Thomas Sankara (1949-1987) - Muasisi wa taifa la Burkina Faso

"While Revolutionaries as individuals can be murdered, you cannot kill Ideas"

Mkuu hayo maneno aliyatamka baada ya wasaidizi wake waaminifu kumwambia kwamba rafiki yake mkubwa yaani Blaise Compaore anapanga kumpindua na kumuua ndipo kwa hali ya usshujaa kabisa akayatamka hayo na kuongeza kuwa kama Compaore ataamua kumuua hawezi kumzuia. Na kweli Compaore akamuua rafiki yake huyo shuujaa wa Africa. Nikikumbuka kifo hicho huwa nachukia madaraka ya kuongoza nchi kwani mtu unayemwamini anaweza kukugeuka. Hata sasa hayo tunayaona katika Africa yetu hii japo yanajificha kwenye vichaka vya demokrasia na hivyo si watu kuuana kwa mtutu bali kufanyiana njama za kumalizana kisiasa. Mungu amrehemu Capt. Thomas Isdore Sankara
 
Alikuwa kijana wa miaka isyozidi 33 tu, lakini aliwaka historia ya kudumu nchi kwake.

 
Last edited by a moderator:
Watu wa aina hii huwa wanaondolewa madarakani na kuuwawa ili lilinda western vested interest in Africa. Kumbuka akina Lumumba, Nkurumah, Gadaffi etc. Ni Mwalimu tu ndiye walimshindwa licha ya kutokea majaribio zaidi ya 8 YA KUTAKA KUPINDUA utawala wake....:hat:

Gaddafi hakuwa shujaa wa afrika wala mwanamapinduzi kutokana na historia yake
 
Ndugu wana JF, nchi yetu hapa ilipo imefikia hatua ambayo kusema kweli kwa kauli za majukwaani inaonekana ni nchi ya utawala wa sheria lakini kusema kweli rekodi za kauli hii zinatia shaka sana.

hali ya umasikini kwa watu wetu imekuwa ni mbaya kila kukicha, huku wananchi wakiendelea kuwa ni wenye subira .
Kinachosikitisha sana, ni kwamba wale tunaowapa dhamana, bila hiyana Wanafanya ufisadi, ambao kusema kweli Unatuathiri sana, Wanajiamnisha kwamba hakuna wa kuwagusa, mtandao wao ni mpana na ni mrefu.

Ni nani mtetezi wetu katika hali hii?- ni nani mzalendo wa kweli, mwenye uchungu na nchi hii?, ni nani anaumia kwa dhulma hii?.

Leo hii nchi inawekwa mfukoni na watu wachache, watu wachache tu!. halafu wenye dhamana wanahaha kuwakingia kifua. hii ni aibu kubwa, hali haiwezi kuendelea hivi hivi. Ni uzuzu kuendelea hivihivi.

Ni lazima Watanzania tufike mahali tuseme enough is enough. Ni lazima wananchi tuheshimiwe. Iwapo mafisdi hawa wanafikia hatua ya kuamni kwamba wao ni untouchables, halafu na sheria zinapindishwa kuwabeba Then kimbilio letu ni wapi?.

Tumeona ndugu zangu kuanzia suala la Wizi wa EPA, RADA, MEREMETA, na leo hii ESCROW- haya mambo yanapita hivihivi mbele ya macho yetu. hapana hii siyo sawa, siyo sawa hata kidogo.

Tunahitaji watu Wazalendo kutuongoza, Tunahitaji Watu kama Thomas Sankara, Wazalendo wa kweli, Watakaowaadabisha walevi wa madaraka na mafisadi.

Wananchi amkeni haki kujitafutia
Tutalala mpaka lini?, saa imeshawadia
Uongo ukataeni, waache kuwatania


Ni nani anayejali, adha za mtanzania
Yule aliye mkweli, moyoni anaumia?
Linamuuma jambo hili, kwa dhati anachukia?


Rushwa imekuwa ngao, kumdhulumu raia
ufisadi ni kama nguo, vazi la kujivunia
Hizi ndizo sera zao, hawana la kutwambia
basi hapo tuamkeni, haki kujitafutia


Mkipiga kura zenu, chagueni wenye nia
Waonesheni wanenu, muelekeo na njia

Simamieni haki zenu, iokoeni Tanzania!
 
Ripoti za mahakama nchini Burkina Faso zinasema kuwa mwili ambao unakisiwa kuwa wa raisi wa zamani aliyeuawa Thomas Sankara utafukuliwa hii leo katika jaribio la kutaka kubainisha ikiwa ni wake.

Familia na marafiki wa rais Sankara wamekuwa na shauku iwapo mabaki hayo ni yake, Bwana Sankara aliuawa wakati wa mapinduzi mwaka 1987. Sankara alichukuwa uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1983.

