Tofauti yetu na wao....

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,185
307
Kipima Joto ya ITV cha jana kimezidi kutudhilishia umuhimu wa kufanya madiriko ya uongozi wa nchi yetu. Katika safu ya watu wanaendesha nchi yetu tuna watu wengi sana wa aina ya Tambwe Hiza, Makamba, Chiligati, JK, viongozi wa UVCCM, n.k kwa bahati mbaya hawa wanaweza kuwa waaminifu wakiwa wamezungukwa na watu wenye weledi wa RA, EL, Somaiya, n.k. ambao nia yao kubwa ya kuchanganyikana na hawa watawala wetu ni kuchuma kutoka kwenye shamba la bibi yao (tz).
Ukiangalia namna ambavyo Tambwe, Makamba, na hata JK wanavyojenga hoja zao utajua kuwa mikataba ya aina ya Dowans, RITES, n.k. iko hapa kuwa sehemu ya maisha yetu mpaka pale tutakapobadilisha chama kilichoko madarakani. Kwa sasa nchi yetu iko mikononi mwa wananchi ambao weledi wao ni wastani au chini ya wastani (very average and or below average citizens)

Kwa upande mwingine hebu jaribu kuangalia safu ya uongozi kwenye vyama vya wenzetu kama Labour/Conserv/n.k kwa UK au Republican/Democrat/n.k. USA utaona kuwa viongozi wao wote wa juu wana weledi wa hali ya juu (extra ordinary citizens)

Hatari kubwa ya kuwa na "average" ni kuwa wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa wanazungukwa na watu ambao wanawazidi weledi ili wawe salama (they suround themselves with assistants who are either less competent or with competency of their level) na hao wasaidizi wao ndio wanatarajiwa waridhi hizo nafasi zao.... watu wa aina hii hufanya kila liwezekanalo kuwaondoa wale wote wenye weledi unaowazidi wao ili kusudi wasionekane hawafai.

Ni wakati sasa wale wananchi ambao ni "extra ordinary" wajitokeze na tuwape fursa watutawale.
Tunahitaji watu wenye weledi wa Mwl Nyerere, Dr Slaa, na Barak Obama, n.k wawe marais na au mawaziri kwenye serikali zetu. Hatutaki tena tuendelee na watu wanaoghushi vyeti vya masomo ili waonekane wasomi watutawale, hatuhitaji mawaziri wa aina ya Tambwe, tunataka mawaziri wa aina ya Mnyika, Lisu, na wengine wanaoweza kujenga hoja zao kwa weledi unaostahili, vinginevyo.........................
 
YANI TAMBWE MICHANGO YAKE YA JANA ILZIDIWA HATA NA MTOTO WA DARASA LA KWANZA ,NADHANI LENGO LAKE HASA LILIKUWA NI KUVURUGA MJADALA NA ALIFANIKIWA KWA KIASI FULANI,HATA HIVYO TAMBWE YUPO KITENGO CHA PROPAGANDA(UONGO) NA LIFANIKIWA KUENEZA UONGO WAKE INGAWA SIJUI KAMA KUNA MTZ MWENYE AKILI TIMAMU ANAYEWEZA KUMWELEWA.:shock:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom