Tido Mhando kwa mkono wa Mungu iokoe Tanzania

hayawihayawi sasa yamekuwa! Tido muhando rasmi aula al jazeera swahili sambamba na joseph warungo!
Uwepo wako huko ndugu tido utasaidia kuanika maovu ya serikali ya tanzania chini ya utawala dharimu wa ccm!

Mungu ibariki tanzania, mungu mbariki tido!

ltk/tiss
 
Kwani alifukuzwa kazi au mkataba wake uliisha?

Wakati haya yanamkuta pamoja na mkataba wake kwisha ila ukweli hawakumtaka huyu jamaa nasema hivi kwa sababu Kiongozi mkubwa mmoja ndani ya chama na serikali wakati wa sakata hilo nilikuwa naye ktk msiba wa jamaa yetu mmoja,nikaanza kuzungumza naye kuhusiana na sakata hilo maana liliniuma sababu nilikuwa TBC kipindi hicho nikifanya mafunzo yangu ya uhandisi wa mawasiliano.Basi nilipomuuliza kwa nini Mhando hakukupewa mkataba mwingine alinijibu kama ifuatavyo"HIVI WEWE UKIOA MWANAMKE UNAYEMPENDA SANA BAADAYE UKAKUTA MKE WAKO HUYO ANAFANYA MAPENZI NA JIRANI YAKO NA UKAMKATAZA TABIA HIYO AKAKATAA HAKUACHA JE UTAFANYA NINI?" Mimi kwa haraka zangu nikajibu "UNAMFUKUZA KWAKO NA KUOA MWINGINE UNAYEONA ANAKUFAA" Akanijibu hivi "CCM NA SERIKALI TULIMUOA MUHADO KUTOKA NJE YA NCHI NA ALIPOFIKA AKAWA NA MWANAUME MWINGINE HIVYO TUKAONA HATUFAI TUKAMFUKUZA,TULIMWABIA ACHA MIDAHALO YA VYAMA AMBAYO INAVIPA NGUVU VYAMA VYA UPINZANI HAKUTEKELEZA"Kwisha.

Nilichoka kwa majibu hayo nikawa mpole.Hiyo ndiyo hali halisi FF na Jf.:lol:
 
Na yule kijana orijino wa kipindi cha 'Uswahilini Kwetu / Kwetu Ushwazi' (jina lake nani vile) jembe sana yule kijana kuweza kuandaa kipindi kinachohusu jamii kilichokwenda shule mpaka walalahoi tusuuzike roho na kujihisi kama vile umasikini umetutoka kidogo vile.

Tido Baba; Muro na yule dogo wa Uswahilini Kwetu kuna vituko baba!!! Wafundishe kazi, waongoze vema kwenye mwanga wa kimataifa na kazi iendelee kiweledi zaidi mpaka kieleweke!!

watu wanaongea vitu vya maana we unajipigia promo!!!!!EATV hakuna anayepaswa kuitwa mtangazaji!!wote kule wazushi!!!wakosa kazi wakapata kingono au kishikaji!!!!
 
Nilidhani alidai maslahi na posho zaidi na alikuwa anataka alipwe kwa Dollar, jamaa wakashindwa masharti yake.

kilichomwondoa ni MICHAKATO MAJIMBONI na KURUSHA LIVE Kampeni za CDM. Alijaribu kubalance, lakini CCM wakamgomea
 
Fuatilia post yangu hapo juu namuongelea nani kabla hujakurupuka kutoa majibu. Utaratibu wa ajira wa Al-Jazeera ni lazima uwe na digrii angalau moja. Sasa kama wewe unabadilisha utaratibu basi haya jaribu.

Mwita 25, kwanza I doubt kama Tido kaomba kazi Al Jereera maana kama katoka BBC, alirudi nyumbani kwa uzalendo tuu, sasa Al Jazeera aende akafanye nini?. Aljazeera na BBC ni sawa na timu ya ligi na timu ya mchangani, mimi kwa Tido nimjuaye, hawezi kurudi timu ya mchangani.

Kama unamzungumzia Jerry, you are wrong, Jerry ni degree holder wa UDSM na amefanya post graduate US!.
 
HONGERA SANA MGOSI. ENDELEA KUIWAKILISHA FANI YAKO VEMA UKIJUA KUWA SIKU ZOTE MTU MZURI HAKUBALIKI KWAO.:plane:
 
Mzee Tido, waandishi vijana wako hapa nyumbni uhuru wao sasa mashakani zaidi!!!!!!!!!!

Hakuna kutofautiana na kile akipendacho Nchimbi tena hivi sasa si kwa TBCCM tu bali ni azimio ya kimya kimya kwa vyombo vyote vya habari kuminywa kwa sauti huru kila mahali wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.

Mambo sasa kweli ni ujima ujima tu kwenda mbele.
 
Wabongo kwa fitna. Tido mkataba wake uliisha wala hakutimuliwa.
 
huwa wana slogan wanasema "All the news all the time" na kati ya magwiji ya habari katika ukanda wa Afrika Masharaki walio wahi kutokea na Tido ni mmoja wao....tumekosa tv ambazo viko constructive kwa muda mrefu, tumekosa utamu wa mahojiano..eti tuna dk. 45 na Semunyo..ukiangalia unapata kichefuchefu hakuna mtu asha wahi kubana maswali mpaka akataja ambavyo hakutegeme......mimi naona mahojiano mengi yanayofanyika kwenye tv zetu ni as if mtu anaenda kulihutubia Taifa na si kuhojiwa
 
Back
Top Bottom