Tiba ya kikombe haitibu - SERIKALI

Dk. Mponda alisema wagonjwa wa Ukimwi wanatakiwa kutumia dawa za kurefusha maisha (ARV). Waziri amenukuliwa vibaya, hakuna dawa za kurefusha maisha, ARV hupunguza makali ya kuzaliana kwa HIV-1 (viral replication).

Tangua mwanzo sisi wengine tulijua babu anapiga sanaa! Kwa kuwa Tanzania ni taifa la wajinga babu alipata promo badala ya kuwa jela.
 
Unasema usichojua, hospitali ngapi, chemists ngapi zinatoa dawa fake na kuishia kuua watu?!
Nonsense,kinaponya hakiponyi ni wangapiwameshaaenda na wamekufa au wako hai?? hatuna serikali tuna genge la majambazi.....
 
ninacholaumu ni babu kutoza jero. angetakiwa kutoza buku 5 au kumi tz tungekuwa na bilionea ndani ya two month. people hawakutakiwa kukurupuka. anyway wajinga tumewajua mpaka mawaziri vichwa maji.
 
Unajua suala la tiba bwana ni suala la kibinafsi..sasa wewe kama unaumwa utakuwa unasubiri serikali ndo ikuambie katibiwe pale..kwa hiyo waliokwenda kwa babu mimi siwalaumu ni matakwa yao binafsi..After all kama umeenda na umepona hivi hata serikali ikisema haitambui hiyo tiba wewe unaathirika nini??..Nadhani imefikia sasa watanzani wenyewe kuwa wadadisi sio tu kufuata mkumbo..oh mbona waziri fulani kafanya..oh mbona mbunge flani kafanya..''fanya unaloona lina manufaa kwako na iga pale unapoona juhudi zako zimeshindwa''

Hebu Mkuu, rudia kusoma jina la anayetoa madai hayo. HADJI MPONDA, ndiyo linasomeka hivyo. tangu mwanzo alikuwa negative sana na mawazo ya tiba ya babu, alizimwa kiaina tu baada ya kugundua bosi wake naye kanywa, akaingiza kichwa mvunguni na sasa anasemea huko tena kwa ustaarabu kidogo. Haji na jipya, mponda kila kilichosemwa na washika misalaba. Na sasa kapata nguvu baada ya Assemblies of God wamewaunga mkono kina Kakobe na Mwingira baada ya nao kukimbiwa na waumini wao.

Imani bila matendo imekufa. Mungu alishasema "Nijaribuni kwa namna hiyo muone kama sitawabariki" Suala la imani is a purely personal issue. Ndio maana hatuelewani katika kuabudu Mungu kwa sababu kuna watu wanaojidai wanamjua Mungu zaidi kuliko yeyote mwingine na ili uonekane unamjua Mungu ati ni lazima uongee lugha ya kwao watu hao, yaani wamezaa majina yenye kufuru kumdhihaki hata aliyewaumba. Utasikia wanajiita "kanisa la kiroho" kwani lingine ni la nini? Wengine wataitwa makafiri. Ole wenu mafarisayo ambao mnawatwisha watu mizigo mizito ambayo ninyi hamuigusi hata kwa ncha ya vidole vyenu!

Makelele hayo ndiyo tunayoyasikia kila siku kwa watu wanaompiga vita babu. Lakini cha moto wanakiona, maana kama Mungu amemkubali babu, binadamu yeyote hawezi kubadilisha upepo huo. Wivu wa kijinga ndio uliomgharimu ndugu yetu Kaini kwa Habili. Kwa nini binadamu hatujifunzi? Hata Yesu Kristo mwenyewe aliitwa majina mengi mabaya kwa sababu wabaya wake hawakutaka Jina la Yesu lisikike masikioni mwao likitenda mambo makuu. Misahafu yot inakataza kubaguana na kufanyiana hiana. Mtume Muhammad angetokea leo angeshangaa wafuasi wake kuwapiga vita watu wa imani tofauti wakati yeye mwenyewe alipigania kuhakikisha amani inatawala na upendo hata kwa watu anaotofautiana nao kiimani. Yesu Kristo naye akija leo atashangaa watu wamfuatao yeye wakianza kudhibitiana wakati yeye mwenyewe alikaa nao na kuwavuta wengi hata wasamaria kunywa maji yao (rejea pale kisimani alipomwomba yule mwanamke wa kisamaria).

Jamanieee, nimalize kwa kusema kuna watu kibao ninaowafahamu wamekwenda kwa babu na hali mbaya na sasa wanadunda ile mbaya mitaani. Nakubali pia wapo waliokwenda kwa babu na hawakupona. Lakini mwenye kuponya ni Mungu sio babu wala mzizi. Hata Yesu alipaka tope alilolikanda kwa mate yake na kumpaka kipofu akamwambia afungue macho, yakafunguka. Ingawa alikuwa na uwezo wa kusema neno tu na kipofu angeona. Wengine wameambiwa kaoge mtoni mara saba na wakapona ukoma. Wangekuwa wabishi kama Mponda wasingepona kamwe. Mungu anatumia njia nyingi kukujaribu imani yako kwake, unajuaje kwamba babu ni mtihani mmojawapo kwako juu ya ugonjwa ulio nao? Kuna maaskofu ambao bado ni wachanga sana kiroho hata hawawezi kuona siri zilizoko Patakatifu pa Patakatifu. Mungu anasema hivi: "Nitawabariki nitakaowabariki" (Rum 9:15). Mwenye masikio na asikie Neno hilo ambalo Bwana Mungu anawataka watu wote wajue.
 
Back
Top Bottom