Tofautisha

MATESLAA

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
1,246
74
Ndugu wasomi tumepewa kazi na prof tutofautishe kati ya tundu na tobo naomba mnisaidie jamani wasomi wenzangu
 
Hiyo kama sio bcom basi telecom eng.... Huyo prof nae mchokoz sasa mambo ya tundu na tobo yeye ya nini? Au anamtetea Cameron nini?
 
tundu...mfano toto tundu. Tobo sijui maana yake.....ahahahaah!!
 
Tundu ni sehemu iliotoboka au kutobolewa ambayo inamwisho,haitokezei upande wa pili.

Tobo ni sehenmu iliotoboka yanyewe au kutobolewa kwa maksudi ila hii hutokezea upande wa pili. yani unaweza kuona upande mwengine ukichungulia.
 
Wakati wa kutoboa, tobo , tobo, tooo...

Wakati wa kutunduwa tundu, tundu, tuu...

Umeelewa au bado nikufafanulie?
 
ishu iko kati ya Tundu, Tobo na Shimo.
1. Shimo ni kama jalala ama Kaburi.
Huchimbwa kwenda chini ardhini.
2. Tundu ili liwe tundu ni lazima uuone upande wa pili.
3. Tobo ni kama vile ukigongelea msumali ukutani kisha ukautoa, basi pale linalobaki ni tobo.
Na endapo utafanikiwa kutoboa mpaka upande wa pili basi litakuwa tundu...
 
Ahahahaah!! Mimi sijaelewa nifafanulie.

Kuna Mganga wa kienyeji zama ni sana alikuwa maarufu kama alivyo Profesa Maji Marefu kwa sasa, akiitwa Mtoboa Tobo.

Na kuna kijana mmoja machachari wa Chama cha upinzani anaitwa Tundu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom