Toa maoni yako juu ya wagombea hawa wa BAVICHA (Chadema) taifa

MIE NAWAFAGILIA
Mwenyekiti - Silinde David (Mbozi)
Makamu - Sharifa (Zanzibar)

Katibu - Deo Munishi (Moshi)
Naibu Katibu - Odero Oderos (Rorya)

Hawa ni vijana walio makini na uwezo wa kukieneza chama hadi vijijini badala ya mijini tu

kwa uhakika upi ulonao?
 
tunaomba cv na evidence za mambo waliyowahi kuyafanya ili tupime nia na mioyo yao kama kweli wako tayari kupambana mpaka kieleweke. Tukumbuke unapotaja chadema cha kwanza kuja kwenye akili ya mtanzania ni vijana. Tunatakiwa kuwa na viongozi wazuri zaidi wenye moyo mkuu kuliko hata mwenyekiti na viongozi wakuu wa chadema. Sasa ni muda wakati mugmu kwa chadema inahitaji watu wenye moyo wa kujitoa wasio na tamaa yakuweza kukihujumu chama kwa namna yoyte ile.
Tunahitaji akina mnyika, wenje,lema wengine ambao wako tayari kupambana.
Napendekeza walio na nafasi tayri kama wabunge wasigombee tunahitaji vipaji vingine pia viingie ndani.
Naam, umenena vema. Kwa kuwachagua viongozi wasio na majukumu makubwa hasa katika nafasi ya M/kiti itasaidi mteule huyo kufanya shughuli za kichama kwa ufanisi mkubwa. nadhani Bw. Heche atafaa zaidi hasa kwa ujasiri wa kusimamia mambo na uwezo wa kujenga hoja.
 
Kama nitapata Cv ya Heche itakuwa vyema kumjaji, maana ni mpambanaji kwa asili kutokana na mambo aliyoweza kuyafanya, na nafasi ya Mwenyekiti au Katibu Mkuu anatakiwa mtu asiyeogopa mabomu wala kusimamia maamuzi kwa njia yoyote ile itakayoamuliwa. Naomba tu nifahamu elimu yake, maana uongozi wa kisasa bila ya kuwa angalau graduate ni hatari.

Jamaa ni graduate mkuu wa SAUT
 
Heche toka lini ukawa wa rorya! Tarime imekuaje?unaogopa nini kujitambulisha wewe ni wa tarime ! Je huoni ubabaishaji umeanza?
 
i have seen Narasi during kampeni, i think he is a gem

Hivi wale waliosema CDM ni chama cha kaskazini wako wapi???
 
Ni ngumu kutoa tathmini bila kujua cv zao ili tujue vizuri wafanye kama alivyofanya ben
 
[JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NA SERA YETU YA MAMBO NJE. [/COLOR][/B][/SIZE][/FONT]

“Natoa onyo kuwa serikali isipochukua hatua ya kutazama mwenenndo wa misimamo katika siasa za kimataifa, basi upo uwezekano mkubwa wa heshima ya Rais na hadhi ya nchi kuchafuka katika medani za kimataifa”.

Nitatoa mfano.

Serikali ya Kenya kupitia Rais wake Mwai Kibaki imekataa kupeleka kesi za watuhumiwa wa vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo (post election violence) katika mahakama ya kimataifa ya wahalifu wa kivita (International Criminal Court –ICC).

Na izingatiwe kuwa katika jitihada za kutafuta kuungwa mkono, serikali ya Kibaki ilimtuma makamu wake wa Rais, Kalonzo Musyoka kufanya ushawishi wa kidiplomasia ili nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania iwaunge mkono (Shuttle diplomacy).

Umoja wa nchi za Afrika (AU) umeunga mkono msimamo huo wa serikali ya Kenya wa kukataa watuhumiwa hao wa vurugu za uchaguzi kupelekwa mahakama hiyo ICC nchini Uholanzi na badala yake wanataka watumie mahakama maalum za ndani ya Kenya (Special Tribunal Courts) kushughulikia tuhuma hizo. Serikali yetu ya Tanzania nayo kupitia AU imeunga mkono msimamo huo wa kukataa watuhumiwa hao kupelekwa ICC.

Lakini naomba itiliwe maanani kuwa msimamo huo wa serikali ya Kibaki si msimamo wa Wakenya walio wengi, kwani kwa mujibu wa matokeo ya kura rasmi ya maoni iliyopigwa hivi karibuni, asilimia zaidi ya 60 ya Wakenya wanataka watuhumiwa hao wakashitakiwe katika mahakama hiyo ya IC iliyoko The Hague nchini Uholanzi.

Pia hata Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Raila Amolo Odinga, yupo upande wa Wakenya walio wengi akipinga uamuzi huo wa Kibaki na wenzake.

Tatizo ni nini?

Tatizo ni kwamba serikali yetu kupitia AU imeunga mkono uamuzi wa serikali ya Kibaki wa kutowapeleka watuhumiwa hao ICC na jitihada za serikali hiyo za kutaka kujiondoa kwenye mkataba wa kimataifa wa Roma (Rome Statue) wakati Wakenya walio wengi hawataki.

Ikumbukwe Tanzania ilipata fursa ya pekee ya kuwa msuluhishi wa mgogoro wa kisiasa nchini Kenya baina ya upande wa Kibaki na Odinga, heshima hiyo tulipewa kwa heshima ya kuaminiwa (Honest broker) katika kusimamia matakwa ya Wakenya.

Na kwa kutambua mchango wa nchi yetu, Rais alipewa zawadi ya kutunukiwa shahada ya udaktari wa falsafa wa heshima kutoka Chuo Kikuu cha Umma cha Jomo Kenyatta.

Kwa mantiki hiyo, kwa msimamo ambao serikali yetu imeonyesha, wa kutofautiana na Wakenya walio wengi (zaidi ya asilimia 60), ni dhahiri upo uwezekano kwa nchi yetu kujiingiza katika mgogoro wa kidiplomasia baina yetu na wananchi wa Kenya.

Upo uwezekano pia wa nchi yetu kujiingiza katika mgogoro wa kidiplomasia baina yetu na serikali ya Kenya katika siku za usoni kama Rais wa nchi hiyo atakuwa Raila Odinga wa chama cha ODM ambaye tayari ameshatangaza azima yake ya kuwania urais wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao wa 2012.

Ninatoa wito wa kumtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta, kutoa tamko la kuueleza umma wa Watanzania kwanini wameiingiza nchi yetu kwenye msimamo unaopingwa na Wakenya wengi ambao ni majirani zetu na ni ndugu zetu wa karibu. Je, waliona ni busara tu kumuunga mkono Kibaki na wenzake wachache na kupuuza matakwa ya
Wakenya walio wengi?

Je hawaoni kwa kufanya hivyo wanalichonganisha taifa na majirani zetu wa karibu?
Katika hali ya kawaida nilitarajia kuona serikali yetu ikiheshimu matakwa ya Wakenya na msimamo wetu wa awali ambao ulikuwa ni kusimamia maslahi ya Wakenya walio wengi.
.

.

Siiungi mkono hoja hii kwa kuwa imebase kwenye hofu badala ya ideology yetu kama taifa huru, lenye maamuzi binafsi.

Tutakuwa ni nchi ya ajabu sana kama foreign policy yetu itakuwa inayumbisha kama upepo kufuatana na umaarufu wa maamuzi yetu kwenye nchi zingine badala ya nini sisi kama nchi tunaamini, katu huo haukuwa msingi wa siasa yetu ya nje chini ya Mwalimu na haupaswi zaidi kuwa msingi wetu wa maamuzi leo na siku nyingi zijazo.

Mathalani, kama ukiogopa kuiunga mkono Kenya kujitoa ICC kwa kuhofia kuathirika kwa uhusiano wetu na Kenya kama Raila Odinga atashinda urais mwakani, ingekupaswa usiishie hapo bali uogope pia kuipinga Kenya kujitoa ICC kwa kuhofia pia kuadhirika kwa uhusiano huo pindi team ya Group of Seven inayoongozwa na vinara wa Ocampo Six Uhuru Kenyatta na William Ruto itakapochaguliwa kuiongoza serikali ya Kenya mwakani kama inavyotarajiwa.
 
Wenye hoja ya kuwachagua watu eti kwa sababu ya 'kupunguza maneno ya udini' wanaleta wasiwasi; ningeomba umakini utumije. Lengo ni kupata kiongozi wenye sifa zinazohitajika; na sidhani dhehebu au uumini wa dini fulani ni moja ya vigezo!

Naomba tusiingie kwenye mtego ambao baadaye utaleta matatizo makubwa. Let's not loose our FOCUS!
 
Habibu mchange anafaa kuondoa ile dhana ya udini!

Sifa za mgombea na nia ya dhati ya kujenga chama bila kujali jinsia, dini, kanda au maumbile ndivyo vitakavyotumika. JK kaharibu nchi kila mtu sasa ni udini udini udini. Hakuna mtu anabaguliwa kwenye dunia ya leo kama anajituma na kutimiza wajibu wake, siasa za kubebwa zimepitwa na wakati. Ndio maan huko lumumba ni January, Nape, malecella, mwinyi, Kolimba, Karume, bila kujali sifa bali jina la mwisho.
 
1. Nassari Joshua --- namfahamu vizuri sana nilisomanae o-level, nina mashaka sana na maamuzi yake labda kama alikuja kubadilika baadae (huwa ni mkurupukaji) na swala la makundi nahisi linaweza kuibuka kwa ninavyomfahamu. msinione ninachuki binafsi, hapana, lengo ni kuiproject CD tunahitaji kiongozi type ya dr. P.W. Slaa. Nadhani joshua hapana,hapana,hapana,,

4. Habib Mchange ( kibaha pwani)--- nilipata kumuona kipindi cha uchaguzi ninahisi busara ipo pale,

Jamani kila lisemwalo lipo kama halipo linakuja ukijaribu kuongea na wana Arumeru hasa vijana hawaamini kama huyu dogo alishindwa ubunge kweli wanadai alivuta chake akakaa pembeni na hiyo siri imevuja kwa muda mrefu huku ila siyo vizuri kutuhumiana bila ushahidi lakini ni vizuri chama kuchunguza hili jambo yasije kutokea yale ya aliyekuwa mwenyekiti wetu wa Mkoa wa Mbeya tukauza timu itauma sana na kama yeye ni msafi akae pembeni kwanza awapishe ambao hawana ka harufu ka aina yoyote ili tusiaharibiane ladha ya nguvu ya umma na umma unatujua kuliko tunavyojifahamu na ndio waliopiga kelele Kule Mbeya lakini tukaziba masikio yakatupata yaliyotupata.
Nawakilisha
 
1.Tunaomba hawa wagombea waweke Cv na motivational letter zao hapa kama alivyofanya Ben.

2.Asichaguliwe mtu kwa dini yake bali uwezo wake ( sio harusi hii ya kutafuta wahudhuriaji wa kunywa na kula)


Wasichana mbona tumejiweka pembeni au ndio tunasubiri kubebwa?
 
Siwafahamu ila kwa kuangalia Jiographia safu niliyowekea damu ya mzee ingewaondolea tuhuma za ukanda. Katibu msaidizi yeyote atawakilisha

Hiki ndo kinachoiangusha ccm kwa sasa, kuchagua viongozi kwa misingi ya jiografia badala ya uwezo. Ni vyema tuwafahamu ndipo tutoe maoni
 
Hivi kweli, CHADEMA ni wafuasi wa Kristu tu? Jinsia je? Mbona sioni majina ya akina Othman, Mohammed, Shida, Aziza, Fatuma ukiondoa huyo Sharif aliyechomekwa/jitokeza wa ZnZ?

CDM, jaribu kuwa makini na: Ka-udini na Ka-ukanda na tazameni jinsi. In whatever you do, you ought to prove wrong all the allegations over your party.

Ni ushauri tu, japo ninajua wengi wenu mtaniporomoshea matusi.....haya leteni tu.
Lawama zingine ni za kitoto nafikiri ni ukosefu wa maarifa fomu zilikuwa wazi kwa mtu yeyote kuchukua kama hao unaowataja hawakujitokeza wa kulaumiwa ni nani Chama au hao watu, je umejaribu kuwasiliana nao kwa nini hawakujitokeza labda nikuulize kwa nini wewe hukuchukua fomu jibu utakalopata linaweza kuwa sawa na la hao unaowasema.
 
hatutochagua mtu kutokana na kabila, rangi au dini yake.. kigezo kikubwa kiwe uwezo wake na dhamira yake kujenga taifa hili

kama wapo humu watoe wasifu wao naona mmoja wao(Ben Saanane) kashatoa hao wengine kama wamo humu nao watupe wasifu wao au kama kuna watu wanawafahamu basi watujuze nasi tupate kuwaelewa
 
imgres


Daddy Igogo katika maandamano ya Chadema Arusha Mwenye Kofia na shati la Khaki akimnyooshea kidole Josephine Mshumbusi

Nyuma ya Dadi Igogo ni Nassari Joshua mwenye miwani.
 
Wachaguane kwanza. Tutawaangalia wanaifanyia nini CHADEMA na TAIFA wakishachaguliwa.
 
Moderators naomba kwanza Muache kunishambulia au Kunifungia kwa Uonevu,Nilikuwa member wa huku bila jina bila kuweza kuandika baada ya ninyi kunifungia pasipo sababu za msingi mwaka jana,kisa nilikuwa na mabishano na kutokuelewana na mtu mmoja humu ndani jina nitamtaja baadae.Nikabaki kuwa msomaji tu.Hata hivyo nashukuru sana kwa kuwa members wengi najua mtaniunga mkono,sitamuonea mtu haya wala sitafuata mkumbo

Anyway,hoja yangu ni kuwa tunatambua kuwa Baraza la Vijana la CHADEMA linafanya Uchaguzi mwezi huu kama sikosei.Ningependa kuwatahadharisha BAVICHA kuwa makini na watu wafuatao kwa kadiri nitakavyowachambua

1. John Heche


Huyu ni kijana mwenye uwezo katika kukuru kakara za siasa Tanzania,alishawahi kuwa Diwani huko Tarime
Pia alishashiriki kwa kugombea Uenyekiti kwenye uchaguzi wa Mwanzo.Ni mhitimu ambaye ni mwalimu proffesionally

Lakini:-

Huyu ni mpenda vurugu na utoto mwingi.Sidhani kama ana uwezo wowote wa kuongoza CHADEMA ktk level hii ya sasa labda kama ingekuwa enzi zile CHADEMA ikiwa changa bado

Huyu naye pamoja na kuwa ameoa bado harakati zake na sketi hazijakoma,hana maadili ya kitanzania.Uchaguzi uliyopita huyu ndiye aliyekuwa Chanzo cha kuvunjika uchaguzi ule.Pia hata uchaguzi wa Tarime,huyu ndiye chanzo cha CHADEMA kukosa lile jimbo kwa sababu ya Ubinafsi wake

2.David Silinde

Huyu ni Mbunge wa mbozi.Ni kijana mwenye bidii na ana ushawishi chuo kikuu cha Dar Es Salaam.Ni mhitimu mwenye degree ya biashara

Uhusiano wake nje ya siasa za UDSM haufahamiki kwa sababu hata Bungeni sijaona jambo lolote kutoka kwake.Huyu ni bora angeachia wenzake wenye nguvu na spidi ktk kujenga jumuiya inayoendana na kasi ya mabadiliko.Kwanza huyu hana uelewano mzuri na wabunge wenzake,ni kijana asiye na dira na hawezi kujenga ushawishi kwa vijana 9kwa maana ya makundi yote ya vijana0.huyu atarudisha kasi ya mabadiliko nyuma.Ninayo ya ziada nitaeleza hapo baadae

Maadili yake ni machafu,kuokota okota vichangu mitaa ya kati tu,hana simile na mademu.Utoto umemjaa mno.Hii ni hatari


3.Ben Saanane

Huyu ni Mpole kwa kumwangalia usoni ila ......
Ni mhitimu mwenye Masters kwenye maswala ya Uhusiana wa kimataifa na Diplomasia.Ana uwezo mkubwa wa kuchambua mambo na kupanga mikakati ya kisiasa.Ni bingwa wa Propaganda

Ila ni Hatari kwa sababu

Kwanza huyuni Mzaliwa wa Kilimanjaro kanda ya kaskizini.Wandugu mnaelewa jinamizi linaloitafuna CHADEMA,Udini na ukabila.Huyu moja kwa moja hafai

Pia ,akiwa chuo kikuuu ana kashfa ya kutembe na profesa wake anaitwa Beer Sheba ambaye alikuwa visiting Professor from Hebrew University ya Israel,alisababisha hadi ugomvi kati ya Profesa Beer Sheba na dada mmoja ambaye alikuwa Ofisa ubalozi kwenye Ubalozi wa South Africa-Indiaambaye naye alikuwa anatoka na huyu jamaa,tena baada ya huyu jama kumzidi kete jamaa mmoja wa Nigeria na Mzambia waliokuwa wanamfukuzia

Pia,nakumbuka huyu jamaa wakati anagombea Urais wa serikali ya wanafunzi wa kimataifa hapo Chuoni,alitumia propaganda chafu kuwagawa wakenya.Alitumia ukabila akaweza kuungwa mkono na wakikuyu na waluya.Pia alitugawa waafrika kikanda ali ajihakikishie kura za nchi za SADC na Africa magharibi.

