Timu ya Rais yatakiwa kuwataja mafisadi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Posted Date::3/14/2008
Timu ya Rais yatakiwa kuwataja mafisadi

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

MJADALA wa kutaka kutajwa majina ya watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu (BoT), umezidi kushika kasi ambapo Timu ya Rais ya kusimamia mchakato huo imetakiwa kuwataja ili kuwapa wananchi haki ya kuwafahamu.

Kutotajwa majina ya watuhumiwa hao ni moja ya mjadala mzito unaoitikisa nchi kwa sasa, kutokana na mtazamo wa wengi kwamba, waliochota mabilioni hayo ya umma, ni vigogo ndani na nje ya serikali.

Akizungumza na gazeti hili jana, Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Eric Ng'mario, alisema wananchi wengi wanataka kujua majina ya watuhumiwa hao na pia ni haki yao kuwajua.

Hata hivyo, Ng'mario aliweka bayana kwamba ni jukumu la timu hiyo kuangalia umuhimu wa kutaja watu hao na upande mwingine athari zake kiupelelezi.

"Wananchi wana haki ya kujua majina ya watuhumiwa, ni suala la tume kuangalia na kuweka katika mizania, kuona umuhimu na athari za kuwataja watu hao ," alifafanua.

Alisema hakuna njia ya mkato ya kutowataja watu hao, kwani hata kama si sasa, lakini ni lazima watajwe mwisho wa siku tume ikimaliza kazi.

Mwanasheria huyo aliongeza pia kwamba, hakuna njia ya mkato lazima watu hao mwisho wa siku wafikishwe mahakamani.

Kwa msisitizo, Ng'mario alisema suala la kurejesha fedha ni hatua moja muhimu na ya kushitakiwa ni nyingine hivyo Watanzania watataka kuona watuhumiwa hao wanashitakiwa.

Alisema sheria za Tanzania si kama Marakeni ambako mtu anaweza kukubaliana kurejesha fedha, lakini asishtakiwe, hivyo ni matumani ya Watanzania kuona watuhumiwa wakirudisha fedha na kushitakiwa.

"Marekani sawa, mtu anaweza kurudisha fedha halafu akafanya mazungumzo asishitakiwe, sisi hapana lazima tuone watuhumiwa wote wanashitakiwa," alisisitiza Ng'mario.

Kuhusu mchakato, alisema ni vema watu wakawa na subira kwani miezi sita si mingi ambayo mwisho wa kazi ya timu hiyo itapaswa kuwa imechukua hatua zote.

"Nafikiri ni suala la wakati tu, tunaweza kuichia timu ifanye kazi yake katika kipindi chote cha miezi sita, mwisho wa siku itatoa majibu,"alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Benno Ndulu, leo anatarajiwa kufanya mkutano na wandishi wa habari.

Hata hivyo, hadi jana jioni ajenda za mkutano huo hazikuwa zimefahamika vema.

Kwa sasa BoT inaangaliwa kama taasisi ambayo inahitaji kusafishwa, kutokana na sakata la tuhuma za ufisadi wa zaidi ya Sh133 bilioni katika EPA.

Tofauti na hoja iliyotolewa na wadau mbalimbali wakiwamo wanaharakati, kamati hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Johnson Mwanyika, imetoa taarifa yake ya tatu ambayo imeshindwa kujibu hoja ya vipi watuhumiwa hawakamatwi.

Hata hivyo, kinyume na agizo hilo na sheria za nchi, watuhumiwa hao katika makampuni 22 yaliyochota fedha hizo, wamekuwa wakirejesha fedha bila kukamatwa huku kukiwa na usiri wa kutaja majina ya makampuni yaliyorejesha fedha na watuhumiwa.

Juzi timu hiyo chini ya Mwanyika ilivyozungumza na wahariri, pia ilisita kutaja majina ya watuhumiwa na makampuni kwa madai ya kuogopa kuvuruga upelelezi.

Ufisadi katika EPA ulibainika baada ya ukaguzi wa kimataifa wa Kampuni ya Ernst&Young, ambao awali uliibuliwa na Deloitte&Touche, ulimfanya Rais Jakaya Kikwete, kutengua uteuzi wa gavana Daud Ballali na kuunda timu hiyo chini ya Mwanyika.
 
Jf ukiingia unakuta thread sio chini ya 8 zinazungumzia, kwa njia moja ama nyingine, UFISADI. Kwakweli sijambo zuri kama jamii ya Kitanzania imetawalwa na tatizo hili. Nia yangu nikujaribu kutoa fikira zangu, kuuliza maswali machache na kujaribu kupata mchango wa wanaJF.

Leo nimesoma kuhusu Freeman Mbowe kuwa ni fisadi kwasababu hajalipa mkopo.Sasa kama mtu alikopa mil.15, alafuleo anadaiwa 1.2Billion na bado riba inaendelea kujilimbikizia labda sio fisadi, labda anachangia taifa.hahaha. Nadhani tumezidi,it makes no sense. Wasomaji wengi mpaka hapa watadhania nia yangu ni kumtetea Mbowe, basi ngoja niweke hilo sawa. Nisingependa kuingiza sera zangu zaki siasa katika hoja hii lakini,suffice it to say, I don't approve of Mbowe's character at all, hafai kabisa kuwa kiongozi.Lakini tuache hayo.Mfano wangu lengo lake nikusema kwamba kila mtu ni fisadi kisa tajiri, ama anafanya kazi serikalini?

