Blaki Womani
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 11,229
- 13,430
wanaJF nimewamiss sana
nimerudi safari ya kwenda kupata kikombe cha dawa kwa Babu anawasalimu sana nilipata angalau muda wa kuuliza swali
dawa inatibu magonjwa yote kama utakuwa na imani na pia wakati unakunywa unaweka ombi kwa ugonjwa unaokusumbua.
Safari ilikuwa nzuri na niliifurahia sana isipokuwa barabara mmmmmmmmmmmh
Napenda kusema kwamba tofauti na kwenda kwa Babu niliweza kufanya utalii wa ndani nimeweza kuona ziwa Natron likiwa limezungukwa na Flamingo pamoja na magadi nimeweza kuchukua na kuja nayo huku, pia nimeweza kuona Twiga, Pundamilia na zaidi niliweza kuona mlima wa OldonyoLengai kwa karibu nafikiri tunaukumbuka huu Mlima.
Maisha niliyoyakuta kule niliyafananisha na kile kipindi kilikuwa kikirusha na TBC1 kilikuwa kinaitwa MAISHA PLUS watu walikwenda Loliondo na majiko ya gesi, na wengine walitumia kuni zilizokuwepo pale pamoja na vyombo vya kupika na vyakula. Walikuwa wanakwenda kuchota maji mtoni wanapika kuosha vyombo na mambo mengine mabalimbali ilikuwa kama Picnic.
kwa sasa wingi wa watu umepungua kiasi
kwa yeyote anayetaka kwenda asiwe na wasiwasi wa foleni kubwa