Tibaijuka ashushwa cheo UN

Masanja pole sana kwa kuumia kwamba mama Tiba alipeleka mradi Muleba. Ungefurahi asiupeleke uko na apeleke wapi?
Kama ni kweli alifanya hivyo basi alifanya kazi njema kwa jamii yake na kama tukipata watz wengi UN watakaojali nyumbani tuna haja ya kufurahia wadanganyika kwenda kwenye mashirika ya kimataifa.
Lakini kama tukipeleka watu wa aina yako Masanja UN basi tuna hasara ya kutupa na hatuna haja ya kufurahia uwepo wa watz kwenye anga za kimataifa.
Nimesikia si Muleba pekee alikokuwa anafanyia kazi project zake kwenda mbele lakini hata miji ya Bukoba kwa habari ya maji, na miji ya Dar, miji kadhaa Uganda na miji kadhaa Tz ikiwamo na Dar.
Mungu akupe nafasi nyingine mama Tiba. Dumu kusaidia watz ambao kwa hakika wamejaa ufisadi kila kona na hawafurahii juhudi zako.

Mchukia Ufisadi hivi wewe unachukia ufisadi kweli au wewe ndo FISADI nambari wani (wa mawazo)? Au husomi mitundiko ya watu unajiandikia tuu?

Katika mitundiko yangu yote..sijaongelea anything to do with Mradi wa Muleba or anywhere..After all mimi sijui anything in that territory..sasa wewe unakuja unalipuka hapa ndugu yangu..Tafadhali bana/bibi!

Soma kwanza uelewe mtu anachozungumza, ndipo uanze ku-finger point. No where nimeongelea mradi wa Muleba au popote pale.

Tuendelee na mjadala!
 
wandugu,

..sikilizine taarifa ya NTV iliyoletwa hapa. wanadai kuna ubadhirifu umetokea na uchunguzi unaendelea. pia Kenya walituma maombi Dr.Tibaijuka aondolewe ktk nafasi hiyo.

Jokaa Kuu, hilo la Kenya ingawa linawezekana lakini sidhani kama liko solid to merit discussion. Mama Tibaijuka amekaa Nairobi for almost ten years, inawezekana kweli NAIROBI waombe BAN Ki Moon kumuandoa akiwa amebakiza miaka less than miwili? Well inawezekana lakini nakuwa na mashaka.

Mimi naamini ukweli utafahamika, maana wenzetu wako very open. Ila mimi nimesikitika maana huyu mama..ikitokea akahusishwa na ufisadi ndani ya UN kwa nafasi kubwa kama ile (by the way ufisadi siyo kuiba pesa tuu hata kuajiri kwa undugunization, kutumia madaraka vibaya etc..ni ufisadi) litakuwa ni DOA kubwa sana katika maisha yake after UN service.
 
inasemekana kinachomtoa ni "undugunaizesheni" yaani wahaya wamejaa ofisi za nairobi hawana elimu za kutosha na kama mnavyowajua viburi vyao......
 
inasemekana kinachomtoa ni "undugunaizesheni" yaani wahaya wamejaa ofisi za nairobi hawana elimu za kutosha na kama mnavyowajua viburi vyao......

Mkuu lete ushahidi wa wafanyakazi hao wa UN....au ndio hao walioandamana...?
 
UN, World Bank, IMF, WTO and many other so called international organization ni full of non sense. The more i study kuhusu hizi international org, the more i hate them. Mwaka jana i got an offer kutoka ILO, but i decide not to take that direction.

Mama Tibaijuka can be more productive in Tanzania kuliko hapo UN. She need to come home and expose this fraud organization. Product za hizi non sense organization ndio Ndulu, matokeo yake ana believe on every benchmark kutoka IMF.
 
Haya mambo ni makubwa, BM siyo mjinga sana mpaka afanye hivyo kuna fyongo zinachezeka. Ila samahani sana kama nitakwua nimekosea, huyu mama nae alikuwa ni mtu wa maneno mengi na ushauri mzuri hakuwa na msaada wowote kwetu.

Ukipata ki cheo kama hiki usijisahau sana kuna watu wanaibuka wazuri who can do better and great job, ndicho kilichotokea.
 
Mi mwenyewe ni muhaya ila tumezidi kujidai na kujikweza sana. Hivi kweli kama makabila yote yangekuwa kama sisi ingekuwaje? sometimes tuwe reasonable siyo kuangalia upande mmoja. UN sasa hivi siyo sehemu ya kufanya kazi ili uwe exposed kwa kupata ajira sehemu nyingine, wewe utakuwa tu wa mule mule sana sana wanachokifanya ni kukutoa kitengo hiki kukupeleka kitengo kingine ufanye kazi kwa uzoefu na siyo ufanisi.