Pia ana Kashfa ya kumdhulumu Nape Nnauye ambaye anaheshimika hapa Tanzania na hasa vijana kwa kumuundia zengwe hadi wakampindua alipokuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi wa Acharya university kule Bangalore India,ingawa yeye hakuwa mtu jimbo lile alihakikisha amewatumia Marafiki zake akina Emmanuel oberlin ambaye alikuwa mwenyekiti mahala pa Nape Nnauye

Huyu hafai kwa sababu amekuwa na kashfa ya kushawishi kundi lake la wanafunzi wa kihindi wafanye siasa za kimabavu na ubabe hadi vurugu zikatokea na wanafunzi 12 kuuwaa na polisi 7 kuchinjwa katika zile vurugu wakati akiwa mwanafunzi chuo kikuu Allahabad,chuo kilifungwa na yeye kuhojiwa na polisi.Kwa sababu ya ushenzi wake wakaiba faili la upelelezi,huyu hafai BAVICHA

Sababu nyingine,alisababisha uhusiano mbaya na ubalozi kwa kumuandikia barua ya vitisho na kejeli huku akijua ni watu waliomzidi umri na wameteuliwa kuiwakilisha nchi,kisa kutaka atoe Amri ya wanafunzi ambao ni wafuasi wa vyama vya siasa wasifungue matawi nje na ofisi za ubalozi zisihusike.Mbona yeye hakufungua tawi la CHADEMA na kumuita balozi ili kupima uzalendo wake kwa chama?Cha ajabu ni msomi wa masuala ya Diplomasia lakini anapenda kutumia vitisho katika kushinikiza,ndiyo maana hata balozi wetu wa zamani alikuwa na uhusiano mbaya na sisis kwa sababu ya huyu jama na kundi lake la Mafia utadhani wao ndiyo ubalozi wa Tanzania

Pia,alishakuwa na kashfa ya kuingia kinyemela kwenye chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Jabalpur na kutumia mwanya wa wanajeshi waafrika akijifanya yeye ni mu-ethiopia.Haijulikani aliingiaje humo ndani na kuchukua mafunzo miezi kadhaa hadi aliposhtukiwa,kama anabisha aje huku au apige picha kidole chake aseme alikopata lile jeraha.Alipoona hali ni tight alikimbilia ubalozi wa Uingereza,imagine huyu ni mtu wa international relations,ishu yake ilitinga hadi ubalozini balozi akasema hilo swala ni kosa lake binafsi.Sasa jamani huyu si angetuingiza kwenye mgogoro na India?

Pia amekuwa na mgogoro na profesa wake wa Uchumi hadi akakaribia kuwa suspended,lakini akatumia mwanya wa kuwa na sapoti ya wahadhiri wengi hadi yule profesa akahamishwa na kupelekwa campus ya mbali.Huyu hafai kwanza ana hulka za kidikteta pale anapoona anazidiwa,yeye anaamini katika kupinduapindua tu.Hana subira,na ni mtu wa Visasi ingawa haonyeshi.Ila akipata nafasi ndipo utajua true colours,aligombana na wakisii wote wa kenya.Kila uchaguzi wao unapofika akijitokeza mkisiii hutumia mamluki kuwavuruga.Tabia chafu kama hizi si siasa hata kidogo,kuna rafiki yangu alikua anagombea uenyekiti wa wanafunzi wa kikenya alikuwa mwanafunzi wa Uzamivu amabaye sasa hivi ni lecturer kenya polytechnic University anaitwa Dr.John Bonuke,alim-frustrate hadi jamaa akashindwa kuandika thesis yake.Alihakikisha jamaa ameshindwa uchaguzi na kutumia mwanya kumpandikiza dada mmoja Mluya..yeye ni mtanzania,huko kwa wakenya kulimuhusu nini?

Hayo na mengine mengi nitayaeleza baadae.

4.Greyson

Pamoja na kwamba ni kijana aliyesomea udaktari,anakazana sana kujitokeza katika fani ya Siasa.Ni kijana anayejitolea

Hata hivyo hatambui chochote nje ya kanda ya ziwa na au huko kwingine kidogo.Huyu anafa katika uhamasishaji.CHADEMA msifanye kosa kwa kumchagua mtu ambaye ataburuzwa,yeye nimefuatilia siasa zake nikajua ni kuwa anataka kujitokeza katika ulingo wa kisiasa tu

5.Habibu Mchange

Huyu angefaa.kwanza ni muislam na hatoki kanda ya kaskazini

Lakini

Bado hajakomaa lakini nahisi huyu ndiye anafaa zaidi.Kwanza huyu ni mgombea Ubunge 2010 ingawa alichakachuliwa kati ya wagombea wote hapo juu

My take: Hii nimeitoa kuleeeeeeee..inaweza saidia na hapa pia!!
Kwa kadri ya uchambuzi wako nadhani huyo Ben Saanane ndie anayefaa zaidi. Kila mtu ana udhaifu na uzuri na hayupo ambaye yupo perfect.
 
Back
Top Bottom