tiGo ni soo - waja na sent 50 (thumni) kwa sekunde

Madabwada

JF-Expert Member
May 8, 2009
541
314
Hawa jamaa hawashikiki ... wanataka kuwapagaisha voda au?? nimesikia nyepesi wanakuja na thumni kwa sekunde. Ngoja tukae mkao wa kula!!! lol!
 
kwa mtindo huo watauwa bendi completely
Hawaui Mkuu!
Ujue, mpaka kufikia uamuzi huo, ni tayari mahesabu yashafanyikaga na kuona hakuna maneno itakayoharibika!
Wamekusanyaga hela mingi sana hawa!
Hii ndio faida ya Ushindani wa kibiashara, faida kwa mlaji!
 
kijana acha chai!ww umesikia wap na hizo redio mbao?

Tariffs hizo tayari zinatumika na wateja wa Zantel, kwa hiyo sio kitu kipya na haiwezi kuwa surprising iwapo Tigo wataiga Zantel. Hata shilingi moja kwa sekunde ilianza na Zantel kabla haijaigwa na hawa wengine.
 
Tariffs hizo tayari zinatumika na wateja wa Zantel, kwa hiyo sio kitu kipya na haiwezi kuwa surprising iwapo Tigo wataiga Zantel. Hata shilingi moja kwa sekunde ilianza na Zantel kabla haijaigwa na hawa wengine.

mshikaji unataka kuanzisha ligi au?? get your facts straight mkuu!!
 
Bora maana huu ndo mtandao wa wanafunzi wa walala hoi. real tigo wanatujali.
 
wametunyonya sana, wajua kupiga simu hapa Tz ni ghali kuliko hata UK na US ambako maisha kwa jumla ni gharama zaidi
 
Voda changa la macho eti kuanzia saa 11.00 jioni hadi saa tatu bei kama ya zamani wapi na wapi wezi wakubwa hao

Mambo yapo tiGO bwana
 
Inawezekana; na hii itasaidia kuwafanya akina Voda na Zain waendelee kushusha gharama zao.
 
If marginal revenue = marginal cost, wanaweza kufanya hivyo kama wameamua kutoa huduma tu bila kutengeneza faida.
 
safi sana ombi langu kwa mungu ni hili eeh mungu ushindani huu usiichie kwenye makampuni ya cm tu yaanzishwe na tanesko pia amen
 
If marginal revenue = marginal cost, wanaweza kufanya hivyo kama wameamua kutoa huduma tu bila kutengeneza faida.

Mkuu hii habari ni ya kweli "TRUST ME" Kuna jamaa anafanya kazi tiGO ameniambia kwamba hii kitu ni kweli na inaanza kesho. ACHANA NA HABARI YA SIKU YA WAJINGA. This is True.
Ila haitakuwa 24hrs, nafikiri ratiba yake itafanana na ile ya voda.
Pia itakuwa sh 1 kwa dk ya kwanza halafu zile dk zinazo endelea ndio 0.5sh.
Haina kujiunga hiyo si unajua mambo ya tigo?
 
Thumni kwa sekunde kwa saa 20 kwa siku. Vigezo na masharti kuzingatiwa.

TiGo
Express yourself.
 
Tigo bei rahisi lakini upatikanaji wa simu, usikivu, customer care ni matatizo makubwa.

mnapobanwa mbavu lazima mtafute visingizio ... usisikilize uzushi mkuu (vodacom propaganda), hayo mambo mbona ni historia mkuu?? me huwa nalonga tu bibi na babu zangu upcountry bila matatizo yoyote yale ... halafu kichekesho hicho kijiji voda huwa haipatikani .... phuuuh ha ha ha ha ha!
 
Back
Top Bottom