Tido Mhando na Ubinafsishaji wa TBC kwa StarTimes

Kikubwa katika ubia huu wa TBC na hiyo kampuni ya China ni kwamba sheria iliyounda mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) imekiukwa. Kwa mujibu wa gazeti la Mwanahalisi toleo la Agost 26 - Septemba 1, 2009, si serikali wala menejimenti ya TBC iliyotangaza zabuni (expression of interest) ili makampuni mengine nayo yaweze kupeleka maombi ya kushirikiana na shirika hilo katika mfumo mpya wa utangazaji. Hapa ndipo kwenye maswali! Na uchunguzi ukifanyika mnaweza kukuta Manji yumo kwenye hiyo kampuni ya China kwani keshamuweka mfukoni Tido Mhando na menejimenti nzima ya TBC.
 
Sikuamini mzoefu kama GT anaweza andika utumbo kama huu alioutoa hapa!

Mkuu Kasheshe, sijakuelewa, Mara nyingi zikubaliani na GT kwa mambo mengi lakini kwa hili nitamsaidia kuweka hata docs. Kuna mambo GT ameweka hisia zake kidogo lakini si vibaya na yeyote anaweza kuweka hisia zake (Where We Dare to Talk Openly), ila kwa kweli hapa kuna tatizo kubwa sana kuhusiana na huu ubia kati ya TBC na Wachina.

Kuna tatizo kwa sababu hayo masafa ni maalumu kwa ajili ya umma na kwamba yanagusa hata USALAMA WA TAIFA (tutasikia hapo baadaye) kwa hiyo kampuni inayoingizwa lazima iwe imefanyiwa upekuzi (Wachina hawajafanyiwa upekuzi kwani imefanywa chapu chapu). Unajua baada ya kuondoka analogue kwenda digital, TV stations hazitaruhusiwa kumiliki minara bali studio tu na masafa yatamilikiwa na hizo kampuni tatu (tutajadili baadaye) na hivyo kwa TBC kuipa Star Technology ya China asilimia 65 ina maana ndio hawatakuwa tena na sauti katika televisheni ya taifa. Lakini kibaya ni kwamba katika MEMAT yao wanasema wazi kwamba NI MARUFUKU KUUZA HISA KWENYE SOKO LA HISA (Any invitation to the public to subscribe for any share or debenture of the company is prohibited). Hii ni HATARI kubwa.
 
Last edited:
Kaka karibu!!!!

Join Date: Fri Aug 2009
Posts: 1
Thanks: 1
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
 
Duh... mpaka tujue uko wapi? hii balaa au ndo kutamba kwenyewe??

yah maana huyu bwana aliniambia nisome mwanahalis ya leo sasa kwa umbali uliopo ni ngumu na website ya gazet hili siku hiz haifunguki.

tafsi unavyoweza!
 
huyo ndiye Tido Mhando ambaye alithuibutu kuwaambia ma meneja wake wamwongopee Mkaguzi mkuu wa serikali!!!

hivi baada ya Nyerere the only Tanzanian institution iliyokuwepo ilikuwa ni TBC nayo kwa sababu anazozijua Tido na waajiri wake wameamua kuigawa

this is really sad! Tangu lini PUBLIC BROADCASTING SERVICE ikabinafsishwa?
 
Kusema ule ukweli TBC inasikitisha! Ni kuganga njaa kwa akina Mhando, wakaamua kulamba viatu vya Manji. Matokeo ndiyo hayo sasa. Kwanza toka imebadilishwa jina kutoka TVT kuja TBC, chini ya Tido, mambo yamekuwa ovyo ovyo tu. Sasa wachina ndio watakuwa na sauti kubwa kwa sababu ya hiyo asilimia 65 ya hisa. It is no more public.

Anajifanya kuiga ya BBC bila dhamira wala dira (mission and vision).

Kila nikijaribu kuingia website yao (www.tbcorp.org), hakuna kitu. Nikaenda ofisini kwao kuulizia kulikoni. Wakaniambia haifanyi kazi. Nilichoka kabisa.
 
I'm very sad today!
Sikuamini mzoefu kama GT anaweza andika utumbo kama huu alioutoa hapa!
Mkuu Kasheshe, naomba ukanushe haya chini...

Huo ubia unampa mtu 65% ni ubia wa wapi? Halafu kwanza hiyo kampuni imesajiliwa kinyemela na Tido ndiye Director wakati yeye si mmiliki, yeye ni mwajiriwa kwa mkataba. Wamiliki ni serikali ikiwa chini ya Msajili wa hazina ama bodi. Pia BRELA wanasema imesajiliwa kimakosa maana wamekiuka sheria ya usajili inayotaka kutumia shilingi, wao wametumia dola katika memat yao. Mengine zaidi baadaye lakini inatisha.
 
Hivi Hawa Wanasheria wetu huwa wanapitia hizi paper au ndio hio 10%....!!! Wachina wanataka wamiliki kila kitu hivi sasa...!!! na wao lengo lao kuingia kila market...!!!

Vp Kuhusu Redio nayo?....Yale matangazo ya wachina kuuza Njugu na Kupiga debe ndani ya Bongo itakuwa basi tena...!!!
 
Hivi Hawa Wanasheria wetu huwa wanapitia hizi paper au ndio hio 10%....!!! Wachina wanataka wamiliki kila kitu hivi sasa...!!! na wao lengo lao kuingia kila market...!!!

Vp Kuhusu Redio nayo?....Yale matangazo ya wachina kuuza Njugu na Kupiga debe ndani ya Bongo itakuwa basi tena...!!!

Hivi ndugu hata wangepitia, ni kipi unachoona wamekosea kiasi cha kuwashangaa?
Inategemea wanasheria hao waliohusishwa jukumu lao lilikuwa nini na walipewa na nani kwa lengo gani.
 
Kuna mtu anaweza kutusaidia kuchokonoa Waziri wa Habari na michezo anasemaje juu ya hili? mbona wanakaa kimya wakiacha tunahaha kama vile hatujawaajili sie?

Tunataka tamko la serikali juu ya jambo hili kabla hatujaanza kufukunyua mengi.....

TBC ni mali ya Umma, tunawaomba wanasheria watushauri, hakuna mtu anweza kupinga hili mahakamani ikigundulika kuna ufisadi ndani yake? maana naona uko wazi....! tukisubiri Bunge likae, mkondo wa siasa kulisimamisha hili utachukua muda mrefu.

Its time to turn around our country...mianya hii wanayozidi kuivumbua inatusaidia kuonyesha nyufa zote mapema kabla ya uchaguzi mwakani!
 
Kama SISIEMU imediriki kubinafsisha chama chao watashindwa nini kubinafsisha chochote kilichopo mbele yao. Kama unabisha, fuatilia kwenye mikutano wa NEC na CC iliyopita zilimwagwa kiasi gani kumsulubu Sitta.......Wenye hisa nyingi ndo walikuwa wenye sauti kubwa though kupitia wanachama wengine. Hayo ndiyo mambo ya STOCK MARKET, right!!
 
Kama vile tu ubinafsishaji wa NBC (1997), Tanzania Railways na ATC ulivyotufanya yatutokee puani, bado hatujajifunza. Kwa mara nyingine tena tumejikita na kuamua kubinafsisha TBC kwa dolla million moja. ...!! Tunakubali kuuza uhuru wa vyombo vyetu vya habari kwa hela mbuzi namna hii... Tumelogwa!!

Kweli mnataka kusema kuwa imekosekana consortium ya Wazawa wenye kuweza kukusanya hata $5 million kwa ajili ya kuendeleza TBC?! Kwani hao Star Network wameshindwa nini kununua kibali na kuruhusiwa kuanzisha Tv zao wenyewe ili ku-stir competition mpaka wanalazimika ku-hold share majority kwenye taasisi ya Kitaifa?!
 
Wanabodi,
Kwa hili la TBC, nadhani kunahitajika explanations to make, wa kwanza kutufafanulia sio TBC, bali TCRA kutuelimisha hii transfer toka Analogy-Digital, what does that mean.

Baada ya hapo ndipo tutapata picha kwa nini service providers ni watatu tuu, Mhe. Dialo alitoa angalizo hili bungeni na kueleza kuna mchezo mchafu kwa milki ya masafa yote ya digital kupewa mtu kumiliki na wengine wote lazima wasubscribe ili kurusha matangazo yao. TCRA itufafanulie ndipo tuje kwenye kampuni ya Wachina na kelezwa ni ubia, ni ubifsishaji au ndio ishauzwa?.

Kwa ufahamu wangu, Digital Broadcasting ni kama inavyofanywa na DSTV, yaani unarusha channel zaidi ya 100 at a go, hivyo kwa nchi kama Tanzania na TBC yetu, kurusha tuu hiyo channel moja ni issue ndio maana kuikubalia kampuni moja kurusha matangazo yote its fine japo ni ukiritimba.

Bado naamini Tido is damm good kwa TBC ilivyokuwa na hii ya sasa. Damu mpya nyingi, Jambo Afrika, Jambo Tanzania ni kipindi bomba kuliko vyote Tanzania kwa wakati wa Asubuhi hadi ITV wameaiga na Star Tv pia wameiga.

Kitu kizuri kabisa kuliko vyote kuhusu TBC ni wamefungua milango kwa production houses kupeleka program zao kwa bei poa kabisa, kurusha program ya dakika 15 ni shilingi 500,000/= tuu!, haijawahi kutokea na labda haitapata kutokea tena!.
 
Pasco, mambo mengine kama ubunifu simpingi sana Tido pamoja na kuwapo kasoro za hapa na pale katika kubagua watumishi (tatizo hilo lipo sehemu nyingi) lakini kwa hili kuna tatizo kaka. Kwanza kwa chombo nyeti cha umma kama TBC hawakupaswa kwenda haraka haraka hivyo kusajili na kuingia ubia na kampuni nyingine ya nje kwa kisingizio tu cha kukosa mtaji kwa sababu suala hili la masafa limezungumzwa kwa muda mrefu sana na TCRA na TBC wameshiriki vikao kadhaa vya majadiliano. Tatizo sisi Watanzania tumezoea kuchukulia kila jambo kirahisi rahisi tu hata mambo mazito kama hili. Tatizo hili linaanzia katika ngazi ya kaya hadi Taifa, inasikitisha sana.

Kuhusu ufafanuzi wa TCRA, mengi yamo katika website yao ya http://www.tcra.go.tz lakini pia, TCRA wamefanya kazi kubwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kwa muda mrefu na inashangaza kuona kwamba TBC wamesajili kampuni chapuchapu kwa ubia na Star jambo lililosababisha kufanya hata makosa ya kisheria
 
Pasco, mambo mengine kama ubunifu simpingi sana Tido pamoja na kuwapo kasoro za hapa na pale katika kubagua watumishi (tatizo hilo lipo sehemu nyingi) lakini kwa hili kuna tatizo kaka. Kwanza kwa chombo nyeti cha umma kama TBC hawakupaswa kwenda haraka haraka hivyo kusajili na kuingia ubia na kampuni nyingine ya nje kwa kisingizio tu cha kukosa mtaji kwa sababu suala hili la masafa limezungumzwa kwa muda mrefu sana na TCRA na TBC wameshiriki vikao kadhaa vya majadiliano. Tatizo sisi Watanzania tumezoea kuchukulia kila jambo kirahisi rahisi tu hata mambo mazito kama hili. Tatizo hili linaanzia katika ngazi ya kaya hadi Taifa, inasikitisha sana.

Kuhusu ufafanuzi wa TCRA, mengi yamo katika website yao ya http://www.tcra.go.tz lakini pia, TCRA wamefanya kazi kubwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kwa muda mrefu na inashangaza kuona kwamba TBC wamesajili kampuni chapuchapu kwa ubia na Star jambo lililosababisha kufanya hata makosa ya kisheria
Halisi, kama sheria itakuwa kushoto kwao, je nani anaweza kutengua ubia huu.. TCRA, Bunge au Mahakama ndiyo wanaweza?!
 
kwanza hapa oneni kwamba TBC wamesajili kampuni Juni 26, 2009 na hapa chini tunaambiwa;

The deadline for submission of Expression of Interest is 2.00 pm local time on Tuesday, 30th April, 2008. EOI will be opened immediately thereafter at TCRA Head office, Mawasiliano House, Plot 304 Ali Hassan Mwinyi/Nkomo
http://www.tcra.go.tz/tenders/Exp_of_Interest_-MUX.pdf

Lakini pia jamani TBC ni public company, ni kampuni yetu si sawa na Channel Ten ya Tanil ama ITV ya Mengi au Star Tv (sio Star ya Kichina) ya Dialo. Hebu someni kifungu cha 3 hapa chini na zaidi 3.7.5, 3.7.6 na 3.7.21 kwa msisitizo na vingine kwa uchambuzi wenu wa ziada mkilinganisha na nyaraka za usajili wa Star Media (Tanzania) Limited.

http://www.tcra.go.tz/consultative_docs/digitalSwitchOverMultiplexOperator.pdf
 
Back
Top Bottom