Tikitimaji kwa afya yako

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,648
Wanajamvi, nitakuwa nawaletea faida ya matunda na mimea mbalimbali kwa ajili ya afya zetu, nikianza na TIKITIMAJI:

Kuna imani kwamba tikitimaji (kama jina lake) ni tunda lililojaa maji kwa wingi na sukari. Ukweli ni kwamba, katika matunda, tikitimaji ni mojawapo lenye virutubisho vingi vyenye asili ya vitamins, madini, kuondoa sumu (antioxidants) kwa kiwango cha chini cha karoli.

Tafuta tikitimaji lililo imara, zito na mviringo lisilo na sehemu laini au michubuko. Likatekate vipande na lichanganye na vipande vya barafu kwenye 'blender' upate juisi nzuri ya kutuliza kiu, hasa baada ya mazoezi (mwanamichezo), au jioni utokapo kazini (mfanyakazi) au shambani (mkulima).

Kinywaji hicho, mara kwa mara, kitaupa mwili wako uwezo wa kujilinda dhidi ya magonjwa kadhaa km pumu, BP, kansa, kuvimbiwa, magonjwa ya ngozi, na maumivu ya misuli.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom