Toa maoni yako juu ya wagombea hawa wa BAVICHA (Chadema) taifa

Hivi kweli, CHADEMA ni wafuasi wa Kristu tu? Jinsia je? Mbona sioni majina ya akina Othman, Mohammed, Shida, Aziza, Fatuma ukiondoa huyo Sharif aliyechomekwa/jitokeza wa ZnZ?

CDM, jaribu kuwa makini na: Ka-udini na Ka-ukanda na tazameni jinsi. In whatever you do, you ought to prove wrong all the allegations over your party.

Ni ushauri tu, japo ninajua wengi wenu mtaniporomoshea matusi.....haya leteni tu.
 
Usiwalaumu chadema, hao ndio walidiriki kuchukua fomu ama demokrasia inalazimisha watu kugombea??? Udini na ukanda tuweke pembeni, tuangalie uwezo na sifa za wale waliojitokeza. Wanazuoni wengi wanashabikia Chama kile pale Lumumba!!!
 
Kwa hoja yako hiyo nzito basi namuweka Heche pembeni na kumuingiza Silinde wa Mbeya maana jamaa wa Rorya bwana Igogo naona anafaa sana pale kwenye unaibu katibu mkuu.

Lakini kote ni amani tu na mshikamano ndani ya BAVICHA na CDM.

Hivi kweli, CHADEMA ni wafuasi wa Kristu tu? Jinsia je? Mbona sioni majina ya akina Othman, Mohammed, Shida, Aziza, Fatuma ukiondoa huyo Sharif aliyechomekwa/jitokeza wa ZnZ?

CDM, jaribu kuwa makini na: Ka-udini na Ka-ukanda na tazameni jinsi. In whatever you do, you ought to prove wrong all the allegations over your party.

Ni ushauri tu, japo ninajua wengi wenu mtaniporomoshea matusi.....haya leteni tu.
 
Hivi kweli, CHADEMA ni wafuasi wa Kristu tu? Jinsia je? Mbona sioni majina ya akina Othman, Mohammed, Shida, Aziza, Fatuma ukiondoa huyo Sharif aliyechomekwa/jitokeza wa ZnZ?

CDM, jaribu kuwa makini na: Ka-udini na Ka-ukanda na tazameni jinsi. In whatever you do, you ought to prove wrong all the allegations over your party.

Ni ushauri tu, japo ninajua wengi wenu mtaniporomoshea matusi.....haya leteni tu.

Bila matusi, je kama hao wa kanda nyingine na dini zingine hawajatangaza nia CDM wafanyeje ??
 
HABIBU MCHANGE ANAFAA KUONDOA ILE DHANA YA UDINI! Owawa pia anafaa kuwa katibu mkuu!
 
karibu sana ben, ila hatujakusikia kwenye harakati za chadema wala kwenye uchaguzi mkuu ambapo tuliwaona vijana waliojitia muhanga na wakaonyesha uwezo wao katika anga za harakati na siasa za chadema na tz kwa ujumla wake, mashaka yangu ni kwamba wanachadema watakuamini vipi? Wapo vijana kama akina John Heche wa tarime, Joshua Nassari wa arumeru mashariki, Dadi igogo wa Rorya, Mwampamba wa mbozi e.t.c. Mimi nadhani ungejiunga kwenye harakati za chama kwanza, ukafanya harakati zikaonekana na baadaye fursa zikafata ukizingatia chama kinaendelea ku-accelerate siku baada ya siku.
Ushauri wangu kwako

Ngurati,

Nashukuru sana kwa kunikaribisha.Nimejihusisha na harakati za CHADEMA kwa muda mrefu sana.Hata nilipokuwa nje ya nchi,nilijitahidi kuhakikisha natumia fursa iliyokuwepo kwa kupitia mitandao ya kijamii(ingawa haisomwi sana na watanzania wa vijijini) kuhakikisha nakieneza chama waziwazi.Hata Balozi wetu,nilimueleza wazi wazi bila kuficha kwamba ,asiige mfano wa Balozi nyingine kufungua matawi ya vyama vya siasa nje ya nchi.Sisi watanzania tunapaswa kuishi kwa umoja kupitia Jumuiya zetu na si kujigawa kwa misingi ya itikadi za vyama.Kwa mantiki hiyo tulifanikiwa kuzima harakati hadaa za CCM

Niliporudi Tanzania,muda wa Uchaguzi ulikuwa umekaribia.Nilishiriki kikamilifu kuhakikisha natoa mchango wangu wa dhati,kufanikisha ushindi wa majimbo kadhaa.Hata katika harakati za kumnadi mgombea urais Dr.Slaa,katika harakati hizo nilipata fursa ya kukutana na wanaJF kama akina Shy na wengineo pale Abla Apartment wakati wa kuzindua mtandao wa Friends Of Slaa(FoS).

Kuna wananchama wa JF tulioshirikaina nao katika harakati za majimbo ya Dar es Salaam kama Ubungo,Kawe na Segerea hadi dakika za mwisho.Naamini kabisa nilitumia fursa zote katika kukitumikia chama changu cha Demokrasia na maendeleo kwa Uaminifu

Kuhusu kutoonekana katika harakati :Mkuu wangu,Harakati za CHADEMA ni kuliondoa Taifa katika janga la uzembe,uongozi na Ufisadi.Kama ilivyo desturi kwetu sisi waafrika,ukishiriki katika kuokoa nyakati za majanga au Msiba ,hautafuti kamera ziko wapi badala yake utajikita katika kusaidia bila kujali kama mfiwa atakuona na kukushukuru na au hata kukufanyia hisani siku za usoni kwani utakuwa umesukumwa kwa dhamira ya dhati kabisa katika kutekeleza wajibu wako
 
Hongera kijana nakutakia mafanikio makubwa mbele ya safari yako ndefu kisiasa.Nikiri baada ya kupitia maelezo yako umenishawishi laiti ningekuwa mpiga kura hakika kura yangu ungeipata.

Msimamo wako kuhusu watuhumiwa wa vurugu za uchaguzi Kenya ninakubaliana nao kwa asilimia zote.Fikiri watuhumiwa kama Uhuru Kenyatta bado anaendelea na wadhifa wake wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha halafu Kibaki anahaha eti washitakiwe kenya !.Laiti Kenya ingewapokonya nyadhifa watuhumiwa wote wangenishawishi kidogo.

Tanzania baada ya Julius KN haina sera ya mambo ya nje inayoeleweka kabisa taifa limekosa heshima na mwelekeo chini ya A H Mwinyi,B Mkapa na J Kikwete tunahitaji vijana wa aina yako turejee kwenye mstari sijui fitina za BAVICHA utaziweza maana bila kujikomba kwa wakuu wa chama chako sidhani kama utapenya.
 
Wanajamvi, haya ni baadhi ya majina niliyoyasikia yakitajwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi wa Baraza la Vijana la Chadema, toa maoni yako tafadhali.

NAFASI YA MWENYEKITI.
1. John Heche (rorya)
2. Silinde David (mbozi mbeya)
3. Mwampamba (mbozi mbeya)
4. Habib Mchange ( kibaha pwani)
5. Ben Saanane ( dar/morogoro)

MAKAMU.
1. Gwakisa Baton (mbeya)
2. Kinabo (moshi)
3. Shalifa (zanzibar)
4.

NAFASI YA KATIBU MKUU.

1. Nassari Joshua (arumeru mashariki)
2. Deogratius Munishi (moshi)
3. Steven Owawa (rorya)

NAIBU KATIBU MKUU.
1. Dadi Igogo (rorya)
2. Odero Oderos (rorya)


mengine nitaweka nikiconfirm. Wadau na wanachadema toeni maoni yenu.

Mbona falsafa ya Chama chetu cha CDM inajulikana mkuu, kanda ya kaskazini kwanza halafu ndiko kwingineko mzee
 
Hivi kweli, CHADEMA ni wafuasi wa Kristu tu? Jinsia je? Mbona sioni majina ya akina Othman, Mohammed, Shida, Aziza, Fatuma ukiondoa huyo Sharif aliyechomekwa/jitokeza wa ZnZ?

CDM, jaribu kuwa makini na: Ka-udini na Ka-ukanda na tazameni jinsi. In whatever you do, you ought to prove wrong all the allegations over your party.

Ni ushauri tu, japo ninajua wengi wenu mtaniporomoshea matusi.....haya leteni tu.

Kwa ajili pia ya kujivua hilo gamba, nadhani timu ingekuwa hivi...

NAFASI YA MWENYEKITI.
1. John Heche (rorya)
2. Silinde David (mbozi mbeya)
3. Mwampamba (mbozi mbeya)
4. Habib Mchange ( kibaha pwani)
Aligombea Ubunge Kibaha na kutoa upinzani mkali sana, na kwa kuwa ni Habib hili
litasaidia kupunguza kidogo hofu za Waislamu.

5. Ben Saanane ( dar/morogoro)

MAKAMU MWENYEKITI.
1. Gwakisa Baton (mbeya)
Ni kijana mwanaharakati, mkakavu,na mwenye msimamo usioyumba, aligombea Ubunge Rungwe Magharibi lakini jina lake liliondolewa na tume kufuatia pingamizi la CCM, uchaguzi wake utasaidia pia kwenye gamba la ukanda.

2. Kinabo (moshi)
3. Shalifa (zanzibar)
4.

NAFASI YA KATIBU MKUU.
1. Nassari Joshua (arumeru mashariki)
Alionyesha umakini mkubwa kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge
Arumeru Mashariki, nashawishika ataweza kuivaa vizuri nafasi hii.

2. Deogratius Munishi (moshi)
3. Steven Owawa (rorya)

NAIBU KATIBU MKUU.
1. Dadi Igogo (rorya)
2. Odero Oderos (rorya)

Yeyote kati yao.
 
tunaomba cv na evidence za mambo waliyowahi kuyafanya ili tupime nia na mioyo yao kama kweli wako tayari kupambana mpaka kieleweke. Tukumbuke unapotaja chadema cha kwanza kuja kwenye akili ya mtanzania ni vijana. Tunatakiwa kuwa na viongozi wazuri zaidi wenye moyo mkuu kuliko hata mwenyekiti na viongozi wakuu wa chadema. Sasa ni muda wakati mugmu kwa chadema inahitaji watu wenye moyo wa kujitoa wasio na tamaa yakuweza kukihujumu chama kwa namna yoyte ile.
Tunahitaji akina mnyika, wenje,lema wengine ambao wako tayari kupambana.
Napendekeza walio na nafasi tayri kama wabunge wasigombee tunahitaji vipaji vingine pia viingie ndani.
 
1. Nassari Joshua --- namfahamu vizuri sana nilisomanae o-level, nina mashaka sana na maamuzi yake labda kama alikuja kubadilika baadae (huwa ni mkurupukaji) na swala la makundi nahisi linaweza kuibuka kwa ninavyomfahamu. msinione ninachuki binafsi, hapana, lengo ni kuiproject CD tunahitaji kiongozi type ya dr. P.W. Slaa. Nadhani joshua hapana,hapana,hapana,,

4. Habib Mchange ( kibaha pwani)--- nilipata kumuona kipindi cha uchaguzi ninahisi busara ipo pale,
 
Hongera sana Ben kwa courage uliyonayo ya kutumikia vijana wenzako kupitia chama chetu. Mimi ni mwanachama wa cdm na wewe ni mtu wa kwanza kusikia una nia ya kutuongoza kukijenga chama chetu. Nawasubiri na wengine watakaojitokeza niwasikilize kisha tutaangalia ni yupi anafaa kushika usukani wetu kwa sasa maana binafsi naamini wote tunaimani moja na tunaelekea njia moja. Kwa maana hiyo sote ni madereva. Tunaamua tu nani wa kushika usukani wakati huu na muda tutakaompa ukiisha atatapokezana. Kila la heri Ben
 
John Heche nimzaliwa wa Tarime mkoa wa mara anashahada moja toka SAUT Mwanza ni diwani wa Tarime mjini. Aligombea nafasi ya kuteuliwa na chama kugombea ubunge Tarime akashindwa. Nikijana machachari,mpiganaji, mwenye kujiamin na kujtolea kwa chama.

Wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo aliwekwa ndan mala 5 mchango wake katika ukuaji wa chama katika mkoa na kanda nzima hauna mfano nim2 asie na kinyongo akishndwa haundi kundi na akishnda habagui mshndwa kimsng anafaa
 
Tunaomba CV na evidence za mambo waliyowahi kuyafanya ili tupime nia na mioyo yao kama kweli wako tayari kupambana mpaka kieleweke.

Tukumbuke unapotaja chadema cha kwanza kuja kwenye akili ya mtanzania ni vijana. Tunatakiwa kuwa na viongozi wazuri zaidi wenye moyo mkuu kuliko hata mwenyekiti na viongozi wakuu wa chadema.

Sasa ni muda wakati mgumu kwa CHADEMA inahitaji watu wenye moyo wa kujitoa wasio na tamaa yakuweza kukihujumu chama kwa namna yoyote ile.

Tunahitaji akina mnyika, wenje,lema wengine ambao wako tayari kupambana.
Napendekeza walio na nafasi tayri kama wabunge wasigombee tunahitaji vipaji vingine pia viingie ndani.
 
