TIOT yatajwa kinara wa kukwepa kod

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
TIOT yatajwa kinara wa kukwepa kodi

2009-04-30 14:39:27
Na Hamisi Kibari
Bunge limeambiwa kwamba kuna udanganyifu mkubwa katika ulipaji wa kodi za mafuta kwa baadhi ya makampuni, huku kampuni la TIOT Limited likitajwa kuwa kinara wa kukwepa.

Aidha, serikali imeombwa kulichunguza kampuni hilo kupitia taasisi kama Takukuru ili kujua usugu wake wa kukwepa kodi unatokana na nini.

Akiwasilisha bungeni taarifa ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa mwaka 2008/2009, mwenyeketi wa kamati hiyo, John Cheyo, alisema kwamba kamati yake ilielezwa na wahusika kwamba udanganyifu uliofanywa na makampuni ya mafuta ulikuwa na thamani ya sh. bilioni 38.4
``Kati ya hizo fedha, hoja yenye thamani ya sh. 35.5, sawa na asilimia 92.5 zilihusu kampuni moja tu ya TIOT,`` alisema Cheyo.

Alisema kamati yake ilielezwa kwamba kampuni hiyo ya TIOT ni sugu kwa ukwepaji wa kodi za mafuta.

``Aidha Kamati inaipongeza TRA kwa kuweza kukusanya sh. bilioni 29.8 ya hoja zote na kubakiwa na bakaa ya sh. bilioni 8.4 ambapo sh. Bilioni 5.6 pekee zinahusu kampuni ya TIOT,`` alisema Cheyo.

Alisema, Kamati yake ilielezwa kwamba njia inayotumiwa na kampuni hiyo ili kuzuia TRA kupata mapato yake kukimbilia mahakamani.``

``Kamati inapendekeza kwa serikali kufanya uchunguzi wa kina kwa kutumia vyombo vya serikali kama vile Takukuru ili kubaini msingi na ujeuri wa kampuni hii,`` alisema Cheyo.

Akihimitisha hoja yake baada ya Bunge kujadili ripoti yake, Cheyo aliomba ikiwezekana wakati kamati yake itakapokuwa ikiwahoji maofisa wa serikali, basi mambo yawe yanafanyika mbele ya kamera, ili baadaye yarushwe hewani na wananchi kusikia.

Alisema hivyo ndivyo inafanyika hata katika baadhi ya mabunge mengi ikiwemo Uganda.

SOURCE: NIPASHE
 
Waandishi wa bongo bwana, mtu anaandika article nzima iliyokuwa centred around TIOT na ulipaji kodi bila kuelezea TIOT ni nini, bila hata ya kutoa kirefu cha TIOT!

Wengine tunavyojua TIOT ni "The Input Output Table".

Halafu kampuni ni "kampuni ya ..." wala si "kampuni la..."

Wanawatoa wapi hawa watu wasiojua hata Kiswahili na kuwafanya waandishi?
 
Tanganyika Investment Oil & Transport Company Limited na mmoja wa wamiliki wake ni Mheshimiwa Mwakilishi wa nchi ya Comoro hapa Tanzania Bwana Islam Saleh.
 
Tanganyika Investment Oil & Transport Company Limited na mmoja wa wamiliki wake ni Mheshimiwa Mwakilishi wa nchi ya Comoro hapa Tanzania Bwana Islam Saleh.

Ahsante,

That wasn't so hard, I mean there are no Cyrillic characters involved or anything like that.

Wamrudishe shule huyu muandishi.
 
Tanganyika Investment Oil & Transport Company Limited na mmoja wa wamiliki wake ni Mheshimiwa Mwakilishi wa nchi ya Comoro hapa Tanzania Bwana Islam Saleh.

Merrey Balhabou yumo humo na pia ana kimeo cha Barclays Bank
 
Back
Top Bottom