Dkt. Mwakyembe: Nimekerwa sana na msimamo wa Jeshi la Polisi juu ya afya yangu

Paul Makonda

Member
Jul 8, 2011
97
186
Dk. Harrison G. Mwakyembe (Mb), NW-UJ

Dar es Salaam

18/02/2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Nimelazimika leo Jumamosi, tarehe 18 Februari, 2012 kutoa taarifa hii kwa vyombo vya habari kufuatia mkutano wa DCI Robert Manumba na waandishi wa habari jana (17/02/12) kuongelea, pamoja na mambo mengine, hali yangu ya afya na kuhitimisha, kienyejienyeji tu kuwa "sikunyweshwa sumu" ila naumwa tu ugonjwa wa ngozi bila kufafanua ugonjwa huo wa ngozi umesababishwa na nini!

Napenda nisisitize mapema kabisa kuwa msimamo huo wa Jeshi la Polisi umenikera sana katika hali niliyonayo ya ugonjwa, kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake unaoendelea hospitali ya Apollo nchini India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu; pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa "sikunyweshwa sumu" wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu;

na tatu kwa Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.

Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Februari, 2011 nilimwandikia barua IGP Said Mwema kumtaarifu kuhusu njama za kuondoa maisha yangu na ya viongozi wengine. Kwa kutambua kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania daima husisitiza kuletewa ushahidi kwanza ndipo lifanyekazi, nilihakikisha nimeainisha katika barua hiyo kila ushahidi nilioupata au kupewa.

(Utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kusubiri kuletewa ushahidi mezani, kama ambavyo mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani, haupo popote pale duniani (ila Tanzania tu) kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. Polisi wanachohitaji duniani kote ni kupata clue au tetesi tu.

Hiyo inatosha kufukua ushahidi wote unaohitajika). Pamoja na kujitahidi kuanika kila aina ya ushahidi niliokuwa nao, mambo manne yalijitokeza ambayo yalionyesha wazi kuwa Polisi hawakuwa na dhamira ya dhati ya kupeleleza suala hilo:

(i) Siku chache baada ya kumkabidhi IGP barua hiyo, nilitumiwa timu ya "wapelelezi" ofisini kwangu kuja kuchukua maelezo yangu ya ziada. Timu hiyo ilikuwa inaongozwa na ACP Mkumbo, afisa wa polisi ambaye wiki chache zilizokuwa zimepita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kumbambikizia madawa ya kulevya mtoto wa Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, suala ambalo mpaka leo hii uongozi wa Polisi umeshindwa kulitolea maelezo ya kuridhisha. Kwa msingi huo, nilikuwa nimeletewa mtuhumiwa wa rushwa/ ujambazi kuendesha uchunguzi wa watuhumiwa wengine wa ujambazi! Nikatambua mara moja kuwa zoezi zima lilikuwa la mzaha, tena mzaha mkubwa!

(ii) Wiki chache baada ya barua yangu kuwasilishwa kwa IGP na timu ya ACP Mkumbo "kuanza kazi", Jeshi la Polisi likachukua hatua ya kuwapongeza na kuwazawadia askari niliowatuhumu kushirikiana na majambazi! Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwa ujumbe tosha wa kunipuuza.

(iii) Hivi karibuni tuhuma za askari polisi kujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto na kuwagusa askari "wale wale" niliowatuhumu kwenye barua yangu, IGP alichukua hatua ya kuwahamishia mikoa mingine!

(iv) ili kunikatisha tamaa kabisa, barua yangu ya "siri" kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kama habari ambayo ilikebehi na kukanusha taarifa nzima niliyotoa, sijui kwa faida ya nani! Lakini huu ni mchezo wa kawaida kwa polisi kwani hivi karibuni Mhe. Waziri Samuel Sitta alipohojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ofisini kwake, wakiwa wawili tu, taarifa ya kikao hicho ikawa magazetini ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta! The integrity of the police force leadership is on the line.

Nimeelezea vizuri katika barua yangu kwa IGP kuwa kundi hilo la mauaji lilikuwa limeelekezwa kuniua kwa kutumia sumu, taarifa ambayo kwa karibu mwaka mzima Polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wenyewe. Sasa huu msukumo mpya wa Jeshi la Polisi kutaka kujua kama nilipewa sumu au la na kukurupuka kutoa tamko hata kabla ya kunichunguza nilivyo, kunihoji mimi na wasaidizi wangu ofisini na hata kuongea na mabingwa wa Kihindi wanaonifanyia uchunguzi, umetokea wapi?

Aidha napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matatibabu yangu au walisoma taarifa "nyingine", na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au "walisomewa"! Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa wandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukidhibiti/ kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi na bila aibu: "hakulishwa sumu", "hakulishwa sumu"!

Nimesoma darasa moja Kitivo cha Sheria Mlimani na DCI Manumba. Baadaye IGP Mwema alikuwa mwanafunzi wangu wa sheria Mlimani. Vigogo hawa wawili wa usalama wa raia nchini hawajanitendea haki, nao wanajua. Wanajua vilevile kuwa sitakaa kimya au kumung'unya maneno come what may pale ambapo haki inakanyagwa.

Tuendelee kuombeana afya na uhai ili kutendeane haki na vilevile tuitendee nchi yetu haki kwa kuvimalizia viporo vinavyokera vya Dowans, EPA, Kagoda n.k. kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Mungu Ibariki Tanzania.

======

Waraka wa siri wa Mwakyembe kulishwa sumu.

WARAKA wa siri ulioandikwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, umezidi kuibua mambo mapya. Waraka huo ulioripotiwa mara ya kwanza wiki iliyopita na gazeti hili na kueleza mbinu, mahala ambapo waziri huyo anaamini aliwekewa sumu kupitia sabuni na taulo vilivyowekwa ofisini kwake kwenye chumba cha kuoshea mikono, safari hii waraka huo unaendelea kwa kumtaja mhudumu aliyetumika kuweka vitu hivyo.

Kupitia waraka huo alioutoa kwa ndugu na rafiki zake wa karibu, Dk. Mwakyembe anasema mhudumu aliyetumika bila kujijua ni wa kike kutoka katika kijiji cha Ipinda, wilayani Kyela, mkoani Mbeya, ambaye alihamishiwa ofisini kwake. Inaelezwa kuwa mhudumu huyo aliletwa katika ofisi hiyo siku chache kabla ya siku ya kuweka sabuni na taulo jipya ofisini kwa waziri huyo.

"Nilipoona kuwa najikuna mfululizo mara baada ya kunawia sabuni hiyo, siku ya tatu nilikuwa na wazo la kupeleka vitu hivyo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, lakini nilipofika ofisini, vilikuwa vimeshatolewa," anasema Dk. Mwakyembe kupitia waraka huo. Dk. Mwakyembe ambaye yuko nchini India kwa awamu ya pili ya matibabu, anasema alianza kumuuliza maswali ya kina mhudumu huyo ili kujua kwa nini vifaa hivyo viliondolewa ghafla wakati alivitumia siku moja, hakufanikiwa kupata majibu ya kina.

Naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, anadai katika mazingira ya kutatanisha, tena ndani ya muda mfupi tangu alipoanza kuathirika baada ya kunawia sabuni na kujifutia taulo hilo, mhudumu huyo wa kike alifariki na kuzikwa kijijini kwao Ipinda. Tukio la kufariki ghafla kwa mhudumu huyo bila kuugua, limeacha maswali mengi sio tu kwa Dk. Mwakyembe, bali pia hata kwa rafiki zake wa karibu ambao wanaamini kwamba aliwekewa sumu.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kuhusiana na taarifa kwamba kuna mhudumu mmoja wa kike wa Dk. Mwakyembe alifariki zilithibitisha kuwa ni kweli.

