Thomas Ngawaia: Zanzibar si nchi na Rais wa Zanzibar ni sawa na wa TFF!

G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
1,391
3,395
Niko naangalia kipindi cha uzalendo kinachorushwa na ITV ndg Thomas Ngawaia ambaye ni mkurugenzi wa taasis ya utawala bora amesema TZ ni nchi moja ktk katiba ya sasa. Na alipoulizwa juu ya uwepo wa rais wa Zanz akasema rais ni jina tu. Hata vyuo vikuu kuna rais na hata TFF kuna rais.
 
Hilo haliwashitui WaZenji wacha aseme Kiwete au Blackberry tuone ? WaZenji watasemaje mimi nimehusu Mtwara huko ndiko alipo bibi yangu ila hatuchanji tu.
 
Ngawaia arudishe misaada iliyopewa jimbo la Mpshi vijijini wakati akiwa Mbunge ndio aongee hiz habari.
 
sasa aangalie sherehe za muungano wiki ijayo ndio ataelewa vzr kama rais wa Zenj ni kama wa TFF au la. Kwenye hizo sherehe Jei Kei atashiriki tu kama rais wa chama cha netball tanzania (CHANETA)

Umenichekesha hatari unaweza ukanivunja mbavu lakn iyo ndo hali halisi kama hajui
 
Hizi kashfa za hii mijitu ya CCM Ndio maana Lipumba ameyaita Interahamwe...
Hapana hapana hapana hapana hapana walioko bungeni siyo ccm pekee wapo wakulima,wavuvi,wafugaji,watumishi wa mungu na vyama vya siasa visivyo na wabunge.
 
Hapana hapana hapana hapana hapana walioko bungeni siyo ccm pekee wapo wakulima,wavuvi,wafugaji,watumishi wa mungu na vyama vya siasa visivyo na wabunge.
Intarahamwe mna taabu sana, leo ndio mna jua kuna watumishi wa Mungu mbona mna matusi sana ......mkiongozwa na mama yenu Asha Baraka?
 
Mtoto Thomas,

Maneno ya watanganyika juu ya kwamba zanzibar si nchi tunayaona kama vile ni hayatiliki maanani

Kwanza kabisa wewe unaonekana hujijuwi nafsi yako, chukuwa somo godo hapa

1. mimi mzanzibari hata ikiwa wewe unaniona znz kuwa sio nchi na serikali yetu ni sawa na TFF sawa tu lakini mimi ninajuwa kwamba znz ni nchi na serikali ya smz ni halali inayopigiwa kura.

2. tatizo liko kwako wewe huna nchi, huna utaifa kwasababu tanzania sio utaifa, tz ni muungano wa mataifa 2 wewe lako umeliuwa sisi letu tunalipenda na kulifagilia. wewe mjomba ni refugee tu ndani ya nchi yako, ikiwa una nchi wewe niambie ni nani raisi wako?
 
Jumuiya ya wazazi CCM itakufa kwa aina ya viongozi hawa ....huku Lemutuz ....kule Ngawaiya ........Mbele Asha Bakari........
 
sasa aangalie sherehe za muungano wiki ijayo ndio ataelewa vzr kama rais wa Zenj ni kama wa TFF au la. Kwenye hizo sherehe Jei Kei atashiriki tu kama rais wa chama cha netball tanzania (CHANETA)
Thank you for this useful Post.....!!
Sasa ngoja nikatafute mdudu na ngumu nyeusi baada ya kazi ngumu ya siku ya leo.
 
Hapana hapana hapana hapana hapana walioko bungeni siyo ccm pekee wapo wakulima,wavuvi,wafugaji,watumishi wa mungu na vyama vya siasa visivyo na wabunge.
Waliopo bungeni ni CCM pamoja na mikia yao 201.
Hutaki unajinyonga!!
 
Back
Top Bottom