Serikali ya Kenya kupitia Rais wake Mwai Kibaki imekataa kupeleka kesi za watuhumiwa wa vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo (post election violence) katika mahakama ya kimataifa ya wahalifu wa kivita (International Criminal Court –ICC)

Kijana na hiyo masters zako unatia mashaka.

Mbona watuhumiwa wameshafikishwa mahakamani the hague,?

Halafu uliona wapi ugomvi wa kidiplomasia kati ya serikali na wananchi wa nchi nyingine?

Ilichofanya serikali ni kuunga mkono serikali ya kenya kama mwanachama wa EAC.

Raila akichukua madaraka kwa wakati huo itategemea hali ya kisiasa na sera zetu zikoje,pengine hata hao CCM hawatakuwepo madarakani.

Huwezi kuomba kura BAVICHA kwa kuchimba mkwara CCM,inaoneka huna wana mkakati wazuri.

Pamoja na kujibodoa kote,umeonesha kuwa ulikua mpiga debe tu wakati wa Uchaguzi,Je tutakuamini vipi kukupa nafasi hii nzito?

Kabombe,

Kwanza kabisa nikushukuru kwa kuchangia hoja hii.Sera ya Mambo ya nje ya nchi yoyote ni kusimamia maslahi ya Taifa(National Interests) pamoja na kuongeza haiba na ushawishi wake katika medani za kimataifa.Ni lazima tuzingatie historia na misimamo yetu ya siku za nyuma kabla hatujafanya uamuzi wowote na hasa ule unaogusa maslahi ya wananchi walio wengi katka nchi fulani dhidi ya maslahi ya wachache kwa gharama ya wengi.Tanzania ilipewa heshima ya pekee kabisa kutatua mgogoro ule kwa kuwa ilisimamia upande wa wananchi wa Kenya,haikuunga mkono pande zilizokuwa zikivutana.Sasa leo hii msimamo wa Tanzania unapingana na msimamo wake wa Awali,unasema hakuna Tatizo?Lipo tatizo.Hebu soma tena vizuri hoja yangu mkuu

Kupwaya kwa sera yetu ya mambo ya nje kunatufanya kudandia hoja(Bandwagon) na kuburuzwa na wengi hata kama hawako sahihi,tunapoteza uwezo wetu wa kujenga Uwiano wa kimadaraka/nguvu ya Taifa (balancing of power) katika siasa za kimataifa.

Mkuu,suala la Odinga kushinda uchaguzi ule usilichukulie kwa Mzaha linaweza kuwa na madhara ya kidiplomasia kati yetu na Kenya.Suala la kusema Tanzania iliunga mkono harakati za serikali ya kenya kama mwanachama mwenzake wa EAC halina mantiki ya kidiplomasia kwani ndani ya serikali hiyo ya Mseto bado kuna mvutano na misimamo tofauti juu ya suala hilo.

Nchi nyingi duniani hutafakari kwa kina zinapofikia hatua kama hii tuliyofikia,ndiyo maana hata kanuni za hifadhi ya kisiasa(political Asylum) huwa zinafuatwa kwa tahadhari sana inapotokea kiongozi fulani wa nchi nyingine aliyeasi (Rebel Leader) kakaimbilia nchi fulani basi tafakari ya kina na busara ya kidiplomasia kwa maslahi ya taifa hilo kwa muda ulipo na baadae hutumika katika kumkatalia au kumkubalia hifadhi kwa kupima kwamba iwapo baadae atakuja kuwa kiongozi wa nchi hiyo hapo baadae itakuwaje?hili la kwetu linafanana na jambo hilo

Nchi Inaweza pata doa la kidiplomasia iwapo kiongozi atakayeingia madarakani kipindi kijacho atakuwa na msimamo unaoshabihiana na msimamo wa wakenya walio wengi na atakuwa na uhakika wa kupata justification hiyo kupitia sapoti ya wananchi
 
CDM, jaribu kuwa makini na: Ka-udini na Ka-ukanda na tazameni jinsi. In whatever you do, you ought to prove wrong all the allegations over your party.

Nadhani CDM wakikomalia kuogopa Udini, Ukanda nk vitu ambavyo vilikuwa propaganda kila mtu makini anafahamu hakika hawataboresha chama.

MUHIMU: Kila mgombea apimwe kwa uwezo wake!
 
john heche ndio chaguo letu, ni lazima ashinde kwa kuwa amejitolea kwa mda mrefu na anamatumain na vijana hasa wa itikadi zote ana nia ya dhati kuwakomboa vijana kitanzania.
 
Back
Top Bottom