Elections 2010 TLP yamkana Augustine Mrema

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
na Andrew Chale

CHAMA cha Tanzania Labor Party (TLP) kimesema kuwa tabia ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Agustine Mrema kumfanyia kampeni mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jakaya Kikwete ni kwa mapenzi yake binafsi na wala si ya chama chao kwani wao hawamtambui juu ya hilo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na mgombea wa nafasi ya urais wa chama hicho, Dk. Muttamwega Mgaywa, wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za urais zilizofanyika kwenye viwanja vya Bakhresa Manzense jijini Dar es Salaam kufuatia kuulizwa swali na wananchi.

Swali liliulizwa na Ezekiel Tesha ambaye alijitambulisha kuwa yeye ni mkazi wa Manzese na hana chama, ambapo alimuuliza mgombea urais huyo, "Ndugu mgombea, wewe unapingana na CCM, wakati huohuo mwenyekiti wako taifa anampigia debe mgombea urais Jakaya Kikwete wa CCM, huoni unapoteza muda?!"

Swali hilo lilionekana dhahiri kuwa gumu kwa mgombea huyo, na kumchukua dakika kadhaa kulijibu, hata hivyo alisema, "TLP si mali ya mtu binafsi, ni mali ya wapenda mageuzi ambao ni mimi na wewe wapenda demokrasia na mageuzi ya kweli na wala si mali ya Mrema swala hilo analifanya kwa mapenzi yake binafi na wala si ya chama hatulitambui hilo," alisema Mgaywa.

Mgaywa aliwataka wananchi kuichagua TLP kwani ina sera za kweli na makini kwa ajili ya kuinua taifa zikiwemo sera za kumkomboa Mtanzania wa kipato cha chini.

"Jamani, mimi nimezaliwa Manzese na ni mjasiriamali; nitahakikisha naingia Ikulu na kuwainua nyote walalahoi wenzangu wa Manzese," alisema.

Katika uzinduzi huo, wagombea na viongozi wa chama hicho waliweza kujumuika pamoja huku mwenyekiti wake Mrema akikosekana.

Chanzo: Tanzania Daima
 
Mrema ataishia kurudi ccm, lakini kimsingi yuko pale kikazi zaidi!...ni wa kumwonea huruma tu!
 
Jinga jinga hili, kazi kujipendekeza tu, si wampindue uwenyekiti tu wanagoja nini?
 
na Andrew Chale

CHAMA cha Tanzania Labor Party (TLP) kimesema kuwa tabia ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Agustine Mrema kumfanyia kampeni mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jakaya Kikwete ni kwa mapenzi yake binafsi na wala si ya chama chao kwani wao hawamtambui juu ya hilo. Kauli hiyo ilitolewa jana na mgombea wa nafasi ya urais wa chama hicho, Dk. Muttamwega Mgaywa, wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za urais zilizofanyika kwenye viwanja vya Bakhresa Manzense jijini Dar es Salaam kufuatia kuulizwa swali na wananchi.

Swali liliulizwa na Ezekiel Tesha ambaye alijitambulisha kuwa yeye ni mkazi wa Manzese na hana chama, ambapo alimuuliza mgombea urais huyo, "Ndugu mgombea, wewe unapingana na CCM, wakati huohuo mwenyekiti wako taifa anampigia debe mgombea urais Jakaya Kikwete wa CCM, huoni unapoteza muda?!"

Swali hilo lilionekana dhahiri kuwa gumu kwa mgombea huyo, na kumchukua dakika kadhaa kulijibu, hata hivyo alisema, "TLP si mali ya mtu binafsi, ni mali ya wapenda mageuzi ambao ni mimi na wewe wapenda demokrasia na mageuzi ya kweli na wala si mali ya Mrema swala hilo analifanya kwa mapenzi yake binafi na wala si ya chama hatulitambui hilo," alisema Mgaywa.

Mgaywa aliwataka wananchi kuichagua TLP kwani ina sera za kweli na makini kwa ajili ya kuinua taifa zikiwemo sera za kumkomboa Mtanzania wa kipato cha chini.

"Jamani, mimi nimezaliwa Manzese na ni mjasiriamali; nitahakikisha naingia Ikulu na kuwainua nyote walalahoi wenzangu wa Manzese," alisema.

Katika uzinduzi huo, wagombea na viongozi wa chama hicho waliweza kujumuika pamoja huku mwenyekiti wake Mrema akikosekana.

Chanzo: Tanzania Daima
TLP kazi iliyopo mbele yenu si kuing'oa CCM bali ni kumng'oa MREMA kumbukeni MARANDO, LAMWAI, NSWANZIGWAKO, JOSEPH SELASINI
, MBATIA na wenzao wengi walishindwa kumng'oa NCCR mageuzi hadi akakimbia mwenyewe na alipofika TLP mambo yaliyompata muanzilishi wake LEO LEIKAMWA nadhani nyinyi wote mashahidi, kawasambaratisha hadi juzi alitaka kumfukuza MUTUNGIREI
aliyegombea nae uenyekiti. Hivyo CCM kwenu ni maji marefu maana imejiimarisha ndani ya chama chenu TLP. Kwa kifupi TLP ni TAWI la CCM hivyo jiondoeni toka CCM kwa kumng,oa MREMA na vibaraka wake harafu karibuni kwenye mapambano ya ukombozi wa watanzania. Kama wenzenu CHADEMA na CUF
 
Mmmhhh mimi najiuliza hivi TLP ni mali ya Mrema nini? Yaani yawezekana vipi Mrema anampigia kampeini Kiwete wakati anaye mgombea katika chama chake na wote wamemnyamazia kimya?
Weee Mtungilei mbona unapoteza muda wako kwenye chama hewa? soon chama hiki hakitakuwapo maana mwenye chama ataki merge na sisi m.
Yatatokea yale yale ya sisi J.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom