TISS (Usalama Wa Taifa): The best National Intelligence Ever!

Mkuu, information za CIA, Mossad na wengineo, ambao unafikiri zipo nje nje, Ni zile tu ambazo mashirika hayo yanataka wewe ufahamu kwa manufaa ya mashirika hayo. Ni habari ambazo zinatolewa na kudhibitiwa na vitengo vya "disinformation and misinformation". Kwa hiyo hapo ni kwamba TISS hawajafanikiwa kwenye hivyo vitengo kama ambavyo wanashindwa hata kufanya economic and technological espionage. Hamna haja ya kuwasifia.

Basi hata TISS watoe information ambazo wanataka tuzifahamu kwa manufaa yao!!
 
Ni ajabu wakati hiyo siyo kazi yao kisheria....katika sheria ya TISS No. 15 ya 1996 Part II, section 5, subsection 2 kinasema; nanukuu:

It shall not be a function of the Service-
(a) to enforce measures for security; or(b) to institute surveillance of any person or category of persons by
reason only of his or their involvement in lawful protest, or dissent
in respect of any matter affecting the Constitution, the laws or
the Government of Tanzania.

Sasa siju ni lugha au?!?!? Hiyo ndiyo kazi yao kubwa sasa!!!

Mkuu unaweza ukatusaidia hizo sheria zilizoanzisha TISS ili zitusaidie sisi walipa kodi kujua mustakabali wa chombo chetu cha Usalama..
 
TISS kazi yao ni kuweka siri ya jinsi nchi inavyotafunwa na wachache.....na pia kazi yao kubwa siku hizi ni kutafuta na kuwaharass wote wanaoisema vibaya serikali ya muheshimiwa au wanaomsema vibaya muheshimiwa na pia wanaoingilia anga za muheshimiwa.

Mataifa yaliondelea, vyombo vyao kama TISS wala haviko tena kwenye zama za usiri ebu cheki websites zao hapa (hadi kuna sections za ajira!!!)

https://www.cia.gov/
http://www.fsb.ru/ (hii ni ya Russia; KGB ilikua dissolved mwaka 1994 au 1995)
https://www.sis.gov.uk/ (hii ni ya UK; yaani hadi wameweka picha ya bosi wao!!!)
www.mossad.gov.il (hii ni ya Israel)

Hapa kwetu TISS ni kizungumkuti!! Kazi zenyewe za kupeana...baba, watoto, wajukuu, wajomba.................

aise hiyo site ya Urusi haina mahala pa kubadilishia lugha kwenga kiingereza?nilitaka niwasome lakini nilipoifungua nikakutana na 'kilugha chao' tu
 
Unadhani waliwezaje kumkamata/kumuua Usama?

Ukiongea na "conspiracy theorists" wanaweza kubishana na wewe kuhusu hilo:

wapo wanaodai Osama alikufa zamani sana, na sio mwezi ulipita.

na wengine bado wanahoji kwa nini alizikwa harakaharaka hivyo, na alizikwa baharini.....yaani hakuna mwili wala kaburi......kuna picha tu (si unajua hata magazeti ya udaku yanaweza kukutoa wewe umekaa na mtoto mnasubiri pantoni kwenda kigamboni)
 
usalama gani wa taifa huu, watu wanatua na madege yao ya kijeshi na kupora maliasili zetu na kuondoka nazo, wamekalia usiri hata namba zao za simu hazijulikani, bila umma utafanya kazi,
wanafanya kazi kizamani na kishamba sana.
 
Hivi kuna usalama wa taifa tanzania au kiini macho tu?
au kazi yao kumlinda JK pekee huku wakiacha makaburu na wazungu wengine wakisafirisha madini yetu usiku wa manane,
wakiacha wanyama wetu wanaibwa usiku.kazi yao nn sasa au tuseme polisi ndio kila kitu?
Nadhani hii sekta ingefungwa wanatumia garama na kodi zetu bure sioni cha maana kwao.
Tujiulize ile kashfa ya kutumika kuchakachua kura wamejisafisha??Mi nlidhani kazi yao ni kulinda sii usalama wa siasa tu pia kulinda uchumi wetu na vyanzo vyake kwa ujumla,kuzuia mikataba feki nk....KAMA YUPO HAPA AJITOKEZE AKANUSHE HAYA.

Ilikwisha geuzwa zamani, siku hizi ni "Usalama wa Serikali ya CCM"
 
TISS = Taasisi Iliyo Siri Sana
ina usiri,lakin mbona wanapigwa bao na mafisadi?moja ya kazi yao ni kuhakikisha ubadhilifu hakuna.....lakini wao wamelala........nadhan kazi yao kuuuuubwa ni kumlinda jk
 
Mkuu, information za CIA, Mossad na wengineo, ambao unafikiri zipo nje nje, Ni zile tu ambazo mashirika hayo yanataka wewe ufahamu kwa manufaa ya mashirika hayo. Ni habari ambazo zinatolewa na kudhibitiwa na vitengo vya "disinformation and misinformation". Kwa hiyo hapo ni kwamba TISS hawajafanikiwa kwenye hivyo vitengo kama ambavyo wanashindwa hata kufanya economic and technological espionage. Hamna haja ya kuwasifia.

Sasa wewe unajuaje kuwa hawafanyi kazi kama hata hujui ni akina nani, na kazi zao ni zipi, na wamefanya nini mpaka sasa.....yaani hawajulikani.

kama ungekuwa unafahamu kitu chochote (zaidi ya stori zetu za kitaa) then ungeweza kusema kama wameshindwa kazi ama vipi.
 
Jamani Usalama Wa Taifa sio Polisi na wala sio Mahakama...kuna mtu kapost document huko juu ambayo inaelezea kazi za TISS, ingekuwa vyema muisome.

Kama wanyama wameibiwa, ni kazi ya polisi kukamata wezi. Kama watu wanakula rushwa ni kazi ya PCCB kuwakamata na kuwapeleka mahakamani.

Ila kama kuna watu wamejaribu kupindua nchi au kuanzisha vita wakafanikiwa, then hilo ni swala ka TISS....au kama kuna watu wamewahi kumKennedy rais wa Tanzania then hiyo ni issue ya TISS
 
Moja ya kazi zao ni usalama wa mali za taifa na raia. Kuibiwa kwa gold na wanyama ni part ya kazi yao. Kazi yao si kukamata ila kuwajulisha polisi na Takukuru nini kinaendelea. Hata FBI na CIA ndivyo wanavyofanya kazi zao
 
Nimeiona hiyo document...ngoja niipitie!

Ila ni kweli tulitakiwa tufahamishwe bajeti yao inakuwaje? Je ipo ndani ya wizara ya mambo ya ndani, au nje? au inajitegemea?
 
Kumekucha !

TISS ni taasisi nyeti ya serikali na ina usiri mkubwa sana. Huwezi jua , huwezi sikia mtu akibwabwaja hovyo , si kwa rafiki yake wa karibu , si kwa mwenzi wake , si kwa ndugu wala jamaa zake.

Wengi huwa tunahisi tu " yule jamaa yupo TISS , huenda yupo TISS ". Ni ngumu sana mtu kukueleza wazi kwamba yupo kitengo fulani , ngumu. Watu feki ndo hujitangaza , lakini si wale wenyewe.

SWALI

Usiri mkubwa walionao ni kwasababu wana mafunzo mahiri au wanaogopa kubwabwaja wakijua adhabu yake iliyopo ?

Kiukweli mm sijawahi muona mtu aliye TISS ninayemfahamu.

Wanatoka humuhumu TZ au wameletwa toka nchi za jirani ? Maana sura zote huwa mpya machoni mwangu.

Nawasilisha.
 
Haaaaaa, mkuu umenifurahisha Sana unaposema kila TISS humjui na sura zao Ni ngeni kwako, vyote hivyo jawabu katika maswali yako....miiko ya kazi na adhabu ndizo chanzo Cha usiri,...

"Kumbuka hata wao wenyewe hawajuani isipokuwa pale inapowabidi"
 
Wale wa kutoka wilaya moja mnajuana tu.... ni kama walimu wa Ilala ni ngumu kumjua wa Kinondoni.. TATIZO TUNAKAZA UBONGO SANA...
 
kwani kazi zao ni zipi mpaka utake kuwajua!?

ukiambiwa mtu ni afisa usalama,usikariri wapo wanaofahamika kabisa na kujitambulisha ni lazima,wapo ambao kujitambulisha sio lazima,kuna ambao ni marufuku kujulikana,ukijulikana ni hatari na hasara kubwa sana.

kwahiyo kuwajua au kutowajua sio jambo la ajabu.
 
Back
Top Bottom