Nimesoma thread ya 'tgeofrey' yenye kichwa cha habari ' Prof.Chacahage na laana ya mauti/Mukandara soon' kwa mshangao mkubwa.Hivi kumbe kuna wanadamu wanaofurahia wenzao wakifa,haya ni mapya.Kwa wadau wa JamiiForums,'thread' hii ni ya aibu sana.Sisi wengi tulimheshimu sana Prof.Chachage kwa hoja zake nzuri ambazo zililenga kumtetea mtanzania wa kawaida,sasa wazo hili ni mchanga wa macho kwa watanzania walio wengi.Zaidi ya hayo ni kwamba huyu mtu ni marehemu, sasa kwa mila za kiafrika, marehemu hana haja ya kukosolewa hata kama alikuwa na makosa.Mwisho ni kwamba mbona wote tunakwenda huko huko,kuna haja gani ya kushabikia kifo cha mwenzetu?Kama fundisho kwa watu wa aina ya 'tgeofrey',naomba administration ya 'JamiiForums' imfungie kwa muda ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia zinazofanana na zake.