Mtu yeyote mwenye familia, nadhini wengi wenumlio katika nafasi hiyo mtakubaliana na mimi, anawajibu wakulisha, kuvisha,kuilinda, kuielimisha nakuijali familia hiyo. Mtu anapokuwa mfanyakazi serikalini, achana na political leaders or high civil service,mishahara duni, matatizo kede kede na bei za bidhaa zote zina panda kutokana na cost push inflation (price of oil morre than $100 a barrel) utamwambia vipi asile rushwa? Ndio maana nasemaga wangiwetu humu wapigakele tu, wangapi kati yetu atakataa milioni 200 kuisadia kampuni yakichina ipate tenda ya kujenga barabara,daraja ama chuo? Hela ambayo itasaidia watoto wako wasome vizuri, uweze kujiuguza ukiumwa, uwajengee nyumba watoto wako...wangapi kweli watakataa humu, wakati wengine wakipata rumours tu wanaenda kublackmale wahusika..hahaha sitaki hata jibu la hilo swali hapo juu, maana Petro nae alisema hato mkana Bwana mara tatu.

Hakuna cha CCM, upinzani walanini! Tatizo linaloleta ufisadi ni umaskini wakiroho, udhaifu wakizalendo... Jambo lakushangaza and rather ironic maana wote wanaotawala tanzania sasaivi walizaliwa katika kipindi cha Patriotic social ideology yakina mwalimu,Mao,Castro etc... Sasa watot wa 1990s wakija madarakani sijui itakuwaje! Lakini mimi nadhani labda uzalendo upeweumuhimu zaidi, watu wapende nchi zaidi kuliko ilivyo sasa ambapo kilamtu anajiangalia mwenyewe na sio Tanzania. Mashuleni, wanafunzi wafundishwe kuwa wazalendo na athari za rushwa. Ili generation ijayo iwedominated na watu wasiona mawazo ya hujma.

Mtu anaewalaumu viongozi ambao tunawachagua baada yakupewa pilau na khanga, au baiskeli ni mnafiki. This is how Tanzanian leaders are elected, kwa kuhonga. Kwahiyo siasa kwetu ni biashara. CCM juzi Kiteto wameona Chadema wanapata wafuasi kwasababu ya helikopta, nawao wakakodi moja... yani nivituko.. Inamaana sera za Chadema na CCM nikuwateka wanakijiji na maajabu ambayo hawajazoea kuona katika maisha yao??? This is stupidity, na hivi ndio vyama ambavyo vinaongoza kwa wafuasi Tanzania. Je, kweli tunademokrasia?? CCM wameiba BOT, kufund campaign, its a fact. Lakini hakuna reprocution ama concequences zozote za maouvu yao... sasa kwanini waache?? hata mimi ningeendelea. kwanini mtu afanye kazi kama anaweza akaingia benki akaiba na asifanywe kitu.haha. Watanzania inabidi tuamke. Ok, admittedly kuna kaji muamko fulani,watu wanaongea lakini haitoshi. Hata humu JF.. oh EPA,Richmond, TICTS,Deep Green,tangold,kiwira,IPTL, Mahalu.. which other one, RADAR,ANBEN, nini tena! is that it? Dili hizi ziko nyingi mpaka inatisha lakini hakuma anaesema kitu... Kila Kiongozi anajiangalia yeye! Ni ideological problem, sio watu wachafu tu, maana atawale wasio walafi bado wanakula vyakutosha. Do you know how much vyakutosha is?? 1 billion, 500million, 200 million.. safi. Nenda kwa wakuu wapolisi park nnje muangalie jinsi wahindi wanavyo kuja na bahasha. Utadhani tiba anatokea Maharashtra na sio Kagera.LMAO. Ingekuwa shuleni, mwalimu anafundisha alafu wanafunzi 100% wanafeli... tatizo sio wanafunzi, at least sio wote.. kuna FUNDAMENTAL FLAW... Jee wenzangu mnadhania nini? And please dont reply with some bulshit like CCM ama JK ama upinzani mbovu. Let the record state: Huwezi kuwa Rais wa Tanzania katika miaka ya leo bila kuwa mchafu, ukiwa msafi, wachafu watakupiku, wataingia. Kwahiyo tuangalie tutabadilishaje mawazo yetu watanzania, tuache tabia zinazo tuhujumu kama jamii??

NEW TANZANIA NDIO HII
 
NEW TANZANIA NDIO HII

Wewe uliye katika old Tanzania huitakii mema nchi yetu maana old Tanzania tulikuwa hatuna mafisadi kama tulionao hivi sasa. Acha kulala usingizi mzito! fungua macho uone udhalimu wa mafisadi!
 
Back
Top Bottom