Tishio la Wana CCM kukimbilia CHADEMA limeugeuza moyo wa Farao

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
1.jpg

Tangu kuibuka kwa wimbi la mkaguzi wa mahesabu ya serikali kuanika hadharani uvujaji wa pesa za umma serikalini, hali iliyosababisha wabunge kuivimbishia mishipa serikali wakiongozwa na wabunge wa upinzani kinara akiwa Zito kabwe, ambaye amezua mtafaruku mkubwa ndani ya CCM kwa kuanzisha mchakacho wa kukusanya sahihi za wabunge wasiopungua sabini ikiwa ni asilimia 20 ya wabunge kujenga hoja ya kupiga kura ya siri ya kutokuwa na imani na Waziri mkuu, kwa lengo la kushinikiza mabadiliko ya baraza la mawaziri kumechafuka vibaya ndani ya CCM.

Pamoja na ajenda ya kujadili na kuridhia mabadiliko ya baraza la mawaziri, CCM imeonja joto la jiwe kwa wimbi kubwa ambalo limetikisa si umoja wa vijana tu, ila hata vikongwe ambao walikuwa damudamu na CCM kuanza kuikimbia Jembe na nyumba na kujiunga na Chadema.

Ajenda kuu ya Kamati Kuu ya CCM ilikuwa kujadili hali ya kukimbiwa na wanachama ambayo imekuwa ni ajenda ya siri, na hii ya kuridhia hoja ya wabunge kushinikiza mabadiliko ya baraza la mawasili ni kuridhia kwa ajili ya kujinasua na mtego wa kukimbiwa na wanachama wake.
 
Ni upepo tu....utapita.... acha nende mazishini nikirudi mambo yatakuwa yametulia.....weweeeee...unachezea pipoz power??... Na bado ngoja arudishe vibonde wake kwa ajili ya uswahiba aone kama bunge la budgeti hakijawaka...Mwalimu aliasa jamani Ikulu chungu..
 
Umenivunja mbavu zangu. Siasa si mchezo wa kuigiza, yataka moyo.

Angalia vizuri picha hiyo unaweza kusoma kitu kwenye nyuso za wajumbe wa kamati kuu. People's powe si lele mama.
 
hawa tunawalea vibay, ikulu sio sehemu ya kufanyia shughuri za chama, hii inaonesha wasivyokuwa serious
 
Chadema inabidi iwe macho sana na hawa hama hama wa ccm wanao toka ccm na kuingia chadema mim nahisi hawana nia njema kabisa.

Kiukweli hawa hama hama wanakuja kukiharibu chadema.

Kwanza inaonyesha wazi wanahamia chadema kwaajiri ya kutaka kugombea uongozi 2015.
Na hawa wakipewa uongozi ndani ya chadema wataleta madudu yao na uchafu wan walio toka nao ccm.
 
Ni upepo unaovuma kwa muda, utatulia wenyewe
 
Back
Top Bottom