Nimefanya kazi for 5 years sasa naondoka kujiunga na kampuni nyingine ya kawaida inayonilipa kidogo ila nifanye kazi yangu kwa ufanisi, watu wakiona ile nembo ya UN wanaishia kukujudge eti una hela sana au umesoma kumbe ni zumbukuku la kawaida.
 
1. Hivi Steiner Mjerumani amekuwepo UNEP Nairobi kwa mda gani?

2. Halafu watu Waafrica wanaandamana eti kupinga..sasa hao yawezekana baadhi hata waliajiriwa kwa upendeleo!

Uungwana Moon angelisubiri hadi mda wake uishe kama tangu 2002 ni Chief wa UN Nairobi walishindwa nini kusubiri tena mwaka mmoja?

Arudi tu Bongo akigombea ubunge kule Kagera au hata Dar atapata na JK atampa Uwaziri! Kwani huyu mama ana kipaji na anajiamini!
 
May be ni ule mradi wa nyumba HABITAT aliopeleka Muleba kule kwake kwa upendeleo!

Hebu tuambiane..ni kigezo gani alitumia kupeleka ule mradi wa nyumba Muleba ktk wilaya zaidi ya 131 Tanzania?

HILI NALO NENO!nadhani mama AMEWAJIBISHWA!
 
Kupeleka mradi kwao sio jambo la kumsemea huyu mama, angalau yeye amekumbuka alikotoka kuliko wengine wanaopeleka nje ya nchi, pia msisahau "mcheza kwao hutunzwa", je watamtunza nini kama hukuwakumbuka? na kama hivi sasa akirudi kwao bado profile yake iko juu hata ubunge aweza kuukwaa, je kama angelikupa wewe Masanja wapi wapi ungelimtunza nini?

Pia, kumbukeni kila aliye na nafasi huanzia kwao, Msuya wakati akiwa Waziri kule Mwanga vipi, Mramba na ile barabara ya Rombo,Magufuri na barabara ya Mza- geita,Diallo na Community air,BWM na barabara ya Kilwa n.k

.
 
Jokaa Kuu, hilo la Kenya ingawa linawezekana lakini sidhani kama liko solid to merit discussion. Mama Tibaijuka amekaa Nairobi for almost ten years, inawezekana kweli NAIROBI waombe BAN Ki Moon kumuandoa akiwa amebakiza miaka less than miwili? Well inawezekana lakini nakuwa na mashaka.

Mimi naamini ukweli utafahamika, maana wenzetu wako very open. Ila mimi nimesikitika maana huyu mama..ikitokea akahusishwa na ufisadi ndani ya UN kwa nafasi kubwa kama ile (by the way ufisadi siyo kuiba pesa tuu hata kuajiri kwa undugunization, kutumia madaraka vibaya etc..ni ufisadi) litakuwa ni DOA kubwa sana katika maisha yake after UN service.

Pamoja na siasa ambazo zimo ndani ya hili swala la huyu prof.Kama walivyosema wengine, UN kuna politics za hali ya juu na hakuna taasis yenye mambo yasiyo wazi kama UN.Kwa nje inaonekana kuwa na uwazi, ukweli, uwajibikaji na kujali meritocrity.Yet the opposite is the case.Kwanza ile kukaa kwa karibia miaka 10 katika nafasi hiyo na katika kipindi chote cha Koffi Annan peke yake inatosha kumsukuma nje apishe mageuzi which is typical of UN.
Kuhusu ufisadi, hata huko nako hakuko immune... kumbukeni kashfa ya mtoto wa Koffi Annan na contracts za kiupendeleo wakati wa crisis ya vita vya Iraq the infamous oil-for food scam
 
Masanja said:
Jokaa Kuu, hilo la Kenya ingawa linawezekana lakini sidhani kama liko solid to merit discussion. Mama Tibaijuka amekaa Nairobi for almost ten years, inawezekana kweli NAIROBI waombe BAN Ki Moon kumuandoa akiwa amebakiza miaka less than miwili? Well inawezekana lakini nakuwa na mashaka.

Mimi naamini ukweli utafahamika, maana wenzetu wako very open. Ila mimi nimesikitika maana huyu mama..ikitokea akahusishwa na ufisadi ndani ya UN kwa nafasi kubwa kama ile (by the way ufisadi siyo kuiba pesa tuu hata kuajiri kwa undugunization, kutumia madaraka vibaya etc..ni ufisadi) litakuwa ni DOA kubwa sana katika maisha yake after UN service.

Masanja,

..inawezekana kuondolewa kwa Dr.Tibaijuka ni mabadiliko ya kawaida tu ambayo Ban Ki-Moon ameamua kuya-implement.

..mwandishi wa TV ya Kenya ndiyo anayesema serikali ya Kenya imeomba kufanyike mabadiliko ktk nafasi ya Director General wa UN offices in Nairobi. ombi hilo siyo la kumbadilisha DG wa UN-Habitat.

..sijui kwanini unataka tuzipuuze habari hizo. labda unataka tuamini NTV ni anti-Kenyan goverment, na wameamua kuipaka matope serikali ya nchi yao wenyewe.

..NTV, ambao wako on the ground in Nairobi, wanadai kwamba Mabalozi wa nchi za Kiafrika walioko Nairobi waliposikia fununu za mabadiliko hayo waliandika barua za kuyapinga.

..taarifa ya habari inadai zimeandikwa barua 3 kwenda kwa SG Ban Ki-Moon lakini zote hazijapata majibu. vilevile wanadai Dr.Tibaijuka hakupewa taarifa rasmi kuhusu mabadiliko haya!!!

..sintomtetea Dr.Tibaijuka kutokana ubadhirifu wa fedha kwasababu masuala hayo yametokea yeye akiwa mwangalizi wa ofisi za UN-Nairobi. pamoja na hayo, nimesoma kwamba mmoja kati ya watuhumiwa ni raia wa Kenya.

..wafanyakazi zaidi ya 100 wa UN waliamua kuandamana kukutetea kumtetea Dr.Tibaijuka. nadhani hiyo ni testimony ya uongozi na utendaji kazi wa mama huyu wa Kitanzania.

NB:

..Ban Ki-Moon inabidi aje na sababu nzito zinazojitosheleza kutetea uamuzi wake wa kumshusha cheo Prof.Anna Kajumulo Tibaijuka [PhD].
 
Kwa maoni yangu, kila mkuu ni lazima aje na watu wake hata kama wapambe wa waliomtangulia walifanya kazi nzuri.

Vilevile kuna tabia moja ambayo haitusaidii watanzania au waafrika wengi. Watanzania wengi wanatafuta kazi katika mashirika ya kimataifa hili wakae huko milele.

Kwa upande wa wenzetu wanafanya kazi kwa muda katika mashirika hayo na baadaye kurudi makwao au kutafuta kazi sehemu nyingine.

Kwa mfano wachumi wengi na wataalamu wengi wa mambo ya fedha katika nchi za latin America walifanya kazi IMF, World bank na sasa wanasaidia nchi zao kwa kuwa na wataalamu mahiri na wenye uzoefu wa kimataifa.

Kama mama ni mahiri kuna nafasi nyingi tu za kuziba bongo.
 
Zakumi,

..naungana na bandiko lako la hapo juu.

..hata mimi naamini baada ya ku-serve vipindi viwili Dr.Tibaijuka anapaswa kutafuta kazi sehemu nyingine.

..hivi SG wa UN si ana-serve a maximum of two terms? mama naye anapaswa kufuata mfano huo hata kama haumhusu.
 
Eti unasema nini? Do you really mean what your talking about? labda huko kwenu latin America lakini Tanzania! watakutupa nje tu. Na hasa kama wewe si mwana SISI M. Na mark you wengine hawapendi siasa na si vema kuwalazimisha kuingia huko.
Mi nakwambia hata akija hapa JMK hatampa nafasi yoyote. Labda kama atajikomba na kuwa young fisadi.
 
Mchukia Fisadi said:

Mchukia Fisadi,

..siyo lazima Dr.Tibaijuka apewe kazi na Raisi.

..kwa mtizamo wangu anaweza kuanzisha foundation ya kushughulika na masuala kama mazingira na elimu.

..vilevile institutions nyingi sana nje ya nchi zinaweza kuhitaji uzoefu wa Dr.Tibaijuka.
 
Eti unasema nini? Do you really mean what your talking about? labda huko kwenu latin America lakini Tanzania! watakutupa nje tu. Na hasa kama wewe si mwana SISI M. Na mark you wengine hawapendi siasa na si vema kuwalazimisha kuingia huko.
Mi nakwambia hata akija hapa JMK hatampa nafasi yoyote. Labda kama atajikomba na kuwa young fisadi.

Unaweza kusema unavyotaka. Lakini kuna nafasi alizopata kwa wanasiasa kumpa nafasi. Na hayo vilevile yanaweza kusemwa kwa kuhusiana na mama Migiro.
 
Zakumi,

..naungana na bandiko lako la hapo juu.

..hata mimi naamini baada ya ku-serve vipindi viwili Dr.Tibaijuka anapaswa kutafuta kazi sehemu nyingine.

..hivi SG wa UN si ana-serve a maximum of two terms? mama naye anapaswa kufuata mfano huo hata kama haumhusu.

Utamaduni huo kwetu haupo. Ndio maana watu wanakaa madarakani miaka 23 na wakiondoka wame-nullify mazuri yote waliyofanya.
 
Una uhakika gani kwamba JK hatompa nafasi kama alifanya kazi kwa ufanisi huko UN?

Hiyo ya kufanya kazi kwa ufanisi ni subjective observation kwa sababu kama ingekuwa hivyo asingekumbwa na demotion aliyopata.
 
Back
Top Bottom