Tlp. Cuf, nccr & wengine wajifuta kwa msajili kama vyama vya siasa

JUST

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
552
234
HOJA HII INATOKANA NA KAULI ZA VIONGOZI WA VYAMA HUSIKA

Katika hali ya kawaida chama cha upinzani nia yake kubwa ni kuonyesha mapungufu ya chama kinachotawala kwa jamii ili waweze kuwaondoa na wao kushika dola. Kwa hapa Tanzania ni kiroja cha aina yake kwa kuona vyama vya upinzani ukiacha CDM vinaondoka kwenye nia hiyo kuu na kuwa wasemaji na maagenti wa chama tawala.

kwa misingi hiyo msajili wa vyama vya siasa nchini anatakiwa kuvitoa kwenye orodha ya vyama vya siasa na kuvijumuisha kama washirika wa chama tawala na avibatize jina la party of few unit "PFU" kwa muungano wao wa kisiri waliounda pasipo mamlaka ya umma unaovifanya viwepo.
 
Vyama zaidi ya 11 kwenye daftari la msajili vipo hai lakini kiuhalisia vimekufa, vile vinavyo jitutumua navyo vimeamua kujipambanua kuwa ni wafuasi wa CCM kivitendo lakini kinadharia ni wapinzani, hapa CDM sijawaunganisha na vyama hivyo.
Lakini ktk hali halisi ya Tanzania vyama hivyo 11 haviwezi kufutwa na msajili maana kwa siasa za Tanzania vyama hivyo vinapiga kazi bado, kumbuka JK aliwakemea CDM kwa kufanya mikutano na maandamano eti kwa kuwa uchaguzi umeshakwisha sasa wasubiri mwingine na Msajili wa vyama Bw. Tendwa nae akaunga mkono, hivyo kibongo bongo vyama hivyo vipo hai maana kukaa kimya kwake ni mtaji wa CCM 2015 na ni salama ya Tendwa kuendelea kuwa Msajili, wakianza siasa za kiuana harakati kama CDM ili kuwahamasisha watanzania kukomboa taifa lao wataitwa wachochezi na wanatakakufanya uhaini.Yaani wanatakiwa waibuke kipindi cha karibu na uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015, Vyama vya kisiasa bongo vinatakiwa kujiendesha kama HOMA ZA VIPINDI yaani vipige kazi uchaguzi ukikaribia ukiisha vipumzike kuiachia CCM ifanye uchakachuaji hadi uchaguzi mwingine.

Hivyo CUF, NCCR, UDP na TLP hivyo ni vyama hai lakini ni ma agent wa CCM wakiendekeza siasa za MTUMIKIE KAFIRI UPATE MRADI WAKO na BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA
 
Ndugu siasa za upinzani nchi hii ni ngumu sana. Kuchagua kuwa mpinzani ni kuchagua njia nyembamba iliyo ngumu kisiasa! Hii inatokana na sababu nyingi lakini kubwa zaidi ni elimu ndogo ya uraia kwa watu na kutokuwa na uhakika au tuseme hofu ya kwamba je wapinzani wakishika dola itakuwaje? Kwa maneno mengine ni kusema heri ya shetani umjuaye kuliko malaika usiyemjua. Ktk hali hii vyama pinzani vinaweza vikawa hodari wa kuibua madudu na mapungufu ya chama tawala lakini linapokuja kwenda kwa wananchi kuombaa ridhaa huko kunakatisha tamaa.

Sasa kutokana na kwamba waongoza vya pinzani ni binadamu wenye mahitaji kama wengine mathalan kufanikiwa ktk nyanya zote za maisha kielimu, kiuchumi, kijamii n.k wanajikuta wanakata tamaa kuendelea kuwatetea watu 'wasiohitaji' kutetewa. Na kwa kuwa na wao wana njaa tena kubwa tu wanajikuta njia panda na hatimae huacha kuwa watetezi wa wanyonge! Badala yake inawalazimu watekeleze kwa matendo msemo usemao if u can't fight them join them na ndicho cuf, tlp, nccr wanachofanya!
Nawasilisha
 
mimi nachojua tz kuna vyama viwili tu cdm na ccm basi ila ccm ina branch nyingi kama ccm b ccm c ccm d ni hayo 2
 
Back
Top Bottom