Timing ya Uondoaji wa wamachinga Mbeya

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,711
2,226
Serikali ya mbeya walikuwa waanze ilo zoezi mapema mara tuu baada ya kupata RC mpya.
Wakangoja bunge lianze ili Sugu awe hayupo jimboni wakidhani uwepo wake ungechochea vurugu zaidi.Wakashindwa kujua kuwa wana Mbeya hukisimamia kile anachoamini at any risk and cost!
Hatimae imebidi kumtumia mbunge kutuliza fujo!
 
Kandoro ni totally failure katika uongozi. Alilianzisha dsm baadae akarudia mwanza na sasa kalianzisha mbeya!
 
Kandoro sijui ana gundu gani,inakupasa kusoma mazingira angalau ata mwaka ujue wana mbeya wakoje!
Sasa mziki kama huo kaunzishe Mbozi aka wataalamu wa siraa za jadi uone mziki wake
 
Kandoro ni totally failure katika uongozi. Alilianzisha dsm baadae akarudia mwanza na sasa kalianzisha mbeya!

sijui hata kama alikuwa anafulu darasani yaani akili zake zimekalia sijui wapi....hovyo kabisa huyu mzee..ye anafikiri anapimwa effectiveness yake kwa kuwaondoa wamachinga....bure kabisa hili zee
 
Kandoro anajiona jembe kwa vile amezungushwa majiji yote! Na watumishi kadhaa wa manispaa ambazo ameziongoza wamekuwa wakimsifia, pamoja na makesheshe yote hayo.
Ila labda mi kipofu, sikumbuki ubunifu wowote wa maana ambao amewahi kuufanya pale dar zaidi ya ubabe wa kupiga marufuku maji ya kwenye vipakti.
Hamna siku itawezekana wananchi waanzishe kwa ubunifu wao masoko na sehemu za kutengeneza riziki, afu kesho aje mpuuzi mmoja tu RC (awe Kandoro au yeyote) aanze kuwafukuza kwa kigezo cha uchafu!
Uongozi ni ubunifu kwa kutokana na maono...
 
Kazi ya halmashauri ni kutoa huduma za jamii ikiwemo usafi wa miji husika! Ni wajibu wa halmashauri wanapoona eneo la biashara fulani ni chafu basi walisafishe na si kuwafukuza watumiaji wa eneo husika. Jiji la mbeya walitakiwa kuboresha maeneo ya hayohayo waliopo wamachinga kwa kujenga miundombinu bora ya biashara!! jiji wana wahandisi, wabunifu majengo na watalaam wengine, kwa nini wasibuni structures hata za muda na zenye kuwa na muonekano wa usafi badala ya kubomoa? Maana Kama ni uchafu basi hata soko la SIDO hapo hapo Mbeya ni Chafu kwani vibanda vimejengwa ki-uchafu uchafu! likewise masoko mengine kama mbalizi, Mkuyuni mwanza, Tandale Dar, Sinza makaburini, Kimara mwisho, na mengine mengi!!
Ifike wakti serikali inapoona raia wake wameanzisha jambo fulani kwa maendeleo yao basi iweke mkono wa support badala ya mkono wa discauragement!!! iweke ubunifu wa kitalaam wenye kuwahamasisha raia kuongeza uzalishaji badala ya kuwakatisha tamaa!!
 
Kandoro ni totally failure katika uongozi. Alilianzisha dsm baadae akarudia mwanza na sasa kalianzisha mbeya!

Atakuwa na kimavi kimemganda kwanini kila mkoa anaoongoza ni fujo tupu? Nenda dar kaoge na maji ya chumvi baharini kikutoke babu
 
Nilishawahi kusema kuwa ipo siku HAKI itaishinda DHULUMA hili la mbeya ni Mwanzo tu.
 
Ujue serikali ya magamba iko kimaslahi wanaeza kukuambia tumepata mwekezaji hata kwenye mambo madogo ambayo wazawa tunayafanya vizuri kabisa
 
Kazi ya halmashauri ni kutoa huduma za jamii ikiwemo usafi wa miji husika! Ni wajibu wa halmashauri wanapoona eneo la biashara fulani ni chafu basi walisafishe na si kuwafukuza watumiaji wa eneo husika. Jiji la mbeya walitakiwa kuboresha maeneo ya hayohayo waliopo wamachinga kwa kujenga miundombinu bora ya biashara!! jiji wana wahandisi, wabunifu majengo na watalaam wengine, kwa nini wasibuni structures hata za muda na zenye kuwa na muonekano wa usafi badala ya kubomoa? Maana Kama ni uchafu basi hata soko la SIDO hapo hapo Mbeya ni Chafu kwani vibanda vimejengwa ki-uchafu uchafu! likewise masoko mengine kama mbalizi, Mkuyuni mwanza, Tandale Dar, Sinza makaburini, Kimara mwisho, na mengine mengi!!
Ifike wakti serikali inapoona raia wake wameanzisha jambo fulani kwa maendeleo yao basi iweke mkono wa support badala ya mkono wa discauragement!!! iweke ubunifu wa kitalaam wenye kuwahamasisha raia kuongeza uzalishaji badala ya kuwakatisha tamaa!!

Umenena vema mkuu. Ni hii tabia ya viongozi kutaka kubuluza watu kila wakati ikome, kwani wakati sio rafiki kwao tena. Wananchi wemebadilika pamoja na mazingira.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom