TICTS: The inside story

Nakumbuka Karamagi alitakiwa kuwasilisha nyaraka kwa ajili ya kutoa ushadi ya kuwa ni kikao cha mawaziri kilikaa na kutoa makubaliano ya kuongeza ,kataba kama sikosei, hivi iliishia wapi au ndo inasubiriwa kikao kijacho??? maana kama hajafanya hivyo nategemea huyu mbunge apewe adhabu kwa kulidanganya bunge

Naomba msaada wa kujua hilo
 
""mkuu Single D"

Uko Right Kabisa Hawa Watu Wanatuibia Kwa Kubadili Majina Ya Kampuni Huku Mmliki Yuleyule .....just For Breaking News Waheshimiwa Wa Celtel Wanabadilisha Jina Kuanzia July Wataitwa ""zein"" Kukimbia Kodi Hii Ndio Tanzania Tajirisha Kichwa Chako Utajiri Tosha Naona Watanzania Wanazidi Kuumia ,,,haya Tujipe Moyo......

""mkuu Tuandamane""

Ile Issue Ya Karamagi Ameshawasilisha Mkuu Na Kikao Kijacgho Tunatarajia Mambo Makubwa Ikiwemo How Come Jamaa Akamata Docs Za Maaumizi Ya Baraza La Mawaziri Wakati Hakuwa Waziri Kutakuwa Na Kazi Kubwa Uko
Mungu Ibariki Tanzania...
 
""mkuu Single D"

Uko Right Kabisa Hawa Watu Wanatuibia Kwa Kubadili Majina Ya Kampuni Huku Mmliki Yuleyule .....just For Breaking News Waheshimiwa Wa Celtel Wanabadilisha Jina Kuanzia July Wataitwa ""zein"" Kukimbia Kodi Hii Ndio Tanzania Tajirisha Kichwa Chako Utajiri Tosha Naona Watanzania Wanazidi Kuumia ,,,haya Tujipe Moyo......

...

Actually hii si kweli, kwa sababu Celtel wanabadili jina katika nchi zote za Afrika kutokana na kuwa imenunuliwa na kampuni ya kiarabu, baada ya Mo Ibrahim kuuza hisa zake. Tayari Uarabuni ipo brand hii ya Zain na wanataka iwe uniform all over the world.
Na jina sahihi ni ZAIN
 
Karamagi ang'olewa uenyekiti TICTS
Na Gladness Mboma

BODI ya Kampuni ya Kupakia na Kupakua Makontena Bandari ya Dar es Salaam (TICTS) imemng'oa madarakani aliyekuwa Mwenyekiti wake, Bw. Nazir Karamagi.

Bw. Karamagi ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), amefikwa na tukio hilo ndani ya kipindi cha miezi mitatu tangu alipojiuzulu wadhifa wake wa Waziri wa Nishati na Madini, kutokana na kashfa ya mkataba wa zabuni ya kufua umeme kati Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) na Kampuni ya Richmond.

Kutokana na mabadiliko hayo, Bodi hiyo sasa itaongozwa na Mkurugenzi wa Kundi la Hutchison Port (HPH) ambalo ni kampuni mama ya TICTS, Bw. John Maredith.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwakilishi wa Kampuni ya HPH kutoka Hong Kong, China, Bw. Neville Bissett, alisema uamuzi huo umetokana na mkutano uliofanyika Mei 8 mwaka huu.

Bw. Bissett alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu hatma ya hisa za Bw. Karamagi na hatua ya kuondolewa kwake kama inahusiana na tuhuma za ufisadi zinazomkabili, alisema hisa za Mwenyekiti huyo wa zamani ziko pale pale na kubainisha kwamba kuondolewa kwake hakuhusiani na tuhuma hizo.

Akizungumzia utendaji wa TICTS, Bw. Bissett, alisema anatiwa moyo na mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya menejimenti ya kampuni hiyo.

"Ujazo wa makontena ulikuwa wastani wa uniti 20 mwaka 2000 wakati mkataba unaanza, hadi mwaka jana ulifikia uniti 344,000. TICTS imefanikiwa kukuza biashara katika bandari ya Dar es Salaam, hivi sasa ukuaji huo umefikia asilimia 16 ikilinganishwa na asilimia nne tu kabla ya kuanza shughuli zake bandarini hapo," alisema Bw. Bissett.

Alisema mafanikio hayo yamepatikana mbali ya matatizo ya ufinyu wa nafasi unaoikabili bandari hiyo. Alisema tayari TICTS imewekeza dola milioni 21 za Marekani tangu kuanza kwa mkataba huo, kiasi ambacho kinakwenda mbali sana kikilinganishwa na mipango ya awali ya uwekezaji wakati ule wa ubinafsishaji ilivyokuwa.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. David Cotty, alisema tangu kuongezwa muda wa mkataba mwishoni mwa mwaka 2005, TICTS imejitahidi kukabiliana na uhaba wa nafasi bandarini hapo kwa kubomoa maghala yaliyokuwa hayafanyi kazi ili kupata nafasi zaidi.

Alisema wameingiza vifaa muhimu kwa kazi za upakuaji na upakiaji makontena na yote yamefanyika kutokana na kuongezwa muda wa mkataba

Bw. Cotty, alisema kiasi cha zaidi ya dola milioni 60 za Marekani kitawekezwa kwenye vifaa na upanuzi wa miundombinu katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Akizungumzia uendeshaji shughuli za bandari katika mazingira ya ufinyu na nafasi, alisema kwa mwaka jana, alisema licha ya kampuni hiyo kuwa na haki pekee kushughulikia meli zenye makontena, waliiruhusu Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kushughulikia meli zenye makontena kwa kuangalia matakwa ya wakati na idadi.

"Kwa sababu nafasi ilikuwa finyu kwa TICTS, lengo likiwa kupunguza msongamano...suala hili la nafasi linabaki kuwa gumu, msimu wa wingi wa makontena ukikaribia, kuna haja ya TICTS kupatiwa nafasi zaidi kwa ajili ya kuhifadhi makontena, pia hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa ili kuepuka makontena kuachwa bandarini zaidi ya muda wa mwisho uliowekwa," alisema Bw. Cotty.

Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo, Bw. Meredith alisema ameridhishwa na jinsi Serikali ilivyounga mkono kuongezwa mkataba wa TICTS na kwamba ni muhimu kwa maendeleo ya muda mrefu wa bandari hiyo.

Alisema TICTS imedhamiria kuendelea kujikita katika maendeleo ya kitengo cha makontena na kwamba jitihada zinalenga kuifanya Tanzania iwe na bandari yenye ufanisi zaidi katika Afrika Mashariki.

Bw. Meredith aliwataka wadau wote kufanya kazi kwa ufanisi na kuchukua hatua, ili kupata suluhu inayofaa katika kuwezesha ufanisi wa operesheni za bandari.

Juhudi za kumpata Bw. Karamagi kuzungumzia hatua hiyo hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kuzimwa muda wote gazeti hili lilipomtafuta jana.

Source: Majira
My take:
1. Hawa jamaa (TICTS na Karamagi) wameona Mtanzania ukimuwekea 'issue ya management' ya Wazungu tunakuwa mandondocha (NetGroup, Citywater, etc.)

2. Mwenyekiti mpya anasifia $erikali kuongeza muda wa mkataba na TICTS; Je, maadhimio ya Bunge hayatatekelezwa tena? Au anajaribu kushawishi muda ulioongezwa usipigwe pangwa?

3. Wana mpango wa kuwekeza dola millioni 60 ndani ya miaka mitano ijayo (janja ya nyani)! Kwani walikuwa wapi tangu wapate tenda takribani miaka nane iliyopita?

4. Ninanusa harufu ya mchezo mchafu na inabidi tuwe madhubuti. Wanafanya hivi tuogope, wakidhani tuko dhaifu kwenye masuala ya sheria hasa pale watapotishia kwenda mahakamani tutapokiuka amri ya Mkapa na Mramba.

4. Swali, wana nia njema hawa?? Walikuwa wapi kuboresha (au kutoa taarifa ya uboreshaji) mpaka baada ya wananchi kupiga kelele?
 
Lakini huyu ni shareholder mkubwa kwenye hili au?

anyway i just hope mambo haya hatuyarukii kusiasa siasa kwani baadae kuna hawa ma lawyers wasio na kazi wanaweza kuigeuzia serikali kibao kisha mkajikuta mnawalipa pesa nyingi kuli mlizotaka kusevu
 
5. Swali, wana nia njema hawa?? Walikuwa wapi kuboresha (au kutoa taarifa ya uboreshaji) mpaka baada ya wananchi kupiga kelele?
 
Dawa hapa ni kukoleza konchokoncho hata kama inawauma akina Pinda lakini iendelee tu hadi kieleweke bwana .
 
Karamagi ang’olewa TICTS

na Irene Mark

KAMPUNI ya kimataifa ya kupakua mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam (TICTS), ambayo iko hatarini kufutiwa mkataba wake wa miaka 15, imemuondoa katika uenyekiti wa bodi yake, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi.

Karamagi anakutwa na zahama hiyo ikiwa ni miezi miwili tangu alipolazimishwa kujiuzulu uwaziri huo, akihusishwa na kashfa ya ufisadi kwenye mkataba wa kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura wa Richmond.
Habari zaidi kutoka ndani ya TICTS zinaeleza kwamba, kuondolewa kwa Karamagi kumechukuliwa kama hatua mahususi ya kurejesha uhusiano imara kati ya kampuni hiyo na serikali.

Kwa mujibu wa habari hizo, mbali ya kuondolewa katika nafasi hiyo, tayari mazungumzo yameshaanza ndani ya TICTS ili kuangalia uwezekano wa kununua hisa zote za Karamagi ndani ya kampuni hiyo.

Baada ya kuondolewa kwake, nafasi hiyo ya Karamagi sasa imechukuliwa na Mkurugenzi wa Kundi la Hutchson Port Holdings (HPH), ambalo ni kampuni mama ya TICTS, John Meredith, tangu Mei 8, mwaka huu.
Katika mazungumzo ya Mwakilishi wa HPH kutoka Hongkong, Neville Bissett na waandishi wa habari yaliyofanyika Dar es Salaam jana, ilielezwa kwamba kuondolewa kwa Karamagi, kutatoa nafasi nzuri kwa uongozi mpya wa kampuni hiyo, inayolalamikiwa kwa ufanisi hafifu, kuzungumzia utata wa mkataba wa TICTS.

“Kampuni iliona ili iweze kuwasiliana vyema na serikali, hasa kuhusu utata uliojitokeza, ni bora haya mabadiliko (kuondolewa kwa Karamagi), yangekuwepo,” alisema Bissett baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi wa nyongeza ya miaka 15 ya mkataba kati ya kampuni yake na serikali, ulioibua mzozo ndani na nje ya Bunge, hivi karibuni.

Mwakilishi huyo alisema, tayari TICTS imewekeza dola za Marekani milioni 21 tangu kuanza kwa mkataba wake, kiasi ambacho ni zaidi ya mipango ya uwekezaji iliyomo katika mkataba wa ukodishwaji wa kitengo hicho.

“Tangu kuongezwa kwa muda wa mkataba mwishoni mwa mwaka 2005, TICTS imejitahidi kukabiliana na uhaba wa nafasi bandarini hapo kwa kubomoa maghala na kuingiza vitu muhimu kwa kazi ya upakuaji na upakiaji wa makontena kwa viwango vikubwa kazi ambayo isingeweza kufanyika bila kuongezewa mkataba,” alisema.

Hata hivyo, Bissette alibainisha kwamba, kiasi cha dola milioni 60 za Marekani zitawekezwa kwenye vifaa na upanuzi wa miundombinu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mwakilishi huyo alisema, Mwenyekiti mpya wa TICTS amefurahishwa kwa kuwa serikali imeunga mkono uongezwaji wa mkataba wake hadi mwaka 2025 kwa sababu ni muhimu kwa maendeleo ya muda mrefu.
“Meredith alitazama mustakabali wa kazi hii, akaonekana kufurahishwa na jinsi serikali ilivyounga mkono uongezwaji wa mkataba wake hadi mwaka 2025, kwa sababu ni muhimu kwa maendeleo ya muda mrefu ya bandari husika.

“TICTS imedhamiria kuleta maendeleo ya kitengo cha makontena jitihada zikilenga kuifanya Tanzania iwe bandari yenye ufanisi zaidi Afrika Mashariki,” alisema mwakilishi huyo kwa niaba ya mwenyekiti mpya ambaye hakuwepo wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Hivi karibuni, suala la kuongezwa kwa mkataba huo lilizua mtafaruku kiasi cha wabunge kuikalia kooni serikali na kusababisha Karamagi ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), kutakiwa kutoa maelezo kwa Spika wa Bunge kuhusu kauli zake ndani ya Bunge alipokuwa akitetea ongezeko la mkataba huo.

source: TanzaniaDaima
 
Hapa ni ujanja ujanja tu kumbe TICTS na wachina wamo du hii sasa balaa yaani wazee wa feki wamo....dah tumeliwa.Hapa dawa ni kuvunja mkataba tu jamaa waondoke tu.Wanataka kuwekeza hizo $60mil. toka hapo mwanzo walikuwa wapi??Kwa hiyo wameona mambo magumu ndo wanataka waanze kutupooza kishikaji hapo tusipo komaa hawa jamaa wataendelea kuwepo.
 
8a0ixqw.jpg
 
Msingahaike sana juu ya kumng'oa karamagi TICTS lemgo langu kuu nim kupumguza ,idomo ya wote wanaomfatafata sana karamagi ili niendelee na mambo yangu ok?
 
My take:
1. Hawa jamaa (TICTS na Karamagi) wameona Mtanzania ukimuwekea 'issue ya management' ya Wazungu tunakuwa mandondocha (NetGroup, Citywater, etc.)

2. Mwenyekiti mpya anasifia $erikali kuongeza muda wa mkataba na TICTS; Je, maadhimio ya Bunge hayatatekelezwa tena? Au anajaribu kushawishi muda ulioongezwa usipigwe pangwa?

3. Wana mpango wa kuwekeza dola millioni 60 ndani ya miaka mitano ijayo (janja ya nyani)! Kwani walikuwa wapi tangu wapate tenda takribani miaka nane iliyopita?

4. Ninanusa harufu ya mchezo mchafu na inabidi tuwe madhubuti. Wanafanya hivi tuogope, wakidhani tuko dhaifu kwenye masuala ya sheria hasa pale watapotishia kwenda mahakamani tutapokiuka amri ya Mkapa na Mramba.

4. Swali, wana nia njema hawa?? Walikuwa wapi kuboresha (au kutoa taarifa ya uboreshaji) mpaka baada ya wananchi kupiga kelele?

Good analysis John!
 
kuna Bao lingine ambalo linafungwa kiufundi na mafisadi,wanatumia njia mbadala na sijui nani kawafundisha.Yaani kama ikienda mpaka June bila ya chenge kushitakiwa basi ushahidi wote utakuwa umepotea.kuna mambo yanaendelea mpaka sasa

1.Fuatilia kwa ukaribu nini kinafanyika Kiwira Gold Mine kwa sasa
2.Suala la lakaramagi kutolewa na wazungu kutishia kununua hisa za karamagi amabzo ni 31%,bado kuna hisa za Rostam ambaoz ni nyingi tu.

