Thread imenipeperushia mwali

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,949
4,444
Amini usiamini nikiwa Vekesheni nikakumbana na mrembo mmoja maeneo ya Mwanjerwa huku na huku ikabidi nimvute chemba kidogo katika maongezi ya hapa na pale story za mapenzi nikamtumbukizia JF akadai anaipata vizuri sana akawa ananitajia hadi members kama ZD, Nguli, MJ1, Nyamayao, Xpin, Kaizer, Geoff, Fidel, F1,bht, carmel na wengineo mm si nakamwambia mi ndo Fidel duh mtoto akabadilika yaani neno kujiexpress likawa ndo agenda ya kunikimbia akaniambia wewe si ulitangaza unastaafu kujiexpress mbona kama hujaacha na unarudia rudia kuliongelea? Jamani nikawa sina kauli nikamwambia ndo hivyo niamini kama huniamini waulize wapwaz dah mtoto akaondoka hivi hivi...ile thread ya kustaafu imenikimbizia mwali any way nahisi alikuwa mtoto wa geti kali au mboga saba yule.
 
DU!...
CHEKA UNENEPE!

Umeniacha hoi broda na hii ishu yako!

Lakini nawe ukumbuke ulionywa mno, kwanini husikii lakini?
Utakujakosa mwana na maji ya moto, na ujue wasichana wa Mbeya hawapendi kabisa mtu anayenaniliu,:eek:shauri yako.
 
Hahahaha mpwa lakini si nimeacha kwa mapenzi ya Mungu!
Yaani mtu kanikimbia hivi hivi ananiogopa kama ukoma mweh!
Na mpango vekesheni ijayo niende Arusha mpaka Babati
 
hahaaa mpwa kwisha habari yako/chali!!!! ndo malipo hayo mpaka yaishe siju lini (nachelea kusema na mda utakuwa umeenda) hahaaaa lol!!
 
Naombeni mnasafishe mbona EL wanamsafisha kanisani mm mnashindwa kunisafisha hapa jamvini jamani? Msaada wapwazi!
 
Amini usiamini nikiwa Vekesheni nikakumbana na mrembo mmoja maeneo ya Mwanjerwa huku na huku ikabidi nimvute chemba kidogo katika maongezi ya hapa na pale story za mapenzi nikamtumbukizia JF akadai anaipata vizuri sana akawa ananitajia hadi members kama ZD, Nguli, MJ1, Nyamayao, Xpin, Kaizer, Geoff, Fidel, F1,bht, carmel na wengineo mm si nakamwambia mi ndo Fidel duh mtoto akabadilika yaani neno kujiexpress likawa ndo agenda ya kunikimbia akaniambia wewe si ulitangaza unastaafu kujiexpress mbona kama hujaacha na unarudia rudia kuliongelea? Jamani nikawa sina kauli nikamwambia ndo hivyo niamini kama huniamini waulize wapwaz dah mtoto akaondoka hivi hivi...ile thread ya kustaafu imenikimbizia mwali any way nahisi alikuwa mtoto wa geti kali au mboga saba yule.

we vipi bana?!! ungetumia wini win method angekubali tu, jamaa yangu yuko mbeya anasema totoz za huko ni kama kumsukuma mlevi kwenye mtelemko!
 
Jamani nikawa sina kauli nikamwambia ndo hivyo niamini kama huniamini waulize wapwaz dah mtoto akaondoka hivi hivi...ile thread ya kustaafu imenikimbizia mwali any way nahisi alikuwa mtoto wa geti kali au mboga saba yule.
pole sana....ndege wako hayuko tena nawe...
 
we vipi bana?!! ungetumia wini win method angekubali tu, jamaa yangu yuko mbeya anasema totoz za huko ni kama kumsukuma mlevi kwenye mtelemko!

hehehe maharage ya Mbeya sio?
Lakini tatizo alisha jua kuwa mm ndo Fidel ikawa noma.
 
Jirani jifunze hivi!!,siku za mwanzoni usiwe wazi sana kwa Mpenzi mpya,unaweza kuwa mwizi/jambazi ukimwambia habari hizo mpenzi mpya anaweza ingia mtini,but ukisha zoeana naye unaweza mwambia habari kama hizo baada ya kujua kama anaweza tunza maneno unayomwambia!!!
 
Huu ushauri wa kiutuuzima, ahsante sana Sugar nadhani wengi wetu utatufaa huko mbele ya safari!!
 
Jirani jifunze hivi!!,siku za mwanzoni usiwe wazi sana kwa Mpenzi mpya,unaweza kuwa mwizi/jambazi ukimwambia habari hizo mpenzi mpya anaweza ingia mtini,but ukisha zoeana naye unaweza mwambia habari kama hizo baada ya kujua kama anaweza tunza maneno unayomwambia!!!
I will be happy if and only if what you wrote is what you mean!
 
Jirani jifunze hivi!!,siku za mwanzoni usiwe wazi sana kwa Mpenzi mpya,unaweza kuwa mwizi/jambazi ukimwambia habari hizo mpenzi mpya anaweza ingia mtini,but ukisha zoeana naye unaweza mwambia habari kama hizo baada ya kujua kama anaweza tunza maneno unayomwambia!!!

suga kwa maneno haya, ninauhakika umtamu! nimekaa nakutafakari binamu, siendi mbali maana wapwazi sijawajua vizuri na speed za akina Fidel80 sidhani kama dead balls kipa anazigusa. hamadi mipira ni kati tu! uzuri, jicho linaanza, sikio linafuata kisha mdomo-- jicho ni vebu sio nomino binamu.
amakweli ugeni kazi, hata sijui senks zinagongewa wapi.
 
Jirani jifunze hivi!!,siku za mwanzoni usiwe wazi sana kwa Mpenzi mpya!!!

Hapa jirani nimesha jifunza neno.
Kumbe n'tu ukiwa muwazi na kueleza fikra zako unakosa kifaa hivi hivi sasa naamini mbinu za uongo ndo nzuri kupatia vifaa.
 
Mbinu za uongo nazo pia sio rafiki,kuna mtu mwingine akigundua tu umemdanganya nayo pia inakua ni issue,kwa hiyo unatakiwa kuangalia pia yule unaeongea nae,ila kwa mara ya kwanza unapokutana na mtu jaribu kumsoma.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom