TLP yamteua mgombea ubunge A.Mashariki Na Rehema Maigala

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

04 APRIL 2012






SEKRETARIETI ya Tanzania Labour Party (TLP) imemchagua Bw. Micah Mrindoko, kuwa mgombea ubunge wa Afrika Masharika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi , Mwenyekiti wa TLP, Bw. Agustino Mrema, alisema kuwa chama chao kisimamisha wagombea watatu na kura zao kwenye Bw. Enock Mugae (0), Bw. Mutamwega (1) na Bw. Micah Mrindoko (4).

Alisema watu hao walichaguliwa na Sekretarieti ya watu sita na ambayo iliona Bw. Mrindoko ndiye anafaa kugombea nafasi hiyo.

"Ni vizuri kumchagua mtu anayefaa hata kwa jamii ndiyo maana sekretarieti ya chama chetu imeamua kumchagua, Bw. Mrindoko kuwa mgombea ubunge wa Afrika Mashariki,"alisema, Bw. Mrema.

Aliongeza kuwa nafasi hiyo ni muhimu hivyo ni vizuri kumuomba Mungu mgombea wa chama hicho apite kwenye kinyang'anyiro hicho.

Vyama vya upinzani vinatakiwa kuwa na mbunge mmoja wa bunge hilo, huku CCM ikiwa na nafasi 8.
 
Huyu atapata kama uchaguzi ni wabunge wote kupiga kura bila kujali chama, CCM hawatampa mgombea wa CDM
 
Hilderbrand Shayo - CCM kaanguka ndani ya CCM, huyu anajipendekeza sana itabidi apande ndege aende zake UK
 
Kwahiyo sekretariati ndiyo inafanya maamuzi makubwa kiasi hiki?

Hadi mgombea uraisi Mutamwega Mugaywa hana sifa za kugombea ubunge kwa muono wa sekretariati ya chama cha TLP.

Si ajabu alipata kura chache sana, kumbe hata chama chake hakimuungi mkono.
 
Back
Top Bottom