Mmoja maafisa wa juu wa wizara hiyo, aliliambia Tanzania Daima Jumatano kwa sharti la kutotaja jina lake kuwa ni kweli mhudumu huyo aliyemtaja kwa jina moja la Sara Richard ambaye alikuwa akimsadia Naibu Waziri huyo alifariki Septemba 29, mwaka jana, na kuzikwa kijijini kwao Ipinda. "Ni kweli kuna mhudumu mmoja ofisini kwa Dk. Mwakyembe alifariki mwaka jana. Ila sijui aliugua ghafla au vipi hilo sijui; isipokuwa ni kweli kwamba mwaka jana tulimpoteza mtumishi mmoja na tulimsafirisha hadi kwao Mbeya," kilisema chanzo chetu cha habari.

Akihojiwa na gazeti hili kuzungumzia waraka huo na tukio hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, alisema hajauona na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wa kina kubaini ukweli wa jambo hili. Hadi sasa wingu zito limetanda kuhusu afya ya Dk. Mwakyembe. Wakati taarifa zisizo rasmi zikisema amepewa sumu, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI), Robert Manumba, amesema hajalishwa sumu.

Taarifa hiyo ya Manumba pia inatofautiana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Nahodha, aliyekaririwa jana akisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi na kuikana taarifa ya Manumba. Manumba naye kwa upande wake, jana alisema kuwa tayari ameshawasilisha faili kwa DPP kuhusu sakata la Dk. Mwakyembe ili afungue kesi dhidi ya watu wanaodaiwa kutoa taarifa potofu kwamba waziri huyo amelishwa sumu.

THE THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

HARRISON MWAKYEMBE

Ni usiku 2011, Jan 21

Kundi la watu saba wanaingia mkoani Songea mkoani Ruvuma wakitumia gari ya wizara ya ujenzi yenye namba STK 6868

Kuna wakati gari hii inabadili namba na kusomeka STK 6869.

The reason for replacing vehicle’s registration number is only known by passengers on board

Gari hii ambayo ni Land cruiser,Inawashushia abiria wale katika eneo liitwalo MADABA.

Baada ya kushuka, abiria wale wanaingia kwenye Land cruiser nyingine “Hard top” yenye usajili wa T 768 BDU.

Gari hii inawapeleka watu hawa hadi bar ya TOP ONE INN Songea mjini.

Abiria hawa ni kina nani?

Baina yao kuna

wasomali wawili ambao ni HAFIDH na FARAJ. Wasomali hawa waliingia nchini wakitokea nchini Kenya tarehe 8 Jan 2011. Walisafiri kwa barabara hadi Dodoma kwa kutumia gari aina ya Toyota Rav4 yenye usajili T 816 AQS.

Kijana mmoja wa Kichaga aitwaye Mustafa Mkusa aka Master. Inasemekana mtu huyu ni mtumishi wa Idara ya “wasiojulikana”

Mwingine aliitwa RAMIKA naye ni afisa kipenyo “hitman” from Tanga.

Watu hawa wanapokelewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea vijijini akiwa na mwenzake aliyejulika a kwa jina moja tu la MANYA.

Jumamosi kesho yake, yaani tarehe 22 January 2011 watu wale wakaelekea Mbunde wilaya ya Namtumbo wakiwa wameshabadili gani tena. Safari hii walitumia gari aina ya Defender likiendeshwa na ZUBERY KOMBA lenye namba ya usajili STK 2654.

Huko Mbunde hawaendi kufanya kitu kingine zaidi ya kwenda kwa “mlozi” aitwaye MAJUNGU. Mganga Majungu alikuwa akiishi kwenye mbuga ya wanyama ya Selous Game Reserve with Impunity. Nia ya kwenda kwa mganga huyu ilikuwa ni “kupikwa” kwa ajili ya kazi maalumu ambayo ilikuwa inawangojea.

Ile Defender iliwaacha na kugeuza mjini watu wale ambao walikaa kwa muda wa siku saba na wakarejea mjini tarehe 29 Jan 2011 na kesho yake wakaanza safari ya kurudi Dar es salaam.

My dear reader, sitaki kuwachosha kwa kuelezea safari ya watu hawa lakini kuna umuhimu mbeleni wa kuandika safari nzima ya watu hawa.

Watu hawa walisafiri mpaka Mafinga na kule wakakuta gari mbili zinawasubiri ambazo ni Hilux Mayai mali ya kampuni ya Vodacom na Defender iliyowasindikiza mpaka morogoro.

Morogoro walikuta aliyekuwa Manager wa Morogoro Hoteli aliyefahamika kwa jina la KARI akiwa ameshawafanyia booking ya malazi kwenye hoteli mbili tofauti ambazo ni Hillux Hotel na Top life. Aliyewapokea ni askari polisi aliyeitwa SABASITA.

Wakiwa Morogoro walitumia gari tofauti kwenye mizunguko yao. Magari hayo ni T 816 AQS (ile iliyowaingiza wasomali kutoka kenya), VX Land cruiser STK 1287, Mercedes Benz T 874 BDT na Toyota Mark II GX100 T 218 BKR

Pale Morogoro kikosi kiligawanyika ambapo watu wanne walienda Dar na kuwaacha wenzao Morogoro.

Walioondoka walitumia gari aina ya Nissan Patrol yenye namba T 845 ADH ya kampuni ya Capsian. Mmiliki wa kampuni hii ni ROSTAM AZIZ.

Haya niandikayo, nimeyatoa katika barua ambayo aliyekuwa mbuge wa Kyela na Naibu Waziri wa Ujenzi wakati ule ndugu HARRISON MWAKYEMBE, alimwandikia aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP SAID MWEMA akifichua mipango iliyokuwa imeandaliwa ya kumuua yeye na kuua baadhi ya viongozi wa kisiasa ndani na nje ya chama chake CCM.

Nanukuu baadhi ya maneno ya MWAKYEMBE katika barua ile;

“Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza,kutajwa kwa jina langu na fursa pekee niliyokuwanayo ya kujua kilichokuwa kinafanyika, kukanipa ari,nguvu na shahuku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi swala hili na ikibidi kuwataarifu wenzangu ili waelewe”

MWAKYEMBE akadai kuwa nia ya kwenda kwa Mganga Majungu ilikuwa ni kuwafanya waliohukumiwa kifo kuwa wapole kama kondoo mbele ya wauaji wao. Pia mganga yule aliwapa sharti la kutotumia silaha za moto katika kutekeleza mauaji yale.

Jijini Dar watu wale walifikia Kiwalani kwenye msikiti wa MALKAZ ambao juu yake una eneo la makazi. Wanatumia muda mwingi uwasiliana na Askari polisi kutoka Central aliyefahamika kwa jina moja tu la MASUHE

Tarehe 5 Feb 2011 kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la HASSAN akasafiri mpaka dodoma kwenda kusurvey nyumba aliyokuwa akiishi Dkt. MWAKYEMBE

Kesho yake Tarehe 6 Feb kilosi kile cha watoa roho kikaondoka Dar kwenda Dodoma saa 4 usiku kikitumia Toyota Land Cruiser T 360 AKU.

Siku tatu baadae yaani tarehe 9 Feb 2011 ndipo Dkt. Mwakyembe akamwandikia barua IGP kumtaarifu njama hizi huku akitaja walengwa wenzake kuwa ni Marehemu Reginald Mengi, Benard Membe, Ane Killango, Dkt. Slaa na Prof. Mark Mwandyosya.

Ingawa barua ile ya Mwakyembe kwenda kwa IGP ilikuwa ni ya SIRI lakini haikujulikana ilivuja vipi na kesho yake tu kuwekwa kwenye vyombo vya habari.

Ilikuwaje mpaka kufikia hapa?

Ikumbukwe kuwa Dkt. MWAKYEMBE alikuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya bunge iliyochunguza mkataba tata wa Richmond ambapo ripoti ya kamati hii ilimlazimu aliyekuwa waziri mkuu Fredrick Lowasa kujiuzulu.

Baada ya hapo ndipo Mwakyembe akaanza kuandamwa na msururu wa matukio,

Tarehe 21 May 2009 akapata ajali tata ya gari maeneo ya IHEMI mkoani Iringa majira ya saa 1 na dk 10 asubuhi.

MWAKYEMBE akielezezea ajali ile, alidai kuwa wakiwa njiani kuna lory lililokuwa linaenda kwa mwendo mdogo mbele yao,dereva wa MWAKYEMBE aliyeitwa Joseph Msuya akaliomba lory lile zaidi ya mara tatu liwaruhusu kuovertake lakini halikufanya hivyo na lilipoamua kuwaruhusu dereva akiwa hata hajamaliza kulipita tela la lory lile, nalo likaongeza mwendo dereva wa lory akashusha kioo cha gari lake kuwatazama vizuri kisha “akawapa body” ambapo gari la MWAKYEMBE likagongwa na kupinduka. Ni dereva wa MWAKYEMBE ndiye aliyemsaidia kwa kuomba msaada wa gari “kibabe” ili kumkimbiza hospitali Mwakyembe ambaye alikuwa amepoteza fahamu.

Sakata hili liliibua mkanganyiko ndani ya vyombo vya Serikali kwani Polisi na Tanroads walitofautiana kauli juu ya chanzo cha ajali ile hali iliyolazimu kuundwa tume ya uchunguzi.

Kama hiyo haitoshi, Mwaka 2011 mwishoni Dkt Mwakyembe akaanza kuugua ugonjwa wa ajabu wa ngozi.

Ngozi yake ilikuwa ikipukutika na kutoa unga huku nywele zake zikinyonyoka.

Baadaye ukaanza kuenea uvumi mitandaoni kuwa MWAKYEMBE alikuwa akiugua maradhi ambayo chanzo chake ni sumu. Uvumi huu ulieleza kwamba sumu ile iliwekwa katika kitambaa cha kujifutia alichopewa kwenye mkutano wa Waandisi na wasanifu uliofanyikia ukumbi wa Mlimani City. Uvumi huo ukataja hadi aina ya sumu kuwa ni Polonium 210.

Lakini Mwakyembe mwenyewe alizungumzia swala la sumu kwa kumuhusisha mtumishi wa Wizara yake(ujenzi) ambaye alihamishiwa pale Wizarani siku chache tu kabla Mwakyembe hajaanza kuugua maradhi yale.

Mwakyembe anadai mtumishi yule ambaye aliitwa SARA RICHARD ambaye ndiye alipelekwa kama msaidizi alitumiwa kwa kutokujua na kumwekea Mwakyembe Sabuni na taulo vinavyoaminika kuwa vilikuwa na sumu katika eneo la kunawia mikono ndani ya ofisi ya Mwakyembe.

Ni baada ya kutumia vitu vile Mwakyembe akaanza kuwashwa sana na alipohisi labda vitakuwa vile vifaa alivyotumia ofisini kwake ndio chanzo cha maradhi, akakuta vimeshaondolewa.

Namnukuu Mwakyembe;

“Nilipoona kuwa najikuna mfululizo mara baada ya kunawia sabuni hiyo, siku ya tatu nilikuwa na wazo la kupeleka vitu hivyo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, lakini nilipofika ofisini, vilikuwa vimeshatolewa,”

Dkt. Mwakyembe alianza kumuuliza maswali ya kina mhudumu huyo ili kujua kwa nini vifaa hivyo viliondolewa ghafla wakati alivitumia siku moja, hakufanikiwa kupata majibu ya kina.

Katika mazingira ya utata sana,Mhudumu yule alikufa ghafla bila kuugua siku chache tu baada ya Mwakyembe kumuhoji juu ya sabuni ile na akazikwa kwao Ipinda Kyela.

Kutokana na hili mashaka ya Mwakyembe yakathibitika kuwa haugui maradhi ya kawaida.

Swala hili la kulishwa sumu au kutolishwa, liliibua mvutano mkubwa baina ya aliyekuwa DCI ROBERT MANUMBA aliyekuwa akipinga madai hayo na SAMWEL SITA aliyekuwa anasisitiza swala la Sumu.

MWAKYEMBE kuna wakati aligeuka mbogo pale aliyekuwa DCI ROBERT MANUMBA alipotoa taarifa kwa waandishi wa habari kuwa MWAKYEMBE hakulishwa sumu na akasema anakusudia kuwashitaki wanaosambaza uvumi huo.

MWAKYEMBE akaandika waraka mrefu ufuatao kujibu kauli ya Manumba akiwa bado anaendelea na matibabu kwenye hospitali ya Apollo nchini India;

Dk. Harrison G. Mwakyembe (Mb), NW-UJ
Dar es Salaam
18/02/2012
 
haya mambo ya kufanya kazi na vyombo vya habari...................... sasa mwakyembe hapa anatafuta nini?................... huruma ya umma?.................... atulie tu aendelee na matibabu yake, ..................Mungu akipenda atamnusuru...............
 
Usalama wa taifa la tanzania mimi nashindwa kuelewa kama ni usalama wa taifa ama usalama wa genge la mafya ya ufisadi. DCI anatoa taarifa ya Ugonjwa wa mtu kama vile imeandaliwa na mtoto wa darasa la tano tena wa shule za kata. Hebu watanzania tuache mizaha. Haitatufikisha popote.
.
 
Dah!

Hii nchi kweli ni mafia hivi haya yanatokea kwa mbunge na naibu waziri tena msomi ss sie wananchi kajamba nani itakuaje?

Si ndo tunauliwa then ushahidi unapotezwa kabisa,mi ni mpenzi mkubwa sana wa kuangalia series za kijasusi nilidhani ni fiction yale matukio ya viongozi wanayafanya na kuficha ukweli kwa gharama yeyote ile na ukiingilia mambo yao wanakushughulikia balaa.

Hizi nguvu za umafia wanazipata wapi?

Pole sana kamanda wa Kyela haya mambo yana mwisho wake
 
haya mambo ya kufanya kazi na vyombo vya habari...................... sasa mwakyembe hapa anatafuta nini?................... huruma ya umma?.................... atulie tu aendelee na matibabu yake, ..................Mungu akipenda atamnusuru...............

Kwani wao polisi wamefanya kazi na yeye Mwakyembe! Mlango alopitia wao ndo anaopitia! Anza na Manumba na mwema ndo umshambulie Mwakyembe! Kweli kichani hamna akili!
 
Mwakyembe ni tatizo kubwa zaidi ya hao Polisi anaowatuhumu. Kumbe anayo taarifa ya awali ya ugonjwa wake, kama mwanasheria ameshindwa nini kuitisha uchunguzi binafsi wa jinai kuhusu tatizo lake?

Hata sasa baada ya Polisi kuonesha "udhaifu" katika uchunguzi wao, kwanini Mwakyembe asiombe msaada wa wataalamu wa nje waliobobea katika upelelezi wafanye uchunguzi upya? Anaogopa nini?

Siwapendi watu walalamishi, lakini huyu amenikera zaidi na ukiwa makini hata faida ya kuwa msomi haionekani!

...tunakoelekea sasa tutegemee kuiona ripoti ya ugonjwa wake kwenye magazeti, kitu ambacho si kizuri sana!
 
Pole sana Dr Mwakyembe, siku zote haki itatawala na dhuluma itasinyaa kwa aibu. Tumwombe Mungu akuimarishe kiafya.
 
Mtu yeyote mwenye busara hakurupuki tu. Hufikiri sana na kwa kina kabla ya kuonge lolote. Hakuna jibu sahihi la swali lako ama la kamuulize mwakyembe. We jadili anayoyasema na si vinginevyo otherwise utakuw ni walewale wa kutumwa
 
Hawa polisi hawapo makini na wanamasihala sana. Pole sana Dr. Mungu atakupigania na ipo siku watakusaluti
 
Back
Top Bottom