Tofauti ya mzaha na utani

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,625
Habarini wajumbe .....

Nipo hapa kuwaelekeza tofauti kati ya mzaha na utani.

Kwa kipindi kirefu haya maneno yamekuwa yakitumika kwa kufananishwa........ila yanabeba maana mbili tofauti. Nitaanza na neno mzaha kisha nije neno utani.

MZAHA.
Neno hili hutakiwa kutumika kumaanisha matendo ya masihara.....ya kejeli .....ya kizembe au kuzembea......au ukosefu wa umakini kabisa katika kufanya au kusema jambo.
Tafasiri ya neno mzaha mtu anapolitumia kwako kwa ufasaha inamaanisha kuwa matokeo ya unachokifanya yataleta madhara kwako au kwa wanao kuzunguka.....

kwa mfano wa1. Rafiki yako anasafiri na ameamka kisha wewe kwa makusudi umeficha viatu vyake na kwa lengo la kucheza naye akili ili kujifurahisha bila kuzingatia madhara ya yeye kuchelewa safari au kuachwa na basi au ndege kujumlisha hasira atakazokuwa nazo.........huo unaitwa ni mzaha.

mfano wa 2....ukachukua pistol ya baba yako bila kujua kama ina risasi ama la kisha ukakatoka nayo nje walipo wenzako ukawanyooshea kwa kutaka ufanye kituko huo unaitwa mzaha maana ni muda wowote inaweza tokea ajali au maafa ya kufyatuka risasi na kuua mtu bila dhamira ila kwa kusudi.

Mfano wa 3......ukimwita mtu mnene kwa jina la kibonge au nguruwe...au kiboko au tembo au manyama uzembe kwa lengo la kufurahisha wengine hiyo ni kauli ya mzaha ambayo inamadhara kwa muhanga upande wa pili ambaye kauli hiyo imemuelekea.......

Mfano wa 4; Umeolewa au umeoa na ukashindwa kulinda hadhi ya cheo ulicho nacho kijamii cha mke / mume wa mtu kwa kufanya mambo bila staha kama kushikana hovyo na wasichana au wavulana.......kukaa baa unalewa na kufanya vituko....kuwa na mahusiano nje ya ndoa yako kwa usiri mkubwa......au kuchezea pesa za mwenzi wako kwa mambo yasiyo na tija kwafamilia yenu haya matendo yote huitwa ni mzaha.

Hivyo basi mzaha ni matendo au kauli yeyote inayofanywa na muhusika kwenda kwa mtu au kundi la watu wengine bila kuzingatia madhara yake kwa kina.

UTANI

Utani ni matendo au kauli zenye uzani au vipimo vinavyozingatia mrejesho wa hisia za upande wa pili. Maana ya neno utani ni matendo au kauli ambazo zinazofanyika bila kuleta madhara yaani ni tayari kunakuwa na ulinganifu umefanika katika akili ya mfanyaji utani akijua kabisa kuwa anachokifanya ni zero (0%) damage result oriented action.Madhara yanayozungumziwa hapa ni ya physical au emotional.......!

mfano wa 1. Rafiki yako anatafuta viatu vyake ambavyo umevificha......ila wewe unajua kuwa ratiba ya safari imebadilika hatotakiwa kuondoka siku hiyo ila yeye hajajua bado sasa unaitumia fursa hiyo kufanya utani kwa kitendo ambacho hakita kuwa na madhara yeyote kwa maana atakasirika atakapojua ulificha viatu ili umchemshe ila umemjulisha habari mpya kuwa safari haipo tena hadi kesho labda na ni habari ambayo yeye ataifurahia huo ni utani.

mfano wa 2: Ukachukua pistol ya baba yako.....unaufahamu wa kutoa risasi katika pistol na kujua kuitumia. Unaichukua pistol hii unakwenda nayo kwa wenzako ukijua wazi haina risasi kwenye magazine wala chemba unawaelekezea na kufanyia utani ukijua hakuna ambaye anaweza pata mshituko wa kuhatarisha afya yake kama presha then mwishoni ukawajulisha huo unaitwa utani.

Mfano:3 Ukimwita mtu mnene baby.....lazizi wangu......my beyonce....my teddybear.....my delicious pumpkin.....majina ambayo hata yeye atajua wazi kuwa yanalenga kutokumfedhehesha mbele ya wengine bali kumfanya ajisikie comfortable mbele za wengine na hali yake ya muonekano wa mwili huo ni utani.

mfano wa 4. Umeolewa au umeoa halafu ukamwita dada wa mkeo mke mkubwa.......au bibi wa mkeo ukamwita mke mkubwa au nyumba ndogo.....au kwa mwanamke ukamwita babu wa mumeo buzi langu.......mdogo wa mwisho wa mumeo suppoz ana miaka kuanzia 0 hadi 18 ukamwita mume mdogo huo ni utani kwa maana haleta hisia tofauti katika mawazo ya unayemfanyia utani kama ni mumeo au huyu unayetaniana naye.......

Hivyo basi utani ni matendo au kauli vinavyozingatia matokeo ya hicho kitendo au kauli kwa anayefanyiwa......

Kwahiyo ndugu zangu katika jamii tunazoishi, kitendo kuchukuliwa kama ni Utani au mzaha itategemeana na aina ya watu wenyewe ila cha msingi au kanuni ya kuzingatia ni kuwa kitendo au kauli ambavyo kinaqualify kuitwa utani huwa kina matokeo yasiyo kuwa na madhara yoyote kwa muhusika au wahusika upande wa pili ila kama hicho kitendo ni kina matokeo ya madhara either kwa kuumiza hisia za mtu/ watu au kikaleta madhara kama watu kukosana....kuumia.....kuchukiana......then huo si utani ni mzaha.

ASANTENI KWA KUSOMA.
 
ni sawa tu na tofauti kati ya vimemo na ushauri
 
Back
Top Bottom