Tigo customers services balaa

Hii ni wiki takriba ya 3 na jaribu kutuma SMS kwenda nje ya nchi South Africa/USA bila mafanikio,niki tuma SMS kwenda South ina kwenda na nakatwa pesa kwenye simu ila haifiki kwa muusika aliyetumiwa,kwa upande wa USA ina goma kabisa kwenda na inanionyesha alama ya X badala ya tick...Nimejaribu kupiga namba 100 ya Customer services bila mafanikio yoyote jibu ninalo lipata ni kwamba ni "Akikisha namba unayo piga na upige tena" Swali: hawa jamaa wamebadilisha namba ya huduma kwa wateja au ndio wametuchoka wateja wao? Najuta kujiunga na huu mtandao!
Wadau wa JF je kuna mtu yoyote amekumbana na tatizo kama la kwangu?
kweli kabisa hata mimi nilijaribu kutuma sms kwenda nigeria tigo wakaniambia message not sent nikajaribu tena na tena kama mara 6 kuja kucheki salio tigo wakawa wamelamba karibu 1000.
sasa nashangaa kwanini wanachaji garama ya kutuma meseji wakati hawatumi hizo meseji?
huduma mbovu!
 
hiyo extreme haipo tangu lini?sisi ndo watumiaji wa tiGO NA EXTREME TUNAYO ILA IPO KWA DAKIKA 200 which is still fairer bado tunaenjoy 1.3 ths per second ambayo ni for 24 hrs na pia haina masharti ya kujiunga wal kuomba
not only that tigo is fairer than voda or zain when you call from tigo to other networks kuliko ukitumia zain au voda kwenda mitandao mingine

naema haya kwani i have all three lines and all are active but still tigo is best to me
 
Tigo Customer care kwa sasa ni namba 15301 na si namba 100 kama zamani gharama ni Ths 100 na si bure kama Zamani.
 
Siyo Customer Service tu yaani hawa jamaa huduma zao zote kwa sasa ni mbovu kabisa.

Si kweli hata kidogo labda kama una ajenda ya siri hapa. Mimi natumia Tigo lakini sijaona matatizo yoyote. Natuma na kupokea sms kutoka sehemu tofauti za dunia bila shida. kuna haja ya kutafuta kiini cha tatizo kwanza kuliko kukimbilia kuwalaumu Tigo. Inawezekana tatizo lipo kwa huyo unayemtumia sms.

Tiba
 
Mkuu Tiba
Sina ajenda yoyote mbaya kwa kampuni ya tigo kwani mimi ni mteja wao wa miaka takribani 7 hivi, hivi unaweza kuniambia ni mtandao gani ambao hauna huduma kwa wateja? endapo mteja atapata tatizo ataliwasilisha wapi? inasemekana namba ya huduma kwa wateja imebadilishwa je kwa nini wasitujulishe sisi wateja wao kama kweli ni mtandao makini ?.

Mkuu unapo sema ujapata tatizo lolote toka tigo na kubaliana na wewe kuwa inawezekana kweli ujakumbana na tatizo lolote kwani ya wezekana watu unaowasiliana nao unawasiliana nao kwa mwaka mara 1!

Angalia mtiririko wa hii thread huone ni watu wangapi wametoa malalamiko yao ya kukumbana na matatizo kwenye mtandao wa tigo. Nia yangu hasa ya kuweka thread hii ni hili wausika wa mtandao huu wapati ujumbe huu na kuweza kurekebisha hayo matatizo.
 
jamani hawa wameidiwa na wateja mitambo inapumulia mashine msifanye masihara
 
hiyo extreme haipo tangu lini?sisi ndo watumiaji wa tiGO NA EXTREME TUNAYO ILA IPO KWA DAKIKA 200 which is still fairer bado tunaenjoy 1.3 ths per second ambayo ni for 24 hrs na pia haina masharti ya kujiunga wal kuomba
not only that tigo is fairer than voda or zain when you call from tigo to other networks kuliko ukitumia zain au voda kwenda mitandao mingine

naema haya kwani i have all three lines and all are active but still tigo is best to me
matambo: sikiliza ni kweli nilipata shida kupata hiyo exreme mwishoni mwa wiki jana. Niliandika neno extreme nikatuma 15372 kama nilivyokuwa nafanya huko nyuma sikupata jibu lolote kabisa.

Sasa hapo nikisema hiyo extreme haipo nakosea wapi? Wewe unaipata wengine hatuipati sasa tusiseme?

Hapa tunapotoa malalamiko yetu si kwa ajili ya nia mbaya. Mimi ni mteja wa tigo kwa miaka mingi (tangu 1998) wakati huo namba yangu ikiwa 788024 nikiwa nimeipatia Mwanza. Baadaye nilipoteza simu na line hiyo nikapata simu nyingine na nikaamua kutumia line ya Voda na Celtel wakati ule nikiwa na namba 887920 kwa mitandao yote miwili lakini huduma ya mitandao hiyo kwa gharama niliona haiwezi kulinganishwa na tigo hivyo nikaomba tena tigo namba yangu ya mwanzo na nilipohitaji namba hiyo baada ya miezi mitatu kupita tangu nilipoacha kuitumia sikuipata tena wakidai imechukuliwa na mtu mwingine.

Kwa kuwa niliipenda tigo nililazimika kuchukua namba nyingine xxx546 ambayo nimeisajili na naitumia mpaka leo. Ninayo line ya Zantel na zain pia.

Kwa siku hizi kwa kweli pamoja na kuwa fair katika bei lakini bado huduma yao imeshuka sana. mtandao wao una kelele nyingi sana, ukipiga kila simu unaambiwa haipo namba hiyo lakini kadri unavyoendelea kuipiga baadaye unaweza kuipata, inachukua muda mrefu ku connect simu ( yaani ukipiga simu inakuwa kimya kwa dakika moja na kisha ndipo inaunga..... na matatizo mengine mengi. Tunalalamika ili tutendewe haki na kampuni isipoteze wateja maana kuna mitandao mingi mingine iliyo cheap kuliko tigo iko mlangoni ingawa sisi tumeipenda tigo.

Tigo wajirekebishe wana matatizo. Bahati tu kuwa customers tume rise voice. Si hivyo wangekuta tumekimbilia kwenye ile mitandao ya mafisadi tanzania.
 
Nimefanikia kupata namba ya huduma kwa wateja ambayo ni. 0713 800 800

Tigo Customer care kwa sasa ni namba 15301 na si namba 100 kama zamani gharama ni Ths 100 na si bure kama Zamani.

Ipi ni namba sahihi? Bado sijaelewa kwa nini mtandao wa Tigo wanacharge huduma kwa wateja shilingi 100. Nilidhani huduma hii inatakiwa kuwa bure kisheria!
 
Hii ni wiki takriba ya 3 na jaribu kutuma SMS kwenda nje ya nchi South Africa/USA bila mafanikio,niki tuma SMS kwenda South ina kwenda na nakatwa pesa kwenye simu ila haifiki kwa muusika aliyetumiwa,kwa upande wa USA ina goma kabisa kwenda na inanionyesha alama ya X badala ya tick...Nimejaribu kupiga namba 100 ya Customer services bila mafanikio yoyote jibu ninalo lipata ni kwamba ni "Akikisha namba unayo piga na upige tena" Swali: hawa jamaa wamebadilisha namba ya huduma kwa wateja au ndio wametuchoka wateja wao? Najuta kujiunga na huu mtandao!
Wadau wa JF je kuna mtu yoyote amekumbana na tatizo kama la kwangu?

Hii ndiyo shida ya bure. Kupenda bure kwa Watanzania. wengi walijifanya kuanza kuacha line zao za uhakika kama Zain na VODA lakini wote wanarudi. Hakuna kitu cha bei rahisi duniani kikawa kizuri. Angalia bei ya bidhaa ya china.
 
Ipi ni namba sahihi? Bado sijaelewa kwa nini mtandao wa Tigo wanacharge huduma kwa wateja shilingi 100. Nilidhani huduma hii inatakiwa kuwa bure kisheria!

hapo mwanzo hoyo ya 13800800 ilikuwa inaepusha usumbufu wa kusubiria foleni ya 100, hivyo ukipiga wanakata pesa kiasi, lakini unasikilizwa moja kwa moja bila kungoja.
 
Ndio maana tigo ni mbaya, matatizo yake ni makubwa. walioizoea wanaing'ang'ania tuuuu! usiku na mchana wanaliwa tu.

Leka
 
Back
Top Bottom