Baada ya kuangalia kwa undani basi utagundu nini kinafanyika,Mie siko tayari kufungwa bao la kisigino tena na nitakuwa tayari kusema nachokijua kabla hawajashtuka
 
Hii aya mbona inaashiria kuna kitu cha siri na ujanja tu unaoendelea ktk huu mkataba?Another Vanity under the sun!

Ina maana lile bunge pamoja na kamati yake havina maana ktk yale waliyoshauri serikali?Pamoja na kutumia kodi za wananchi kutembelea bandarini na kupeleka maoni kwenye mjengo kule Dodoma bado ushauri unapigwa teke.Nini maana ya bunge la viwango na kasi?Udhalilishaji wa maoni ya wote wanoingia mjengoni mle.Au hizi ndo siri za mambo ya sirini ya baraza la Mawaziri zisemwazo kwenye viapo

"Mwakilishi huyo alisema, Mwenyekiti mpya wa TICTS amefurahishwa kwa kuwa serikali imeunga mkono uongezwaji wa mkataba wake hadi mwaka 2025 kwa sababu ni muhimu kwa maendeleo ya muda mrefu.
"Meredith alitazama mustakabali wa kazi hii, akaonekana kufurahishwa na jinsi serikali ilivyounga mkono uongezwaji wa mkataba wake hadi mwaka 2025, kwa sababu ni muhimu kwa maendeleo ya muda mrefu ya bandari husika".
 
Mie siko tayari kufungwa bao la kisigino tena na nitakuwa tayari kusema nachokijua kabla hawajashtuka
single D said:
Ina maana lile bunge pamoja na kamati yake havina maana ktk yale waliyoshauri serikali? Pamoja na kutumia kodi za wananchi kutembelea bandarini na kupeleka maoni kwenye mjengo kule Dodoma bado ushauri unapigwa teke.Nini maana ya bunge la viwango na kasi? Udhalilishaji wa maoni ya wote wanoingia mjengoni mle. Au hizi ndo siri za mambo ya sirini ya baraza la Mawaziri zisemwazo kwenye viapo
Gembe, Single D, ...mi nasubiri kuyaona ya FILAUNI; hakika hapa ndipo watapoona nguvu ya UMMA!

Gembe mwaga mambo tumkome. Fisadi ukimsubiri anakuwahi, wana nguvu za giza hawa -- hahahh!
 
Karamagi lazima ajutie kuingia kwenye siasa, mbio za sakafuni huishia ukingoni... sasa kuhusu TANGOLD mbona Wakurugenzi bado ni Balali, Chenge, Rutabanzibwa, Mgonja nadhani na Karamagi. Govt show your teeth here, this is worse than innocent Pemba elders.
 
Mkianza kusikia wafanya biashala wanasifia makontena yao kufika haraka na kuweza kuyaondoa bandalini ndani ya siku tatu basi ,tunaweza kushawishika kuwa mambo ni shwari ila ,kama bado wanapiga makelele kuwa hata kontena likifika dar basi linaweza kupitisha kama miezi sita hawajafanikiwa kuyaondoa hapo mjue kuna ulaji.Unatoa kontena China unalipata baada ya miezi sita ukiuliza unaambiwa kuna mengine yameshafikisha mwaka bado zamu ya kutolewa haijafika ,yaani bidhaa ikitoka inakuwa imeshapoteza soko.
 
Waungwana najua sasa hivi mambo ni mengi sana ya kujadili na ndio njia wanayotumia kila kukicha kuibua jambo jipya.

Ila naomba kuuliza, mtanisamehe kama nitakuwa nimepitwa na hili: HIVI YALE MAELEZO ALIYOAMBIWA KARAMAGI NA SPIKA ATOE KUHUSIANA NA TICTS NA MAAMUZI YA BARAZA LA MAWAZIRI YALIFIKIA WAPI? Any idea?
 
Back
Top Bottom