Timu bora ya soka duniani.

Danny Massawe

JF-Expert Member
Oct 15, 2012
1,295
755
Timu zipo nyingi duniani, ila wewe unafikiri ipi ndio inaongoza kwa ubora wa soka lake na mashabiki wake. Mi binafsi naona ni klabu iliyopo england jina lake linaanza na herufi A
 
timu 5 bora zaidi zipo South America. Sasa tuendelee:
6. Barcelona
7. Arsenal
8. ...
 
Nilikuwa namaanisha klabu, kwa timu za taifa spain haina mpinzani kwa sasa. Mi kwa mtazamo wangu arsenal inatisha
 
Japokuwa barca hatuwapendi kwa kutunyanyasa sana miaka ya karibuni lakini tuwatendee haki,,, wanatisha sana,,

Wakifuatiwa na chelsea fc champions league winner 2012,, up chelsea, blue is the colour this year... Let's go and defend back the title
 
England hakuna ntimu yoyote ya maana. Wanacheza mpira wa magazeti. WaTZ tumegubikwa na England Mania tu. Tujadili Barcelona na Real Madrid hizi mwisho wa kokoto. Hizi timu zinapocheza (EL CLASSICO) dunia yote ya Soccer Stands still. Hawa jamaa kila kitu chao ni bora. Viwanja vyao ni mwisho wa manaeno (NOU Camp na Santiago Bernabue). Zina nyota wawili hawa wanatoka sayari nyingine (MESSI Na CR). Barcelona wana mfalme wa kutoa pasi duniani (XAVI).
Hizi ni klabu mbili ambzo kwa pamoja zimeshinda Champions league mara nyingi kuliko zote duniani.
Achaneni na wapiga mateke wa England.
 
leo saa 6 usiku ni spain vs france world cup 2014 qualification group I ,uwanja wa vicente calderon jijini Madrid,sasa utaona ipi timu bora,spain ikiundwa na wachezaji wengi toka barca,na france ambayo wengi wanaitaja ndio kama japo sio wote ni arsenal style! maana diaby,giroud,koncielyn wa kujifunga,sagna majeruhi achilia mbali waliohama kina clichy na nasri.
 
Kwa wale wana arsenal mi naona sasa GIROUD anaanza kuonyesha mambo,lile bao alilopiga jana lilikuwa kali sana. Pia alilowapiga westham lilikuwa powa. Atakuwa mkali sana
 
England hakuna ntimu yoyote ya maana. Wanacheza mpira wa magazeti. WaTZ tumegubikwa na England Mania tu. Tujadili Barcelona na Real Madrid hizi mwisho wa kokoto. Hizi timu zinapocheza (EL CLASSICO) dunia yote ya Soccer Stands still. Hawa jamaa kila kitu chao ni bora. Viwanja vyao ni mwisho wa manaeno (NOU Camp na Santiago Bernabue). Zina nyota wawili hawa wanatoka sayari nyingine (MESSI Na CR). Barcelona wana mfalme wa kutoa pasi duniani (XAVI).
Hizi ni klabu mbili ambzo kwa pamoja zimeshinda Champions league mara nyingi kuliko zote duniani.
Achaneni na wapiga mateke wa England.

Urongo!
El-Classico kitu gani bana, pata timu ucheki Superclasico ya La BOMBONERA inayowachezesha CA Boca Juniors na River Plate, halafu uje urudie maneno yako.
Kwangu mimi timu bora ama inatoka Brasil au ni CABJ a.k.a La Boca.
 
Timu zipo nyingi duniani, ila wewe unafikiri ipi ndio inaongoza kwa ubora wa soka lake na mashabiki wake. Mi binafsi naona ni klabu iliyopo england jina lake linaanza na herufi A

Coastal Union ya Tanga ndio bora kwa sasa, usiniulize kwa nini!
 
1.Simba Sports Club
2. Liverpool Footbal Club
3. Barcelona
4. Boca Juniors
5. Riverplate
 
Back
Top Bottom