchi wengi tu na wamezingatia maoni yao,huyu mama hata simuelewi kwa kweli,yaani ni utani utani tu!!nchi hii bwana!
 
Du! Kwa hiyo ccm ndo wameamua kufanya maamuzi ya wananchi wote zaid ya 45mil, kwel wanataka makubwa!
 
Yaani anavyohitimisha na kuongea kwake pasipo kujiamini wala kujua akiongeacho, ni kituko. Anadhani anaonge na mke mwenzake aliyempora mume hapa. Anapendekeza eti wabunge wa chadema walipaswa wagome kutoka nje ya bunge kwa kama wangejua kuwa Mheshimiwa Tindu Lissu alitukana ktk haotuba yake. Then anajichanganya kwamba kutoka kwao eti wamekubaliana na matusi yalotolewa na Tindu Lissu.

Kuna haja ya huyu mama kuondolewa kwenye hii wizara, maana inaonekana mambo mengi sana hayajui kabisa. Ni mzigo sio ktk wizara hiyo bali ktk nchi pia.

Sijui tutafika wapi na huyu mama!
 
waziri wa sheria na katiba anatoa majumuisho ya michango ya wabunge juu ya "janga linaloendelea" kutokana na ukosefu wa michango nae kajikita kumjadili JEMBE LETU Tundu Lisu, hali kadhalika nae Ag Hakua na jipya ni kumjadili Lisu tu.
 
Nani atasimamia hilo zoezi? kama ni tume ya Taifa ya uchaguzi basi hakuna kinachofanyika maana hata tume yenyewe siyo huru!!!!!!!!! Hizi nguvu wanazotaka kuzitumia CCM nahisi kama damu yaweza kumwagika TZ Mungu aepushie mbali


Hilo daftari lina makosa mengi na linapaswa kutengezwa upya.

Tanzania haiwezi ikawa na wapiga kura Millioni 27. Ni wengi mno. Haiwezekani kila uchaguzi tukaambiwa kuwa wamejitokeza 40% ya walioandikishwa.
 
Back
Top Bottom