Sankara, alipinduliwa na Blaise Compaore ambaye aliitawala Burkina Faso hadi mwaka uliopita alipolazimishwa kuondoka na maandamano makubwa katika mji mkuu wa wa nchi hiyo Ouagadougou.

Madaktari wawili kutoka Burkina Faso na mmoja kutoka Ufaransa watachukua chembechembe za mwili huo na kuipima wakitumia mashine na mbinu za kisasa za DNA ilikubaini kikamilifu iwapo inahusiana na mwili wa Sankara. Miili mingine 12 ya wafuasi wake waliouawa pamoja naye pia itafukuliwa.

Mabaki hayo ya Sankara yamezikwa katika makaburi ya Dagnoen katika mji mkuu wa Ouagadougou, Familia yake inashuku kuwa huenda mwili huo sio wake.



Chanzo: BBC News


attachment.php


Authorities in Burkina Faso are exhuming the remains of former President Thomas Sankara and 12 of his colleagues, 28 years after they were killed during a 1987 coup.

Younger brother Paul Sankara said the exhumation will answer a number of key questions, including how Sankara was killed, who killed him, and where he is buried.

The body is believed to be buried in a cemetery in Ouagadougou, but the family said it hasn't seen the body since the assassination.

Sankara said, once these questions are answered, then those responsible for his brother's death will have to answer for it.

"The exhumation of the bodies is one part of the process. The most important thing is to define who, where and how Thomas was assassinated. The exhumations would be some evidence, proof, that indeed the remains of Thomas' body is in a given grave because no one in the large African family has seen the body of Thomas," he said

He said forensic might help in determining who assassinated his brother and, once that is determined, then the family will seek justice and reconciliation.

"First, we will find who assassinated him in October 1987, and where it occurred, how, and then somebody, or people, [will] have to respond to the justice. The DNA process through exhumation will help to get to the bottom. The whole point is to have truth, justice and, eventually, reconciliation. Without that, it won't be possible," he said.

He said the demand for justice for Sankara is being made not only by his biological or political family, but his entire African and global family.

"People in Africa and out of Africa have been working, supporting voluntarily the family to get this job done," he said.

Paul Sankara said he has no doubt that the interim administration in Burkina Faso is ready to prosecute anyone responsible for his brother's death.

He said the protests of 2014 that drove President Blaise Compaore out of power were motivated by the spirit of Thomas Sankara.

"By the way, people came because they wanted to know exactly what happened, the truth, the justice for Sankara's assassination. The second reason is the transitional government said many times it came to clean everything [up] and make Burkina Faso a democratic country," he said.

He said everything Thomas Sankara did as a leader was done with the people of Burkina Faso and the image of Africa in mind.

Source: voanews
 

Attachments

  • 28AFEDEF-8A27-4457-8CE4-3592B052259F_w640_r1_s.jpg
    28AFEDEF-8A27-4457-8CE4-3592B052259F_w640_r1_s.jpg
    15.3 KB · Views: 720
Ya Blaise Compaore na Thomas Sankara ni kama ya Mobutu na Patrice Lumumba
 
Kumbe kuna nyuzi ya mjomba Thomas N.I. Sankara Humu!?

Nimefurahi sana, rest in peace Captain..
 
Dah huyu jamaa alikuwa na ideas kama za nyerere.sa hivi afrika tuna makapi na vibaraka sio viongozi.
 
Mkuu AshaDii , Compaore na Sankara walikuwa marafiki. Compaore aliongoza mapinduzi na kumuingiza Sankara madarakani. Sankara akawa mzalendo kuliko walivyokuwa wakidhani wao kwamba ni kuingia Ikulu na kuanza kunyonya. Wanajeshi wenzake (akiwemo Compaore) wakamchukia ndio Compaore akaanda mapinduzi mengine ya kumuondoa Sankara na kukaa yeye. Of course Compaore was powerful in the army circles.

Kwa mambo aliyokuwa akiyafanya aliamini kuwa yuko sahihi na hakuna wakumpindua. Hata alipoambiwa kwamba Compaore anajiandaa kumpindua alipuuzia tu na kutoa hiyo kauli akiamini kwamba hata akifa ideas zake zitabaki na kweli zimebaki na mimi zinagonga kichwani mwangu kila kukicha. Natamani atokee mtu mmoja katika nchi yoyote ya Afrika awe kama Sankara. Hizo kwa sasa naona ni njozi!

Ila Sankara anabaki kwenye historia kama kiongozi mzalendo katika Afrika.
Je kwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli tunakaribia kumpata Sankara mwingine? Walimwingiza wakidhani wataendelea kunyonya, sasa anawashughulikia!
 
Nimefarijika sana baada ya kusikia kwamba Compaore anatakiwa akamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji ya Sa kara
 
dah hotuba za jamaa zimenitoa machozi,siku ndoto zangu za kuiongoza Tanzania zikitima nitakuwa kama sankara.please god help me one day yes!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom