tofauti ya miaka 25 kati ya wanandoa ni sawa?

Pretty

JF-Expert Member
Mar 19, 2009
2,575
552
Habari wana JF,
Kuna mwanaume ana umri wa miaka 50, kapata msichana wa miaka 25. Huyo mwanamume kampenda binti na anataka kumuoa, binti naye kampenda huyo baba.
Mwanaume hajawahi kuoa, alikuwa bado anajiandaa na maisha vizuri.
Maswali yangu,
1) Umri huu ni sawa kwa wanandoa kupishana?
2)Je kwa umri wa mwanaume, anaweza kuperform kazi yake vizuri ya ndoa kama mwanaume?
Huyo binti kampenda kweli huyo mwanaume, kaja kuniuliza haya maswali, nami nikaona niwashirikishe. Mnasemaje wana JF kuhusu hili?
 
Wanawake bwana..Ina maana vijana mashababi wameisha au ndo yale mambo ya kutaka mteremko?
 
Kampenda mwanaume au kapenda mshiko wake? Ushasema mwanaume alikuwa anajiandaa kwa maisha! Naamini mambo safi ndo maana ameamua kuoa, hivyo demu hakumpenda bali kapenda pochi lake.
Huyu bwana mzee naye anatafuta pressure bure. Binti wa miaka 25 kazi kwelikweli kumlea. Ukianzia rigwaride mpaka kwenye starehe za nje. Mtu wa miaka 25 anataka bado kujirusha na amini kuwa hatatoka na mtu ambaye sura ilishaanza kujikunja.
Huu ni usanii wa mapenzi kama ilivyo sehemu nyingi za coast ambako wasichana wengi wanataka kuolewa na vizee vya kizungu. Ukiuliza kisa wanakwambia "kwani huyu na muda gani kufa".
 
Mwanaume wa 50 years kwa miaka ya sasa anaweza kuonekana bomba vibaya sana tena idara zote - including ofcourse financial capability.
Mshauri rafiki yako kama ifuatavyo:
1.Ausikilize moyo wake..kisha aamue maana mwisho wa siku ni yeye,huyo mumewe na Mungu wao.

2. Kama ni forward looking basi ajitayarishe kuja kumlea huyu "mumewe" na watoto alee/wasomeshe peke yake.Sasa ana 50-25.By the time she is 45 na majukumu ya kusomesha watoto college na nini he will be 70 akihitaji msaada.Is she prepared for this?
 
Kuna mwanaume ana umri wa miaka 50, kapata msichana wa miaka 25. Huyo mwanamume kampenda binti na anataka kumuoa, binti naye kampenda huyo baba.

Kama wamependa kweli ni vizuri maana wataweza kukabili vizuri changamoto zitakazotokana na tofauti ya umri. Ni vizuri wakaweka wazi matarajio yao ili waone kama yanaendana au wanaweza kuyafanikisha kwa pamoja. Inawezekena mwanaume hafikirii habari ya kuzaa wakati binti anataka kuwa na watoto!

Mwanaume hajawahi kuoa, alikuwa bado anajiandaa na maisha vizuri.

HAkuwahi kuoa? Hajazaa pia? Huyo binti inabidi afanye uchunguzi wa kutosha kabla ya kufanya maamuzi. Na mbona amejiaandaa muda mrefu hivyo? Napata hisia kwamba kuna tatizo jingine na si kujiandaa pekee. Hata hivyo kama ni kweli amejiandaa, then nadhani hilo pia ni bora kwani atakuwa ameandaa mipango madhubuti ya kulea 'wajukuu'.

1) Umri huu ni sawa kwa wanandoa kupishana?

Umri si issue sana kama kuna mapenzi ya kweli kati ya wawili hao. Likely kutakuwa na incompatibilities nyingi tu kati yao lakini kama wanapendana watakuwa tayari kuzi-absorb. By the way Mandela na Graca wamepishana miaka 27!!

2)Je kwa umri wa mwanaume, anaweza kuperform kazi yake vizuri ya ndoa kama mwanaume?

Yes anaweza lakini si kama kijana wa miaka 28!
 
Mimi sioni tatizo kama watu wamependana hamna shida kuna wanaume wengine umri umeenda lakini bado wana afya njema na huwezi kudhania kama ana miaka 50 , kama yeye kampenda waendelee na mambo yao maana hata sisi tukishauri haisaidii.
Mpaka huyo bitni anaomba ushauri tayari alikuwa na maamuzi yake kichwani alichotaka kujua ni kwamba watu wa nje watamfikiriaje,mwisho wa siku ni yeye ataishi naye sisi hatupo.
 
Ila huyo mwanamke kapenda maisha safi ya huyo jamaa na anaweza kumsaliti mwanaume hapo baadaye.

Life is a gamble ndugu. Mwanaume anabahatisha mdada mwenye umri mdogo akidhani huko mbeleni atamsaidia, mdada nae anajaribu bahati yake.Yatakayotokea huko mbele ni majaliwa.TUWAOMBEE HERI TU.
 
Habari wana JF,
Kuna mwanaume ana umri wa miaka 50, kapata msichana wa miaka 25. Huyo mwanamume kampenda binti na anataka kumuoa, binti naye kampenda huyo baba.
Mwanaume hajawahi kuoa, alikuwa bado anajiandaa na maisha vizuri.
Maswali yangu,
1) Umri huu ni sawa kwa wanandoa kupishana?
2)Je kwa umri wa mwanaume, anaweza kuperform kazi yake vizuri ya ndoa kama mwanaume?
Huyo binti kampenda kweli huyo mwanaume, kaja kuniuliza haya maswali, nami nikaona niwashirikishe. Mnasemaje wana JF kuhusu hili?

Age aint nothing but......
1. Kupishana miaka 25 ni mingi sana..,hapo wanakuwa kama baba na bintie! Ila kama msichana ameridhika na hilo its up to her to decide.
2. Kuna msemo wa "ng'ombe hazeeki maini" so wanaume wa miaka 50 anaweza kuperform kazi yake bila matatizo kama afya yake ni njema.
 
Habari wana JF,
Kuna mwanaume ana umri wa miaka 50, kapata msichana wa miaka 25. Huyo mwanamume kampenda binti na anataka kumuoa, binti naye kampenda huyo baba.
Mwanaume hajawahi kuoa, alikuwa bado anajiandaa na maisha vizuri.
Maswali yangu,
1) Umri huu ni sawa kwa wanandoa kupishana?
2)Je kwa umri wa mwanaume, anaweza kuperform kazi yake vizuri ya ndoa kama mwanaume?
Huyo binti kampenda kweli huyo mwanaume, kaja kuniuliza haya maswali, nami nikaona niwashirikishe. Mnasemaje wana JF kuhusu hili?

Kwani wanamuda gani katika mahusioano yao kabla ya kufikia maamuzi ya kuoana?Je hawajawahi kudo hata siku moja ili kuthibitisha swali no.2 alilouliza dada yetu?
na kama walishadoo alifanya ulinganifu kati ya perfomance ya huyo mzee na kijana mwenzie aliyewahi kudo nae ''Hopefull atakuwa siyo bikira''.
 
Hili ni swali la kisanii na anayeuliza ni msanii vilevile... anajua kabisa anachotaka kufanya ni kitu cha ajabu kwenye jamii. Hana haja ya kuuliza yeye aendelee tu. Sijui asili yake ya wapi, definitely sio wa 'pwani' maana sie hilo kawaida sana kwa nyumba ya pili, tatu na kuendelea. Kwa mke wa kwanza hata kwetu gap hiyo inatisha. Namshauri aendelee kimyakimya tu wala asimtangazie mtu.
 
Ni poa tu! Wasije wakazeeka wote pamoja- mama awe na nguvu za kuangalia familia!

Je mngetaka atafute mwanamke wa miaka mingapi? Miaka 45?

Hata Zuma ameoa tu juzi mke ana miaka 34 na Zuma is 67!

Mwanamme hazeeki maini!
 
Last edited:
Kama wamependa kweli ni vizuri maana wataweza kukabili vizuri changamoto zitakazotokana na tofauti ya umri. Ni vizuri wakaweka wazi matarajio yao ili waone kama yanaendana au wanaweza kuyafanikisha kwa pamoja. Inawezekena mwanaume hafikirii habari ya kuzaa wakati binti anataka kuwa na watoto!

HAkuwahi kuoa? Hajazaa pia? Huyo binti inabidi afanye uchunguzi wa kutosha kabla ya kufanya maamuzi. Na mbona amejiaandaa muda mrefu hivyo? Napata hisia kwamba kuna tatizo jingine na si kujiandaa pekee. Hata hivyo kama ni kweli amejiandaa, then nadhani hilo pia ni bora kwani atakuwa ameandaa mipango madhubuti ya kulea 'wajukuu'.

Umri si issue sana kama kuna mapenzi ya kweli kati ya wawili hao. Likely kutakuwa na incompatibilities nyingi tu kati yao lakini kama wanapendana watakuwa tayari kuzi-absorb. By the way Mandela na Graca wamepishana miaka 27!!

Yes anaweza lakini si kama kijana wa miaka 28!

Una uhakika?
 
Maswali yangu,
1) Umri huu ni sawa kwa wanandoa kupishana?
2)Je kwa umri wa mwanaume, anaweza kuperform kazi yake vizuri ya ndoa kama mwanaume?
Huyo binti kampenda kweli huyo mwanaume, kaja kuniuliza haya maswali, nami nikaona niwashirikishe. Mnasemaje wana JF kuhusu hili?

...haina shida hiyo, ....hata Madiba (1918) na Graca (1945) wamepishana 27!...

JOHANNESBURG -- President Nelson Mandela celebrated his 80th birthday yesterday by marrying Graca Machel, the former first lady of Mozambique, in a private ceremony at his suburban house.

Breaking a tight web of official and family denials late yesterday afternoon, Deputy President Thabo Mbeki, who acted as Mandela's best man, delivered the news: "I have a very short statement to make and a very happy one. President Mandela and Graca Machel got married this afternoon."

...nami nikigonga '80yrs young' naweka 'vunja mifupa' mwingine ndani!
 
Ila huyo mwanamke kapenda maisha safi ya huyo jamaa na anaweza kumsaliti mwanaume hapo baadaye.

Kweli kabisaa....nina mfano hai dada yangu amefariki na miaka 42 amemwacha shemeji ana miaka kama 55 na watoto 5, chakushangaza binti wa kazi aliyeishi nae kwa miaka zaidi ya 6 ambaye sasa ana miaka kama 23 ameolewa na huyo baba na wameshazaa mtoto. yaani wakiongoozana ni baba na mtoto hata kwa maumbile binti ni mdogo na bonge la jibaba.
 
chakushangaza binti wa kazi aliyeishi nae kwa miaka zaidi ya 6 ambaye sasa ana miaka kama 23 ameolewa na huyo baba .

kweli ndugu yangu inashangaza saaaana!
they must have been having sumsing going on hata kabla sista hajafariki!
 
Habari wana JF,
Kuna mwanaume ana umri wa miaka 50, kapata msichana wa miaka 25. Huyo mwanamume kampenda binti na anataka kumuoa, binti naye kampenda huyo baba.
Mwanaume hajawahi kuoa, alikuwa bado anajiandaa na maisha vizuri.
Maswali yangu,
1) Umri huu ni sawa kwa wanandoa kupishana?
2)Je kwa umri wa mwanaume, anaweza kuperform kazi yake vizuri ya ndoa kama mwanaume?
Huyo binti kampenda kweli huyo mwanaume, kaja kuniuliza haya maswali, nami nikaona niwashirikishe. Mnasemaje wana JF kuhusu hili?

Huyo dada kafuata vitu hapo, hajamfuta mtu,
Vikisha hivyo vitu, atatafuata mtu,
Huyo dada anapenda mali, hapendi mtu!

Namhurumia kuwa atakuja kuwa mjane mapema na kupenda kwake vitu, vitamtokea puani hapo wenye vitu (watoto alozaa pembeni ) watakapokuja kudai vitu vyao.

Pretty wala usijidanganyike kirahisi kuwa huyo baba hajawahi kuoa katika umri huo! KAma ni wewe basi fikiria mara 50 dada yangu.
 
Habari wana JF,
Kuna mwanaume ana umri wa miaka 50, kapata msichana wa miaka 25. Huyo mwanamume kampenda binti na anataka kumuoa, binti naye kampenda huyo baba.
Mwanaume hajawahi kuoa, alikuwa bado anajiandaa na maisha vizuri.
Maswali yangu,
1) Umri huu ni sawa kwa wanandoa kupishana?
2)Je kwa umri wa mwanaume, anaweza kuperform kazi yake vizuri ya ndoa kama mwanaume?
Huyo binti kampenda kweli huyo mwanaume, kaja kuniuliza haya maswali, nami nikaona niwashirikishe. Mnasemaje wana JF kuhusu hili?

Namfahamu mtu ambaye anapishana na mke wake 20 (kasoro miaka 5 kufikia ya huyo bwana). Sijui kama wake alishawahi kupungukiwa kitu - sexually etc. Kila siku wanaonekana kama - they have made the right choice to be able to meet and marry.Siyo rahisi ku'define' who's the right partner katika ndoa. You can only define or talk about your own experience.After all, upendo ni wa kwanza na mengine yanafuata.
 
Last edited:
Back
Top Bottom