TIGO sasa mnakera!

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
23,914
23,077
Kumekuwa na usumbufu mwingi wa mtandao huu wa Tigo toka wiki iliyopita, unampigia mtu simu kupitia mtandao huu unawekewa muziki tu na kuambiwa mtu huyo unayempigia hapatikani wakati simu yake iko hewani, unawapigia "customer services" bado unawekewa muziki tu na kuambiwa haipatikani. Hali hii imetokea kwa watumiaji wengi wa mtandao huu kuanzia wiki iliyopita.

Kibaya zaidi sijasikia kuomba msamaha kutoka kwa wakuu wa mtandao huu wa TIGO kuhusu usumbufu tunaopata watumiaji.
 
Jamani tahadhari na hatari! Kwa sasa tigo kumekua tishio, wizi umekithiri na ma-wakala wa tigo-pesa baadhi wameanza kusitisha huduma. Kuna mchezo unafanywa wanachokifanya wanawatuma kwenda kutoa hela kwa wakala akifika anatoa kiwango kama laki moja,anapewa kisha anasaini akisha maliza kuchukua anaanzisha lawama kama vile alitoa mara mbili,ukimdai msg ya pili anadai nimeifuta. Kisha anaondoka kwa hasira anaenda moja kwa moja hadi kwao anataja namba ya yule wakala kisha wahamisha hela kwa wakala husika. Wakala ukiuliza anajibiwa mkato, akienda ofisi kwao anambiwa kitengo hicho mhusika hayupo, mara katoka ilimladi kukudhoofisha. Wamekua wakifanya hiyo kwa kushilikiana na baadhi ya watu. Kaa chonjo wewe wakala ambaye hujapatwa na msala huu, kwa anaebisha kuhusu wizi huu nipo tayali kutoa ushaidi wa nyalaka zilizotumika.
 
Jamani tahadhari na hatali!
Kwa sasa tigo kumekua tishio,wizi umekisili na mawakala wa tigo-pesa baadhi wameanza kusitisha huduma.kunamchezo unafanywa na customer care wa kitengo cha m-pesa

Hapo penye red, Kama vile umechanganya?
 
Tulizoea wizi wa bunduki na wezi wanaume (Wakiwezeshwa wanaweza),
hali imebadilika mwizi mkubwa anaitwa fisadi, hakimu wake ni mtukufu sana Raisi, hukumu yake huwa ni urudishe kile ulichoiba, mwizi wa kati huitwa Mjasiria mali yeye anapoiba na akakamatwa huukumiwa na wateuliwa wa mtukufu, hukumu huwa ni kuwapa pasu waheshimiwa sana hao.

Mwizi mdogo huwa ndo hawa hujitahidi kuiga mbinu za wakubwa zao, lakini sehemu ya fungu huwakilisha kwa wajuu wao.

Kweli Kukusanya usipotawanya, na kuvuna usipopanda = bongo life
 
Tulizoea wizi wa bunduki na wezi wanaume (Wakiwezeshwa wanaweza),
hali imebadilika mwizi mkubwa anaitwa fisadi, hakimu wake ni mtukufu sana Raisi, hukumu yake huwa ni urudishe kile ulichoiba, mwizi wa kati huitwa Mjasiria mali yeye anapoiba na akakamatwa huukumiwa na wateuliwa wa mtukufu, hukumu huwa ni kuwapa pasu waheshimiwa sana hao.
Mwizi mdogo huwa ndo hawa wakina lulu, hujitahidi kuiga mbinu za wakubwa zao,lakini sehemu ya fungu huwakilisha kwa wajuu wao.
Kweli Kukusanya usipotawanya, na kuvuna usipopanda = bongo life

hivi mmoja wa boss tigo ametoa kauli ya matumaini kwamba anafatilia,ikipita siku mbili tangu leo inabidi kufata taratibu za kisheria maana kwetu wamehamisha pesa za kutosha,
 
Wanajamf leo hii nimepanda zangu mlimani city nikarudisha lain ya Tigo bahada ya ufumlifu wa kutosha nimeachana na kuachana mitandao ya maji taka je wewe
 
Tulizoea wizi wa bunduki na wezi wanaume (Wakiwezeshwa wanaweza),
hali imebadilika mwizi mkubwa anaitwa fisadi, hakimu wake ni mtukufu sana Raisi, hukumu yake huwa ni urudishe kile ulichoiba, mwizi wa kati huitwa Mjasiria mali yeye anapoiba na akakamatwa huukumiwa na wateuliwa wa mtukufu, hukumu huwa ni kuwapa pasu waheshimiwa sana hao.
Mwizi mdogo huwa ndo hawa wakina lulu, hujitahidi kuiga mbinu za wakubwa zao,lakini sehemu ya fungu huwakilisha kwa wajuu wao.
Kweli Kukusanya usipotawanya, na kuvuna usipopanda = bongo life

imekaa vizuri mkuu.
 
Naunga mkono 100%. Hawa jamaa wezi Watupu . Wanatuibia wateja bila aibu naungana nawe kuanzia January baada ya kumalizia balance yangu nautema rasmi mtandao wa wezi
 
kweli maisha ni magumu. Nimesoma blog moja, kuna mama amekunywa sumu kutokana na ugumu wa maisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom