Tofauti ya wanaume na wavulana.......kitabia...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,063
115,462
1.Mvulana atatembea na msichana bila kinga,halafu akiletewa taarifa ya mimba,ataruka
na kukimbia....Mwanaume atajadili na huyo msichana nini kifanyike.....

2.Atamuacha mkewe ambae hana kazi wala biashara bila matumizi ya kutosha..
halafu ataanzisha ugomvi mkubwa akihisi mkewe 'anatoka nje'....Mwanaume atapigania
mahitaji ya mkewe na watoto kwanza kabla ya kuanza 'kuunguruma'nyumbani..

3.Mvulana akipata mshahara moja kwa moja bar na atarudi nyumbani kesho yake....
Mwanaume ataingia bar pale anapoona hali inaruhusu tu...

4.Mvulana atashangaa 'kudondokewa na kuzimikiwa na mwanamke'
Mwanaume hushangaa kumtongoza mwanamke na 'kumkosa'

5.Mvulana akimnunulia bia mwanamke lazima 'alipwe'
Mwanaume huwa hadai 'malipo' kwa kumpa bia au favour mwanamke
but anaweza tu kukataa akiona sio lazima..

6.Mwanaume hujali zaidi 'heshima' yake....
Mvulana hujali zaidi 'tamaa' yake....

7.Mvulana hupiga kelele au kuguna guna au kutoa sauti au kubadilika tabia
akiona 'mrembo ' kaingia au anapita karibu...
Mwanaume hujifanya hajaona kitu,sana sana akiamua 'huchukua hatua'
muafaka....kimya kimya...

8.M wanaume hukubali kukosa kama gharama za kupata ni kubwa mno...
Mvulana hung'ang'ania 'apate' hata kama gharama 'zitamuumiza' ...

9. Mwanaume huwa 'anajifunza 'kila siku
Mvulana huamini 'anajua' yote...

10. Mwanaume hufikiria maisha kwa ujumla na 'future' ya watoto...
Mvulana anafikiria pamba,magari,warembo 24/7......


Mengine mnaweza kuongezea.......wanasema kuna 'mvulana' kwa kila mwanaume
but wengine huwa wanabaki kuwa 'wavulana' milele.........lol......

ANGALIZO= HAPA NAZUNGUMZIA WATU MNAOFAHAMIANA TAYARI SIO ONLINE PEOPLE AMBAO HUJAKUTANA NAO
NA UANZE KU WA JUDGE KWA POST TU ZA HUMU...
 
kumbe kuna wanaume na wavulana eeeh ngoja nitafute wanaume sasa
 
ulikuwa hujui??? lol
nilikuwa sijui umenifungua macho na nimecompare nimeona ni kweli pia umesahau mwanaume hapendi kabisa mwanamke ampe chochote ila wavulana wanapenda sana marejesho yaani akikupa kitu leo anategemea kitarudi mfano akikupa hela leo wk ijayo atajifanya mmezoeana na wewe umpe eti mambo si mazuri
 
nilikuwa sijui umenifungua macho na nimecompare nimeona ni kweli pia umesahau mwanaume hapendi kabisa mwanamke ampe chochote ila wavulana wanapenda sana marejesho yaani akikupa kitu leo anategemea kitarudi mfano akikupa hela leo wk ijayo atajifanya mmezoeana na wewe umpe eti mambo si mazuri

labda marioo...
mariioo wote ni wavulana hata kama ana miaka 50..lol
 
hapo uliposema kuna wengine watabaki kuwa wavulanaaaaaaaa milele ni balaa ngoja nimsome huyu wa kwangu yupo kiumeni ngapi na kivulana ngapi? kama sio mwanaume nampiga chini
 
I love U for this, that's why I can't date. Sikutani na wanaume, nakutana na wavulana tu ambao hata ukiongea haelewi unaongelea nini.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom