SHERRIF ARPAIO
JF-Expert Member
- Aug 25, 2010
- 9,539
- 5,903
Mkuu SHERRIF ARPAIO kila nikiona hizi picha na maandiko yanayomhusu Thomas Sankara huwa machozi yananitoka na kisha kuwa na hasira zisizomithilika dhidi ya Balaise Compaore ambaye hadi sasa anaiongoza Burkina Faso.
Lakini pia huwa najipa moyo kwa kuwakumbuka wanamapinduzi wengine ambao waliingia madarakani hapa Afrika wakiwa na mioyo ya kizalendo lakini baaday ya kukaa madarakani kwa muda mrefu wakajisahau na kugeuka kuwa mabaradhuri.
Sijui kam Tom naye angegeuka ila yote kheri tu ni mpango wa Mungu kumleta, akafanya alichokifanya ambacho hadi leo kimebaki vichwani mwetu na kisha kumchukua.
Mbaya zaidi nasikia Blaise alilelewa na baba yake Sankara.
Sankara alinifurahisha alipomsemea hovyo mbele ya waandishi wa habari rais wa France wakati huo, Mitterrand kwa kitendo cha kumualika Peter Botha wakati huo wa Apartheid. Mitterrand aligeuka mwekundu kama steak!
Namkumbuka Sankara kwenye speech yake kule OAU alipowasemea hovyo viongozi wote wa Africa kuachana na kutegemea misaada "Bakuli"