This is University of Dar es Salam bwana,its challenges towards brighter education!

Calnde

JF-Expert Member
Oct 7, 2008
1,373
277
No one doubt over importance of UDSM in biulding this nation,neither do I.Nowdays there are going stories around overt this university which some of them are true though many are exaggerated.
Hata hivyo still management under Mukandala imeprove failure to large extent.

1 Ulinzi kwa wanafunzi hasa wale international imekuwa issue.Siku za karibuni wamekuwa wakivamiwa mno.Pale wapo wanaoitwa auxilliary police though kwa kweli presence yao naweza kuifananisha as too ceremonial.Hawana dhana za kuwasaidia kiasi kwamba vibaka wanawazidi nguvu!

2 Maji yamekuwa yakikatika bila taarifa maalumu kwa siku nzima hasa ukizingatia kuwa Dar hii joto ndo nyumbani kwake!

3 Uongozi wa DARUSO umeingiliwa na management kiasi kwamba ni kama vile haupo!Imagine juzi umefanyika uchaguzi watu 1000 tuu over over 15,000 peple ndo wamevote!

4 Miundo mbinu ni mibovu mno kiasi kwamba haiwezi kukidhi namba kubwa ya watu.Katika hili malazi yamekuwa issue kiasi kwamba kitanda cha mtu mmoja wanalala wawili.Hapa waderns ndo wanapatia ulaji maana first year wana wanaporipot after two weeks kama hawajalipia fedha za chumba wanauza tena kwa bei ya juu mno!
Changamoto ni nyingi mno though kwa ufundishaji walimu wanajitahidi sana,this is call kwa wapenda elimu wote kutoa special attention ili kukinisuru hichi chuo.TOGETHER WE REACH THERE!
 
Kuna ripoti iliwahi kutoka kwa wataalamu wa chuo cha ardhi kuwa yale mahall yanazidiwa na idadi ya watu na maafa yanaweza kutokea....hii inasababishwa na wanafunzi kubebana kitanda kimoja 2.

Halafu sidhani kama kuna crisis plan ikiwa umetokea moto itakuwaje maana sijawahi kusikia hata imefanyika drill ni kama vile wanaishi kwa kudra za mwenyezi MUNGU. Tusubiri janga then Raisi ataunda tume na kutoa ubani, mkuu wa chuo atajiuzulu, wanafunzi wataandamana, wazazi watafungua kesi ya madai kwa waliofariki, waziri wa elimu hatajiuzulu, wanazuoni watazungumza then after 2-3 years tutasahau na kurudi kwenye tatizo tena, Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.
 
Siku ikitokea moto au yale majengo mabovu kuanguka itakua ni hatari sana,maana hakuna utaratibu mzuri wa usalama pale.Wanafunzi wana survive kwa kudra za mnyazi Mungu maana mazingira yale hayastahili kuishi binadamu.
 
Miaka ya 1997-??? kulikuwa na project ya kuboresha chuo interms of infrastructure na nakumbuka wakati huo Prof. Mbwete ndiye aliyekuwa Project Manager... Kuna mwenye habari zozote kuhusu hatima ya huu mradi? And I remember this was to run together with Mlimani City project!!!
 
Mlimani city kwa sasa ni city kwelikweli but chuo kimezidi kuzeeka.Kuna mahall utadhani ni ngome walizotumia babu zetu kupambana enzi ya mkoloni!
 
No one doubt over importance of UDSM in biulding this nation,neither do I.Nowdays there are going stories around overt this university which some of them are true though many are exaggerated.
Hata hivyo still management under Mukandala imeprove failure to large extent.

1 Ulinzi kwa wanafunzi hasa wale international imekuwa issue.Siku za karibuni wamekuwa wakivamiwa mno.Pale wapo wanaoitwa auxilliary police though kwa kweli presence yao naweza kuifananisha as too ceremonial.Hawana dhana za kuwasaidia kiasi kwamba vibaka wanawazidi nguvu!

2 Maji yamekuwa yakikatika bila taarifa maalumu kwa siku nzima hasa ukizingatia kuwa Dar hii joto ndo nyumbani kwake!

3 Uongozi wa DARUSO umeingiliwa na management kiasi kwamba ni kama vile haupo!Imagine juzi umefanyika uchaguzi watu 1000 tuu over over 15,000 peple ndo wamevote!

4 Miundo mbinu ni mibovu mno kiasi kwamba haiwezi kukidhi namba kubwa ya watu.Katika hili malazi yamekuwa issue kiasi kwamba kitanda cha mtu mmoja wanalala wawili.Hapa waderns ndo wanapatia ulaji maana first year wana wanaporipot after two weeks kama hawajalipia fedha za chumba wanauza tena kwa bei ya juu mno!
Changamoto ni nyingi mno though kwa ufundishaji walimu wanajitahidi sana,this is call kwa wapenda elimu wote kutoa special attention ili kukinisuru hichi chuo.TOGETHER WE REACH THERE!

Huyu ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu anaandika hivi? Kama ni hivyo tuna matatizo mengi makubwa zaidi ya yaliyotajwa hapo.
 
Kama level yetu ya mwanafunzi wa UDSM kujieleza ndiyo hiyo, tatizo hili ni kubwa kuliko yote yaliyoelezwa.
 
Ulitaka wajielezeje?

Kwenye haya majumuisho, unasupportive indicators au ndo vile..kuosha kinywa?
 
Wewe unaona presentation iliyyotumiwa hapo, kuanzia spelling, lugha, tense, redundancy and all ni ya level ya Chuo Kikuu?

Mtu anayeshindwa kujieleza kwa ufasaha - kuandika kwa level ya chini ya ile inayotakiwa shule ya msingi- ananipa mashaka kama kweli anajua alichoandika.

Halafu anashindwa kujiudhuru kwamba hajui kiingereza, na kuamua kutumia Kiswahili, ambacho nacho probably hakijui vizuri lakini angekuwa na afadhali- sijui ni katika kujitutumua kujionyesha nshomile?

I could dissect the post and find many problems that would worry me more than the problems identified in the content of the post.

Fundamentally speaking, he described resources and logistics problems, which can easily be tackled with funds - hata Watanzania wenye uwezo wakiamua kuchanga kujenga mabweni na ku supply maji wanaweza kufanya hivyo- tatizo kubwa kuliko hilo ni kwamba huyu kijana wa Chuo Kikuu anaandika katika lugha iliyo katika level ya mtoto wa darasa la tano, tena siyo yule mjuzi kabisa kati ya hao basi.Huyu mtu mwingine anaweza kusema muda wake wa kumsaidia unaweza kuwa umepita.

Na kafika Chuo Kikuu.

No wonder tuna Vikwete, wametoka hapo hapo.Halafu leo tunashangaa tuna rais mchumi lakini "kilaza".
 
Kama level yetu ya mwanafunzi wa UDSM kujieleza ndiyo hiyo, tatizo hili ni kubwa kuliko yote yaliyoelezwa.

Unaweza kuwa na hoja ya msingi kuhusu mapungufu ya maelezo ya Calnde. Lakini kama wewe hutaweka maelezo jinsi unavyoona yangetakiwa kuwa, basi hauna sababu ya kumkosoa mtu ambaye walau ametupa mwangaza, japo, kwa mujibu wa maelezo yako, hajaweka kikamilifu. Better something than nothing!
 
Wewe unaona presentation iliyyotumiwa hapo, kuanzia spelling, lugha, tense, redundancy and all ni ya level ya Chuo Kikuu?

Mtu anayeshindwa kujieleza kwa ufasaha - kuandika kwa level ya chini ya ile inayotakiwa shule ya msingi- ananipa mashaka kama kweli anajua alichoandika.

Halafu anashindwa kujiudhuru kwamba hajui kiingereza, na kuamua kutumia Kiswahili, ambacho nacho probably hakijui vizuri lakini angekuwa na afadhali- sijui ni katika kujitutumua kujionyesha nshomile?

I could dissect the post and find many problems that would worry me more than the problems identified in the content of the post.

Fundamentally speaking, he described resources and logistics problems, which can easily be tackled with funds - hata Watanzania wenye uwezo wakiamua kuchanga kujenga mabweni na ku supply maji wanaweza kufanya hivyo- tatizo kubwa kuliko hilo ni kwamba huyu kijana wa Chuo Kikuu anaandika katika lugha iliyo katika level ya mtoto wa darasa la tano, tena siyo yule mjuzi kabisa kati ya hao basi.Huyu mtu mwingine anaweza kusema muda wake wa kumsaidia unaweza kuwa umepita.

Na kafika Chuo Kikuu.

No wonder tuna Vikwete, wametoka hapo hapo.Halafu leo tunashangaa tuna rais mchumi lakini "kilaza".

Wewe kipanga umeifanyia nini nchi yako?
 
This is outrageously stupid..

Mtu anaelezea matatizo ya UDSM, halaf mwingine anajifanya mwalimu wa kufundisha essay!

Naomba niishie hapa, kuna watu wanaboa sana hapa JF..
 
This is outrageously stupid..

Mtu anaelezea matatizo ya UDSM, halaf mwingine anajifanya mwalimu wa kufundisha essay!

Naomba niishie hapa, kuna watu wanaboa sana hapa JF..

Nilikuwa nazungumza na rafiki yangu mmoja hivi karibuni, juu ya kwa nini Watanzania walikuwa hawana outrage kutokana na matamshi ya Waziri wetu wa Mambo ya nchi za Nje Bw. Membe ambaye kimsingi alituambia wazi kuwa nchi yetu ni sawa sawia kuwa malaya wa kisiasa ili mradi tunapewa pesa.

Tukazungumzia tabia yetu ya kuangalia na kuyapa umuhimu mambo ambayo yanatutatiza immediately tu, na kuacha matatizo ya msingi katika fikira na falsafa yetu nzima ya maisha.Kamba ukitaka watu wawe na outrage na Kikwete, basi sema wananchi huko Mara wana njaa, wanapika majani na maembe mabichi, basi kila mtu atakuja kumtukana Kikwete hata kama kwa kweli tatizo ni la serikali ya kijiji.

Lakini Membe akikosea fundamentally kifalsafa na kuwatukana Watanzania wote, pamoja na kutoa msimamo wa kimalaya unaotukashifu kama taifa, hatuna muda wa kumshurutisha arekebishe kauli yake, ingawa kufikiri hivi ndiko kunakotufanya tuwe na matatizo haya tunayoyaona yako immediate.

Sasa kama wewe unaona huyu mwanafunzi tatizo lake kuwa ni hizo logistic resources, basi mwache a graduate na kuwa engineer, au mwalimu au rais, hapo ndipo utaona matatizo.

In a way tunaona matatizo haya kwa hao kina Kikwete na Membe na administations zinazoendeshwa kishaghala baghala. Kwa hiyo tatizo kubwa linalosababisha haya mengine yote ni uongozi mbovu, ambao kwa kiasi kikubwa unaletwa na elimu duni.

kwa hiyo, katika kujaribu kusaidia matatizo ya maji na logistics nyingine pale UDSM, ukitengeneza mfumo wa maji na kujenga mabweni peke yake utakuwa umesaidia no doubt, lakini utakuwa umesaidia kufunika symptom, na wala si ugonjwa.Ni kama nyumba yenye uvundo wewe unapaka marashi, ni kweli marashi yatasaidia kuondoa harufu kwa muda, lakini baada ya nguvu ya marashi kuisha uvundo utanuka tena vile vile, tena pengine maradufu.

Tunachotakiwa kufanya ni kusafisha uvundo na kuutoa kabisa ili usinuke, hapo ukipaka marashi sawia.

Niletee mwanafunzi wa chuo kikuu anayejua kujieleza, nitamuelewa vizuri, nitaweza kujadiliana naye vizuri, tutapanga mikakati vizuri, atakwenda kutumikia taifa vizuri zaidi, atajiamini vizuri zaidi hata kwenye nyanja za kimataifa, atatuletea fumbuzi zenye tija zaidi.

Huyu ambaye anashindwa kuieleza napata mashaka kwamba hata anachokieleza ndicho anachotaka kueleza.

Sorry, did not mean to come off as lofty and "high and mighty", lakini kwangu mimi muandishi ame violate mambo muhimu katika kujieleza kiasi cha kusikitisha, hususan kwa mwanafunzi wa chuo kikuu.

Ningeweza kumsamehe kama angekuwa form one "nyuka" ambaye alikuwa na somo moja tu la kiingereza katika shule ya msingi, lakini Chuo Kikuu? Anshindwa kujieleza? Halafu hata hajui hilo, anashindwa kuandika Kikswahili kuficha aibu yake?
 
Pundit, kama umekaa nje ya tz miaka mingi,ndiyo hali ya kiingereza kwenye vyuo vyetu, mnaobisha msibishe ukweli. Watanzania wengi kujieleza kwa kiingereza ni tatizo. Nimesoma Tanzania najua, na huku nilipo nakumbushwa kila siku na waafrika wenzangu ambao wanasema tz tunajua kiswahili tu. Wenye watoto hakikisheni mnawafundisha watoto wenu nyumbani, kusoma kwenye english medium schools siku hizi sio jawabu kuna usanii kama ulivyo kwenye sekta nyingine
 
Wewe unaona presentation iliyyotumiwa hapo, kuanzia spelling, lugha, tense, redundancy and all ni ya level ya Chuo Kikuu?

Mtu anayeshindwa kujieleza kwa ufasaha - kuandika kwa level ya chini ya ile inayotakiwa shule ya msingi- ananipa mashaka kama kweli anajua alichoandika.

Halafu anashindwa kujiudhuru kwamba hajui kiingereza, na kuamua kutumia Kiswahili, ambacho nacho probably hakijui vizuri lakini angekuwa na afadhali- sijui ni katika kujitutumua kujionyesha nshomile?

I could dissect the post and find many problems that would worry me more than the problems identified in the content of the post.

Fundamentally speaking, he described resources and logistics problems, which can easily be tackled with funds - hata Watanzania wenye uwezo wakiamua kuchanga kujenga mabweni na ku supply maji wanaweza kufanya hivyo- tatizo kubwa kuliko hilo ni kwamba huyu kijana wa Chuo Kikuu anaandika katika lugha iliyo katika level ya mtoto wa darasa la tano, tena siyo yule mjuzi kabisa kati ya hao basi.Huyu mtu mwingine anaweza kusema muda wake wa kumsaidia unaweza kuwa umepita.

Na kafika Chuo Kikuu.

No wonder tuna Vikwete, wametoka hapo hapo.Halafu leo tunashangaa tuna rais mchumi lakini "kilaza".

Sijaona tatizo ktk uwakilishaji wa hoja wa kijana wa Chuo ila naona tatizo liko kwako mkuu. Unakuwa kama hujakata shule ktk level hiyo ya chuo na ukasoma pale UDSM. Labda ndio walewale kamlete umesoma nchi za nje na sasa unataka kufananisha na UDSM. Uliza tuliosoma pale tukupe uzoefu wa pale ndio uanze hizo nyodo.

Kuandika neno lolote mtu yeyote awezakukosea hata wewe umekosea ukaandika iliyyotumiwa badala ya ilivyotumiwa. Yeye hasomei kuandika pale mkuu kuna vitu vingine vizito anasoma kuja kuwasaidia wewe na watoto na jamaa zako.

Tukirudi ktk mada halisi kwa kweli pale ni tatizo kubwa hatuombei maafa lakini maafa yawezatokea wakati wowote. Binafsi nimeishi pale Hall 5 nikiwa mwaka wa kwanza na nimejionea namna mambo yalivyobadilishwa mwaka huo wa 2003/2004. Chumba kilichokuwa na kitanda kimoja basi kikawekwa viwili nikimaanisha deki. Na zile side room za zilizokuwa na vitanda viwili zikawekwa vinne yaani deki mbili. Haya watoto wa mkulima nao wanaamua kubebana hawataki kutupana na kuacha wenzao wahangaike mjini kwa kukosa japo pa kuweka ubavu mmoja. Kwa hiyo room ya mtu mmoja ikabeba watu wanne na ile ya watu wawili ikabeba watu nane. Kumbuka makabati, bafu, vyoo nk havikuongezwa wala kuboreshwa inauma sana. Ktk chumba nilichokuwepo mimi ambacho ni side room ambaye sikualika mtu ktk kitanda changu ni mimi pekee hivyo tulikuwa saba. Nikajaribu kupeleka malalamiko nikaambiwa kama sitaki niondoke na wampe mtu mwingine. Yap baada ya miezi mitatu mkuu nikahama na kupanga mitaa ya Msewe maana mkitoka kuoga asubuhi ni kugonganagongana hapo ndani hapatoshi na hewa huwa ni nzito inayopelekea kuchoka na kusinzia wakati wa darasani.

Umeshauli kwamba matajiri wawezajitokeza na kujenga mabweni yap ni sawa yapo yale ya mabibo ni bomba lakini issue iko palepale. Utawala chuo walijitoa ktk hili na kuawaachia USAB walijua mambo hayaendi inavyotakiwa na idadi ya madent inazidi kupaa.

Nawapongeza waalimu hasa wa kitivo Engineering ni wachache lakini wengi wao wanafanya kazi ipasavyo japo ktk mazingira magumu ya ukosefu wa vifaa japo hawakemei hili swala la makazi wakijua wazi wakati wanasoma walikuwa hawajazani vyumbani kama sasa. Ufisadi unaanzia huku

Mungu saidia Hall sisidondoke na kutupotezea vichwa ambavyo Serikali imegharamia kuvikandaa na kuvikusanya pale.
 
Pundit take it easy man!
Lakini kusema ukweli hilo tatizo la kujieleza lipo, kama mtu ambaye natarajia kuingia kwenye job market soon, naambiwa waajiri wengi wanataka watu waliosoma nje kwa sababu wa UDSM kwenye kujieleza ni tatizo.
 
Pundit...nimekusoma mkuu.

Kujieleza kwa hawa wananzuoni ni shida kubwa...hasa hawa wanaosoma masomo ya sayansi..hawa weki juhudi katika lugha ambayo wanatumia katika kusoma..hasa kiingereza.Nimeona hawa wanaosome miamba...(Geology)wanaweza kutambua miamba lakini inapo kuja kwenye swala la kuwakilisha...kile walicho tambua inakuwa ni tatizo kubwa...hii inafanya baadhi hata ya nafasi wanaletwa wataalam toka nje ya nchi kuja kufanya kazi hii..

Amini kuna wanao maliza chuo wanakwenda kusoma english course pale British embasy hawa wanaakili kwa kweli..kwani wanajua.Kwani akisipo fanya hivyo mtu huyu mtamuona kituko,baadhi ya sehemu atakapo pewa nafasi ya kuongea watu wakiwa wamesubiri maelezo yake...ataongea kiswahili na kiingereza kwenye hadhara ya wanakijiji ambao hicho kiingereza hawakijui....wataalamu wa lugha wanasema kuwa "kama unaongea kiingereza na kiswahili,inamaa ligha zote mbili huzifahamu"
 
Kuna ripoti iliwahi kutoka kwa wataalamu wa chuo cha ardhi kuwa yale mahall yanazidiwa na idadi ya watu na maafa yanaweza kutokea....hii inasababishwa na wanafunzi kubebana kitanda kimoja 2.

Hiyo report ya chuo cha ardhi itakuwa ya kisiasa na si kitaalam. Chuo cha ardhi wao wanadeal na usanifu wa majengo kama utaniambia kuwa kulala wawili kunaaharibu mandhali ya majengo ntakubaliana na wewe. Ila ukitaka hasa structural issue na stability of buildings nenda CoET (Former Faculty of Engineering) pale ndiyo kuna wataalamu wa structure ( structural engineers) hawa ndiyo watakupa ukweli kama majengo yanaweza kuanguka ama la. Kuna kitu wanaita "design load" siku zote huwa ni more than "actual load", [ or they call margin of safety], kuepusha mambo kama haya ya overloading.
 
Pundit take it easy man!
Lakini kusema ukweli hilo tatizo la kujieleza lipo, kama mtu ambaye natarajia kuingia kwenye job market soon, naambiwa waajiri wengi wanataka watu waliosoma nje kwa sababu wa UDSM kwenye kujieleza ni tatizo.

Huu ni uongo wa kijiweni.

Watanzania hatuna shukrani na kile M/Mungu alichotujaalia. Ila naona watu wenye kukrihi wanazidi kuongezeka ktk thread.

Njoo hapa: Skilled – Recognised Graduate (Temporary) visa (subclass 476) ..

Huu ni mfano kuwa UDSM iko juu kwa sana tu ..ila hata Jesus alisema 'Nabii hutambulika isipokuwa nyumbani kwake'

Mmenikera sana 'wajuaji'

Nawaachia thread yenu.
 
Back
Top Bottom