This Sunday LIVE on Star TV 19th DEC

Yahya asante sana kwa kuyatoa maoni yangu hewani. Bahati mbaya hayakupata michango sana tokana na kukatika kwa mawasiliano ya Dar. Lakini naona umedhamilia kusaidia katika kuyaunganisha mawazo ya watanzania juu ya msatakabali wa nchi yao. Na hakuna namna nyingine sasa mbali na nyinyi waandishi wa habari kutusaidia. Bahati mbaya tulidhani wawakilishi wetu (wabunge) wangebeba jukumu hili lakini badala yake wanapofika kule Dodoma wao upeleka mambo ambayo hatukuyachangia mawazo. Fikra zao wengi ni je nitarudije tena bungeni baada ya miaka mitano na malalamiko kuwa kuna watu wanawaingilia kwenye majimbo yao. Mungu akubariki sana. Tuendelee na tusiache kwa namna yoyote kushirikiana kuijenga na kuiendeleza nchi yetu.

Jambo moja la ziada bwana Yahya, ningeomba kama utaweza hizi video ya mada hizi ungeweza kuziweka hapa na kule Youtube ili wale wenzetu walio nje ya nchi wasioweza kuiona star tv wajue nini kimekuwa kikiendelea katika michango ya haya mambo na waweze kujua na kuyatolea maoni pia.
 
Yahya M.

Asante sana kurusha maoni yangu na watanzania wengine, hayo ni maoni ya watanzania tuliochoka kuburuzwa, hata kama mzee wetu alikosa moral authority kujitambulisha kuwa yeye ni msekwa na kusema yeye ni mjuni goerge, sasa kwa taarifa yake labda tumwambie tu kwamba mpango wa kuzuia katiba mpya utaifikisha nchi pabaya, maoni tunayotoa ni maoni ya wengi na ndio ukweli huwezi na maendeleo kwa katiba kandamizi kama ya sasa -inayoua demokrasia na kubariki uchakachuaji, tunamwomba mzee agundue zama zao zimekwisha sasa tupo damu changa kabisa na kibaya zaidi wazee wengi wa rika lake wanabariki madai yetu kama anabisha akamuulize shivji au lwaitama -sio kudanganya identity wakati tunajua sauti yake-mzee tunampenda na tunaheshimu lakini ajue change is inevitable either akubali change ama atalazimishwa kuchange.
 
Yahya m.
Asante kwa mjadala wa leo, mzee wetu msekwa alikosa ushujaa alipopiga simu kuchangia-lakini lazima atambue kuwa maoni yetu ni ya watanzania. Lakini pia atambue kuwa katiba kandamizi imefikia tamati. Pia atambue kuwa chnge is inevitable kwahiyo yeye na wenzake wanaojaribu kucapitalize kwa watanzania wajinga -mpango wao hautafanikiwa tutatembea nyumba kwa nyumba tanganyika nzima kutoa elimu ya uraia -lakini pia tutasema ukweli siku zote kwa maendeleo ya nchi hii. Mwisho wa uchakachuaji umefika, muda wa kuanika maovu yao umefika na mwanzo wa serikali ya watanzania umefika-tunampenda mzee na tunamheshimu lakini ajue kama amefunga masikio watanzania tupo kwenye harakati za uhuru. Big up star tv
 
napenda kujua kipindi hiki kitaanza saa gapi? Naomba kujuzwa waungwana.
Kila jumapili saa 1.30 asubuhi ndipo kinaanza. Ila maoni haya tunayochangia hapa ni ya kipindi ambacho tayari kilisha pita. Subiri jumapili asubuhi na wahi mapema kuamka na enjoy our contributions with other Tanzanians. Tembelea hapa JF ili ujue ni mada gani itaendelea end of week maana huwa wanaisema mapema.
 
Back
Top Bottom