Tundu Lissu aibuka kidedea

PrN-kazi

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
2,900
444
Tundu Lissu aibuka kidedea katika kesi iliyokua inamkabiri juu ya kuwekewa pingamizi ya uhalali wake kuwepo mjengoni kama Mbunge kutokana na ushindi alioupata kwenye uchaguzi wa Oktoba 31, 2010.

Mwenye habari kamili juu ya hilo atujuze kwa mapana zaidi..
 
wengine ndio kwanza tunasikia toka kwako, mengi tunangoja kutoka huko huko kwako
 
Tindu Lissu aibuka kidedea katika kesi iliyokua inamkabiri juu ya kuwekewa pingamizi ya uhalali wake kuwepo mjengoni kama Mbunge kutokana na ushindi alioupata kwenye uchaguzi wa Novemba 31, 2010.

Mwenye habari kamili juu ya hilo atujuze kwa mapana zaidi..

acha kukurupuka, fanya utafiti kabla ya kupost chochote humu badala ya kuomba "habari zaidi!" Hakuna uchaguzi uliofanyika Novemba "31," 2010 kwa kuwa tarehe hiyo haipo!
 
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma, jana ilifutilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (Chadema) na kusema kuwa kesi hiyo ilifunguliwa kimakosa hivyo haiwezi kuendelea kusikilizwa.

Jaji Sivangilwa Mwangesi,alisema kuwa kesi hiyo ilikuwa na kasoro nyingi kutokana na vifungu vya kisheria na akasema haiwezi kuendelea kusikilizwa mahakamani hapo.Kesi hiyo ilifunguliwa na wanachama wawili wa CCM, Shaban Itambu na Pascal Hallu ambao wamewafungulia kesi ya kupinga matokeo Mbunge wa Singida Mashariki, Tindu Lissu, msimamizi wa uchaguzi na mwanasheria wa serikali.

Hata hivyo wakati kesi hiyo ikifutwa jana, Lissu mwenyewe hakuwepo mahakamani baada ya kuelezwa kuwa aliharibikiwa na gari akiwa njiani kuja Dodoma ambapo aliwakilishwa na ndugu yake Samson Mkotya ambaye alisema kuwa mbunge huyo alikuwa Morogoro baada ya juzi kuharibikiwa na gari lake.

Kufutwa kwa kesi hiyo ni ushindi kwa Tundu Lissu ambaye tangu mwanzo wa kesi hiyo alionekana kujiamini zaidi na kusema kuwa kesi hiyo ingeishia katika hatua za mwanzo bila ya kufika mbali.

"Mimi nasema kuwa,kesi hii naisimamia mwenyewe na ninatambua kuwa haiwezi kufika mahali popote kwa kuwa imejaa makosa mengi ya kisheria ambayo kimsingi kama Jaji ataamua kufuata haki hakuna kesi hapa," alisema Lissu siku alipowasilisha ombi la kufutwa kwa kesi hiyo.

Mbunge huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria aliwasilisha kumbukumbu za hukumu za kesi nyingi ambazo zilifunguliwa kwa mtindo huo ambazo alisema kuwa yeye (Lissu) alizisimamia lakini alishindwa.

Baadhi ya kesi alizonukuu Lissu ni pamoja na kesi ya John Mnyika na Charles Keenja, Joyce Chitende na Zainabu Gama, John Jomba na Christopher Ole-Sendeka ambazo alisema kuwa zote zilifunguliwa kwa mtindo huo lakini zilishindwa kuendelea.

Jana Jaji Silivangira alisema licha ya Kifungu cha 111 (b) ambacho Lissu alisema kuwa kimekosewa kutokuwa na mapungufu ya moja kwa moja, lakini kwa kutumia sheria hiyo katika kifungu 112 (a),(b) bado ufunguaji wa kesi hiyo ulionekana kuwa na makosa.

Moja ya vitu ambayo Lissu alitaka viwekwe ni pamoja na wadai hao kulipa gharama za kesi ya uchaguzi ambazo walishindwa kuzilipa,kingine ni pamoja na kufutilia mbali ombi la wadai walilotaka kusamehewa kulipa gharama hizo akidai kuwa kama hawana fedha wasingeweza kuweka mawakili.

Kwa upande wao Mawakili waliokuwa wakisimamia kesi hiyo kwa upande wa wadai kampuni ya Uwakili la Wasonga walishindwa kuzungumza chochote kwani mara baada ya kumalizika kwa kesi hiyo waliondoka mahakamani hapo.

Source: Mwananchi
 
Tetesi na kukurupuka tofauti yake ni nini?
 
Inamaana hawakuilipa mahakama ada ya kufungulia kesi? Sasa msajiri aliisajiri vipi? Mambo haya.
 
Ingekuwa ni CCM wameshinda hapo duh kila tusi lingeelekezwa kwao, siasa jamani si mchezo.
 
Crashwise mimi si wa hivyo ndugu, kimeshapitishwa na mahakama hakina siasa. Hakijaniuma kwa kuwa ndiyo justice na justice haina siasa.
 
acha kukurupuka, fanya utafiti kabla ya kupost chochote humu badala ya kuomba "habari zaidi!" Hakuna uchaguzi uliofanyika Novemba "31," 2010 kwa kuwa tarehe hiyo haipo!

unaiaibisha ID yako. We ndo unakurupuka haswa. Ebu soma tena ndo umuelewe mwenzio.
 
Duh mawakili wetu hovyo sana kama walijua wateja wao hawana vijisenti vya kugharamia kesi kwa nini walienda kuisumbua mahakama wkt kuna watu wamejaa magerezani wakisubiri majaji hao wawasikilizie kesi zao
 
Aliyeweka thread hajakurupuka ni ulimi kuteleza tu akasema novemba badala ya octoba. Pili unaposema afanye chunguzi kabla kuandika unakosea, yeye alikua hana uhakika ndio maana akaandika tetesi.

Tusiwe tuna challenge kila kitu ili tuonekane sisi tunajua sana. Tetesi haiitaji kufanyiwa uchunguzi kiasi unachotaka wewe vinginevyo neno tetesi halina maana. Hongera lissu.
 
Back
Top Bottom