TIGO huu sasa Utapeli wa wazi!!

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,458
29,151
Nimekwama mahali na sina vocha,
Ninaempigia ambae ndie mwenye ufmbuzi wa tatizo langu hapatikani kwa tigo na najua namba zake zingine za mitandao mingine nashawishika kukopa kwakua sina Jinsi!!
Na mkopo wenyewe nitaulipa kwa Riba kubwa tu!!
Kama ndivyo, kwanini mnanichagulia watu wa kuwapigia??
Ni lazima nimpigie wa tigo tu?
Masharti ya nini kwenye mkopo ambao nitaulipa??
Kwani mmenipa msaada sasa??
Huu ni utapeli na unyanyasaji uliopitiliza huu
 
Haswaa umewapa ukweli nadhani watarekebisha wajaribu kushindanisha biashara zao kwa kuwapa uhuru wateja wao
 
Nimekwama mahali na sina vocha,
Ninaempigia ambae ndie mwenye ufmbuzi wa tatizo langu hapatikani kwa tigo na najua namba zake zingine za mitandao mingine nashawishika kukopa kwakua sina Jinsi!!
Na mkopo wenyewe nitaulipa kwa Riba kubwa tu!!
Kama ndivyo, kwanini mnanichagulia watu wa kuwapigia??
Ni lazima nimpigie wa tigo tu?
Masharti ya nini kwenye mkopo ambao nitaulipa??
Kwani mmenipa msaada sasa??
Huu ni utapeli na unyanyasaji uliopitiliza huu
TIGO ni wezi tu. Ninachikifanya ni kuwahamasisha jamaa na ndugu zangu kidogo kidogo kuchukua line za mitandao mingine then wajionee wenyewe utofauti. Mtu umekopa then unapewa masharti ya aina gani ya mtandao unaruhusiwa kupiga. Lakini pia kwanini unipangie kiasi cha kukopa. Nipe range kutegemea na matumizi yangu. Sasa kama mtu amezoea kutumia 2000 wanakukopesha 1300 then unarudisha 1420. Je pengine kwasababu ya shida yangu labda nipo mahali siwezi kupata vocha na 500 ingenitosha, kwanini usinipe option ya kuchagua kiasi ila nisizidi matumizi yangu. Kwanini unilazimishe kukopa kiasi chote hicho? Mbaya zaidi huwezi kupiga kwa mtu mwenye line nyingine kama Airtel, Voda Zantel etc.
Lakini zaidi ya hiyo charge yake ipo juu zaidi ya wanavyojitangaza kwenye matangazo yao.
Kuna vocha zoa zaTSH 2000 nazo zinatatizo sana, ukikwangua na kujaribu kuongeza salio nyingi zinagoma na kukupata message kuwa ni invalid nalo hili wamekaa kimya. Hawaapologoies kwa watumiaji maana si kila mtumiaji anajua nini afanye anapokwama au kughafirika na huduma.
Ila solution rahisi ni kuachana nao na kuhamasisha jamaa zako kuachana nao.
Huo ni WIZI, TCRA wanatakiwa kuliua hilo na kuchukua hatua.
 
Mm nliwarushia lain yao pale mlima city bahada ya kukataa kuniunganisha na internet kwenye simu yangu. nipo natumia voda na airtel nakushangaa unaetumia tigo mpaka sasa
 
Ukikopa 1,300 utarudisha 1,430 (riba 130 ambayo ni 10%) tuseme ndani ya siku mbili.
Hivi kweli kuna watu wanaoangalia hizi rate kama zinawiana na halisi ya Mtanzania?
10% kwa siku mbili ni sawa na 1,825% kwa mwaka!!
Tukirudi kwenye somo, ni kwanini wanatulazimisha kuwapigia tigo tu wakati salio lenyewe ni letu??
Kwanini wasituruhusu tuwe na full access kwenye hili salio??
Tena kwakuwa tunalilipia riba kubwa ikiwezekana access yake izidi hata lile salio la kawaida?
 
Wakuu mimi nina ushauri mmoja. Tujaze attachment ya form ya malalamiko ya mtumiaji wa huduma za maasiliano (hii inatoka TCRA,nimeattach) then tuzitume kwa wingi kwenda dq@tcra.go.tz tuone hawa watanzania wenzetu watatusaidiaje kwa sababu haya malalamiko dhidi ya tigo yamekuwa mengi mno siku za karibuni.Kama hii thread haitotembelewa sana(kutokana na kuzoeleka kwa haya malalamiko) nashauri ianzishwe thread mahususi.Huenda tukafanikiwa who knows!!
View attachment fomu_ya_Malalamiko.pdf View attachment complaintform.pdf
 
Hivi kwanini Mods wasiandae mchakato ili wawakilishi wa haya makampuni wawe wanakuja hapa na kutujibu kero zetu?
Kama kweli wanawapenda wateja hao, ili kuzui kuendelea kuharibu public image ya kampuni, wangekuja tu tukawapa kero moja baada ya nyingine.
Sio lazima wanasiasa tu, huu mtandao unagusa nyanja nyingi sana katika maisha yetu ya kila siku
 
Back
Top Bottom